Alex Fredrick
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 680
- 1,338
Tanzania toka Mwl JK Nyerere alipoondoka madarakani Nchi ilianza kuseleleka pasi na wengine kuelewa tunapoelekea.
Rushwa ilianza kutamalaki kuanzia ngazi ya chini mpka magogoni huku Viongozi tuliowapa dhamana kujifanya hamnzo kwa kuinua mabega juu,Wale tuliohoji tunakoelekea tuliambiwa tuache wivu wa kike.
Wafanyabaishara wakajipenyeza kwa wakubwa ili wapate kandarasi nono,Tukashuhudia rushwa ikimea kila uchao wafanyabiashara wakashika Nchi na Viongozi ndio tuliwapa dhamana ndio wakawa visemeo cha wafanyabiashara rejea pesa za Escrow.
Nchi ikashikwa rasmi na matajiri na Kandarasi zote zikawa zao huko Mahakamani Majaji na baadhi ya Mahakimu Tukashuhudia wakigaiwa pesa kama njugu.
Wanyonge wakatupwa rasmi na wakakosa sauti ndani yao Nchi (Viongozi na wafanyabiashara tu wakifaidi keki ya Taifa).
Rais Magufuli alipoingia madarakani aliliona hilo kwa kwa jina la Tai,kwahiyo maamuzi mengine anayofanya Mh Rais Magufuli yupo sahihi kabisa na apaswa kuungwa mkono.
Hizi kesi za wafanyabiashara zingekuwa zinaendeshwa kwa mfumo ule tuliouzoea hawa majizi sasa hivi wangekuwa nje maana wangehonga Majaji na Mahakimu kama walivyozoea hapo awali.
Na Hii haipo kwa Rais Magufuli tu ipo Duniani kote pindi Nchi inapokuwa hovyo na kupata Kiongozi sampuli ya Magufuli.
Na tusiombe siku Rais Magufuli afukue makuburi ya Epa,Escrow na mengine.Angola sasa hvi Edouardo Dos Santos anatapika pesa za Nchi yeye na familia yake huku akitolewa kinga ya kutoshtakiwa.
Bado tunamhitaji sana Rais Magufuli kwenye Nchi hii ili tuweze kupiga hatua kama Rwanda ya Paul Kagame
Alex Fredrick
Dar es salaam