Rais Magufuli wewe ni Rais wetu sisi sote Watanzania. IGP Sirro hafai ukiapishwa teua IGP mwingine

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
3,161
4,571
Mimi ni Mwana CHADEMA ila msema ukweli na ukweli unampa mtu uhuru.

Uchaguzi umeisha ila tumeshuhudia mambo mabaya sana hasa huko Zanzibar Pemba. Tumeshuhudia picha za maiti zikiwa zinatisha na ndugu wa marehemu wakisema ndugu zao waliuliwa na polisi.

Kwa jeshi linalofanya kazi kwa weledi sisi kama watanzania tulitakiwa tupate ukweli juu ya hizi picha na mauaji haya.

Niseme ukweli kuna mambo mabaya sana Polisi na vyombo vya usalama wanayafanya ila wanalindana na kuyaficha.

Tanzania ya leo sio ya miaka ya 70 ambayo watu walikuwa wanateswa na kufa mpaka Mzee Mwinyi akajiuzulu na viongozi wakuu wa vyombo vya usalama.

Niseme ukweli tu Polisi na vyombo vya ulinzi hawafanyi kazi kwa weledi sababu wakuu wao kama Sirro hawna weledi na sio wakweli. Leo hii ukiunda Tume huru utakuta 90% ya watanzania waliuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama bila makosa na Polisi walipotosha na kutoa ripoti za uongo.

Unaenda kumaliza awamu ya pili tafuta IGP ambae atawafaa watanzania na sio IGP kama Sirro ambae analinda makosa ya askari wanaoonea raia wasio na hatia.
 
Sawa Tumekusikia ila unaweza ukapendekeza IGP unaemtaka wewe ili utusaidie pakuanzia?
Wanamtaka Lema ili iwe full maandamano kila siku. Hopeless citizens upinzani gani huu?

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge nchi.

URT- JPM
SMZ- MWINYI

UCHAGUZI UMEISHA SASA TUIJENGE NCHI
 
Kwangu mimi askari wetu wakiteka au hata kuuwa najua ni hao watu waliotekwa au hata kuuliwa kama ikibidi ni watu wabaya na wanastahili, kwani Askari wako kwa ajili ya kutulinda Watanzania, BTW sijui chochote khs habari za kuuliwa au kutekwa mtu.
 
Huyo unae muomba amuondoe IGP Sirro si ndio aliomtuma kufanya kazi hio huko Zanzibar. Kesi ya nyani unampelekea tumbili.

Tusali, Tufunge na Tumuombe Mungu tu "laana/fedheha/adhabu/mateso/maradhi" yawafikie kila alietoa maelekezo, aliesababisha, aliehusika na aliefurahia kuuliwa kwa watu wasio na hatia.
 
Kwangu mimi askari wetu wakiteka au hata kuuwa najua ni hao watu waliotekwa au hata kuuliwa kama ikibidi ni watu wabaya na wanastahili, kwani Askari wako kwa ajili ya kutulinda Watanzania, BTW sijui chochote khs habari za kuuliwa au kutekwa mtu.
Ni kweli askari wa Tanzania, Wana kazi kubwa sana ya kuwalinda wananchi hasa watawala lakini mbona maisha yao hamyajari kabisa, kwani ukipita kwenye vibanda vyao wanavyoishi, huwezi amini kabisa! Zamani walikuwa hawalipii umeme kabisa, lakini sasa hivi kila mtu na mita yake!

Daaa, na awamu hii waliokuwa wana wasemea japo kidogo huko bungeni ndio, hivyo tena! Wamebakia yatima!! Japo walikuwa wana jiriwaza na pombe za nusu bei kwenye makambi yao, awamu hii hakuna! Ila wanatumikaa!
 
Ni kweli askari wa TZ, Wana kazi kubwa sana ya kuwalinda wananchi hasa watawala lakini mbona maisha yao hamyajari kabisa, kwani ukipita kwenye vibanda vyao wanavyoishi, huwezi amini kabisa!!! Zamani walikuwa hawalipii umeme kabisa, lakini sasa hivi kila mtu na mita yake!!!! Daaa, na awamu hii waliokuwa wana wasemea japo kidogo huko bungeni ndio, hivyo tena!!! Wamebakia yatima!! Japo walikuwa wana jiriwaza na pombe za nusu bei kwenye makambi yao, awamu hii hakuna!!! Ila wanatumikaa!!!

Maisha ya askari wa Tanzania yanaendana na mazingira ya Mtanzania, wote sisi tunaishi hivyo kama askari wetu pia, ...
 
Walaaniwe wote wauwaji na walioficha taarifa,ajabu hata siku ya kuapishwa bwana yule hakusema lolote juu ya wahanga!!!! Tumetengeneza bomu baya la chuki tusubiri mavumbi na misiba.
 
sawa
9b7d929a33e943ea9b42aa13b3883056.jpg
 
Wanamtaka Lema ili iwe full maandamano kila siku. Hopeless citizens upinzani gani huu?

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge nchi.

URT- JPM
SMZ- MWINYI

UCHAGUZI UMEISHA SASA TUIJENGE NCHI

Hatujengi nchi kwa kushirikiana na wezi wa kura. Kila mtu apambane na hali yake.
 
Walaaniwe wote wauwaji na walioficha taarifa,ajabu hata siku ya kuapishwa bwana yule hakusema lolote juu ya wahanga!!!! Tumetengeneza bomu baya la chuki tusubiri mavumbi na misiba.
Binadamu tutasahau kishatendewa mema tutasahau kila kitu ndio faida ya binadamu. Mabaya hayo hayatatokea Nchini kwetu kwa Jina la Mungu mwenye Rehema. Usiombee mabaya nchi yetu Maneno yako yasifanikiwe na yakafutikie Baharini na Tanzania itaendelea kuwa ya Amani. Bila Covid19.
 
Hatujengi nchi kwa kushirikiana na wezi wa kura. Kila mtu apambane na hali yake.
Basi laleni majumbani kwenu....barabarani acheni yatembee magari.

Nchi tutaijenga wazalendo wa nchi hii na tupo wengi.

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge nchi

URT- JPM
SMZ- MWINYI

UCHAGUZI UMEISHA SASA TUIJENGE NCHI
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom