Rais Magufuli wembe uliotumbua rafiki yako Kitwanga,ugeuze upande wa pili umtumbue mkuu wa mkoa wa Morogoro

lingamba lidodi

JF-Expert Member
Nov 15, 2018
965
1,000
Habari familia ya jf.
Mh Rais,watu wa Kilosa watafurahi sana kama WEMBE ule uliotumia kumtumbua jipu KITWANGA ugeuze upande wa pili umtupumbu jipu mkuu wa mkoa wa morogoro Steven kebwe.

RC huyu ni jipu linafurumia halihitaji WEMBE mkali maana liguswa hata na WEMBE ulotumika linapasuka
Hivi karibu kebwe alipewa jukumu na Katibu mkuu wa ccm,baada ya kusikiliza matatizo ya wakulima kuporwa mashamba yao zoezi lililoongozwa na afisa tarafa ya Magole ndugu nchimbi na kundi lake, la kuchukua hatua dhidi ya afisa tarafa ya Magole ndugu nchimbi, kwa tuhuma ya kuomba rushwa ya kulimiwa shamba na mkulima mmoja ili asiligawe shamba la mkulima huyo kwa Rafiki zake.

Rc kebwe alihaidi kufanya hivyo,na papo hapo alimsimamisha kazi Ndg nchimbi ili kupisha uchunguzi.

Kumbe Rc kebwe alikuwa anafunika Kombe mwanaharamu apite.
Rc hakuunda tume ya uchunguzi,kama haitoshi afisa tarafa nchimbi bado yupo kazini.

Sasa imefahamika na kudhihirika wazi kuwa nyuma ya uporaji mashamba ya wanyonge yupo mkuu huyo wa mkoa ndugu kebwe.

Mh Bashiru Rc kebwe anawaumiza sana wananchi wa tarafa za kimamba na Magole kwa maslahi yake.
Wananchi walihisi kuwa DC ndiye jipu,kumbe ni Rc.

Mh Rais komesha uozo uliopo wilaya hiyo kwa kuwatumbua RC NA DC ILI WENGINE WATAKAOKUJA KUWATUMIKIA WANA MOROGORO WOTE WAOGOPE.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,610
2,000
Kitwanga hakutendewa haki. Msimtie kichwa rais wetu Magufuli kufanya maamuzi yoyote ya utumbuaji kwa pupa na papara bila kufanya uchunguzi.

Scenario ya kutumbuliwa Kitwanga ni tofauti kabisa na scenario ya huko Moro, hivyo kumtolea Kitwanga mfano huo sio kumtendea haki.
Tuendelee kumsisitizia rais wetu atende haki, kama ni utumbuaji atumbue tuu kwa haki.
P.
 

masara

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,722
2,000
Kitwanga hakutendewa haki. Msimtie kichwa rais wetu Magufuli kufanya maamuzi yoyote ya utumbuaji kwa pupa na papara bila kufanya uchunguzi.

Scenario ya kutumbuliwa Kitwanga ni tofauti kabisa na scenario ya huko Moro, hivyo kumtolea Kitwanga mfano huo sio kumtendea haki.
Tuendelee kumsisitizia rais wetu atende haki, kama ni utumbuaji atumbue tuu kwa haki.
P.
Hivi kati ya Kitwanga na yule aliyesema madai ya waalimu ni bilioni 48+18b=1bilioni..
Nani alikuwa maji zaidi na anastahili kutumbuliwa?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom