Rais Magufuli, wazungu hawaepukiki tusijidanganye. Wasikilize watanzania waliokuchagua

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,617
34,061
Habari,

Nadhani wote tunajua ni zaidi ya miaka mitatu sasa tangu Magufuli achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania.

Ndani ya muda huu Tanzania imekuwa na mahusiano mabaya sana na nchi za wazungu kutokana na matendo na maamuzi ya Rais Magufuli.

Tanzania ni mali ya watanzania, hivi wazungu wanakosea nini kukwambia uheshimu taratibu tulizojiwekea wenyewe na wewe uligombea uongozi ukijua zipo tena ni kwa faida ya watu wako waliokuchagua ??!

Kabla hujagombea uliona kabisa urais ni mzigo, kuna kukosolewa, kutukanwa, kuzodolewa na kulalamikiwa na watu wanaokulipa mshahara na kila kitu, sasa kama ulijua huwezi kuvumilia hayo ni kwanini uligombea, maana siyo lazima ?

Leo wachina wanakujua kuwa huna altenative na watakuburuza sana kwa mikopo isiyolipika na bond za raslimali, huna tena pa kukimbilia ?
 
Habari,

Nadhani wote tunajua ni zaidi ya miaka mitatu sasa tangu Magufuli achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania.

Ndani ya muda huu Tanzania imekuwa na mahusiano mabaya sana na nchi za wazungu kutokana na matendo na maamuzi ya Rais Magufuli.

Leo wachina wanajua huna altenative watakuburuza tu kwa mikopo isiyolipika na bond za raslimali maana wanajua huna altenatives, huna tena pa kukimbilia ?
Kwa hiyo tuendelee kuwanyenyekea mabeberu wa kizungu badala ya Wachina?.
Hata Nyerere alikataa, Rais Magufuli usikubali, shikilia msimamo. Tz tusikubali misaada na mikopo yenye masharti kuingilia sovereignty yetu - JamiiForums

P
 
Habari,

Nadhani wote tunajua ni zaidi ya miaka mitatu sasa tangu Magufuli achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania.

Ndani ya muda huu Tanzania imekuwa na mahusiano mabaya sana na nchi za wazungu kutokana na matendo na maamuzi ya Rais Magufuli.
Siyo wajomaba wale, ni maslahi tuu ndiyo yanawaleta Tanzania, kama hakuna chao wanasepa.
Tanzania ni mali ya watanzania, hivi wazungu wanakosea nini kukwambia uheshimu taratibu tulizojiwekea wenyewe na wewe uligombea uongozi ukijua zipo tena ni kwa faida ya watu wako waliokuchagua ??!

Mbona unajichanganya, mara Tanzania ni ya Watanzania mara unataka wazungu wamwambie Rais cha kufanya, hivi uko sawa wewe?
Kabla hujagombea uliona kabisa urais ni mzigo, kuna kukosolewa, kutukanwa, kuzodolewa na kulalamikiwa na watu wanaokulipa mshahara na kila kitu, sasa kama ulijua huwezi kuvumilia hayo ni kwanini uligombea, maana siyo lazima ?
Utakuwa umebanwa mahali wewe, si bure.
Leo wachina wanajua huna altenative watakuburuza tu kwa mikopo isiyolipika na bond za raslimali maana wanajua huna altenatives, huna tena pa kukimbilia ?
Mbona amewahi kukataa mikopo ya china?
 
pascal saa nyingine unajitoa ufahamu hawa wachina pia sio watu wazuri bure inagarama.
utakuja kuona matokeo baada ya mda. kampuni za watanzania zinaenda kufilisika tender nyingi watachukua wachina, na mchina kwenye kazi bora mzungu. mchina hana huruma na vibarua(waTanzania wenzako)

mchina haangalii uwe dikteta usiwe anakusaidia ila mwisho wa siku tutalia.

na hapo tumechokoza mabeberu tumeegamia china bila kificho.

jk aliweza kung'ata nakupuliza huyuu ni pupa tuu, mara donor country mara makinikia yani hamna kitu anafanya kinachoeleweka.
 
Nyerere alikuwa na ushawishi mkubwa sana NAM ( China, Russia, Cuba, ....) ndio maana alisumbuasumbua.

Sasa huyo Magufuli ana kipi cha kujivunia.?

Akishindwa kujifunza kwa yaliyomtokea MUGABE ataumia sana.

Hata hivyo ni jambo gani gumu hasa kufanya wanalotaka wazungu mpaka apate tabu kuuubwa kulitekeleza ?

Imagine pesa za kusomesha wasichana wanapata ujauzito hutoi wewe, wajawazito hawakai wala kula kwako sasa roho mbaya na katili anayowafanyia anapata faida gani ??
 
Habari,

Nadhani wote tunajua ni zaidi ya miaka mitatu sasa tangu Magufuli achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania.

Ndani ya muda huu Tanzania imekuwa na mahusiano mabaya sana na nchi za wazungu kutokana na matendo na maamuzi ya Rais Magufuli.

Tanzania ni mali ya watanzania, hivi wazungu wanakosea nini kukwambia uheshimu taratibu tulizojiwekea wenyewe na wewe uligombea uongozi ukijua zipo tena ni kwa faida ya watu wako waliokuchagua ??!

Kabla hujagombea uliona kabisa urais ni mzigo, kuna kukosolewa, kutukanwa, kuzodolewa na kulalamikiwa na watu wanaokulipa mshahara na kila kitu, sasa kama ulijua huwezi kuvumilia hayo ni kwanini uligombea, maana siyo lazima ?

Leo wachina wanajua huna altenative watakuburuza tu kwa mikopo isiyolipika na bond za raslimali maana wanajua huna altenatives, huna tena pa kukimbilia ?

Alijua urais ni kama unyampara! Aachwe apambane na hali yake.
 
Siyo wajomaba wale, ni maslahi tuu ndiyo yanawaleta Tanzania, kama hakuna chao wanasepa.
Kwahiyo wachina ndo wajomba na hawajali maslahi yoyote ?

Mbona unajichanganya, mara Tanzania ni ya Watanzania mara unataka wazungu wamwambie Rais cha kufanya, hivi uko sawa wewe?
Tumia akili, ninachosema ni Rais afuate taratibu tulizojiwekea wenyewe.
Unaumiza raia wako mwenyewe, hicho ndicho kichokupeleka IKULU ?

Utakuwa umebanwa mahali wewe, si bure.
Ni kweli mdogo wangu Akwilini kauawa na utawala dhalimu na katili, nikae kimya ?

Mbona amewahi kukataa mikopo ya china?
Kama alikataa kinachompeleka sasa hivi kwenda kulialia na kuombaomba ni kitu gani, wachina wamekuwa weusi ??
 
Nyerere alikuwa na ushawishi mkubwa sana NAM ( China, Rursia, Cuba, ....) ndio maana alisumbuasumbua.

Sasa huyo Magufuli ana kipi cha kujivunia.?

Akishindwa kujifunza kwa yaliyomtokea MUGABE ataumia sana.

Hata hivyo ni jambo gani gumu hasa kufanya wanalotaka wazungu mpaka apate tabu kuuubwa kulitekeleza ?
Nyerere alikataa kugeuka jiwe akaona in vizuri kung'atuka akamwachia Mwinyi .Mwinyi akakubali masharti maisha yakaendelea.pia wakati wa mwalimu watu walitibiwa bure mahospitalini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika.

At least Nyerere alikuwa anakiri akivurunda.

Huyu wa sasa ni MALAIKA aka MR PERFECT.
 
China anainukia kiuchumi labda kuliko taifa lingine duniani,hata Umoja wa Ulaya wanakopa China.
Kwa vyote vile China si muarobaini bali kimbilio la dharura kwa yale yenye mashiko.
 
Back
Top Bottom