Rais Magufuli: Wauaji Kibiti, Rufiji waombewe waokoke

Rais John Magufuli amewataka Watanzania wawaombee wanaofanya mauaji mkoani Pwani, waokoke ili wajue kuwa damu ya mtu ina thamani kubwa.

Ameyasema hayo (Jumanne) wakati akihutubia katika mkutano wake wa kwanza katika ziara yake ya siku tatu, mkoani Pwani.

“Niwaombe wananchi wa Pwani, msishirikiane na watu waovu, wanachelewesha maendeleo. Ndiyo maana huko Kibiti hata viwanda hakuna, hakuna imani ya dini inayosema watu kuuana,” amesema.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano si ya kuchezea kwa sababu mpaka sasa wauaji hao wameshaanza kuuona moto.

“Watanyooka, actualy wameshaanza kunyooka, kama wapo hapa wanaotusikiliza, wakapeleke salamu,” amesema na kuongeza;

“Niwaombe sana, tuwaombee hawa watu waokoke, ili wajue damu ya mtu ina thamani kubwa.”
Naomba kurlewa hapa wamenyooka vipi na wanauona moto vipi ilhali so far mashambuluzi ni upande mmoja na hatujasikia mtu kukamatwa?au ndio wale maiti okotwa zisizojulikana ndio majibu ya serikali?mwenye kuielewa kauli ya jemedari wetu anifafanulie maana mpaka sasa Sirro na vijana wetu wa usalama wameshindwa kutupa jawabu lenye matumaini kama la Amuri Jeshi wetu !
 
Kama maombi tumeomba sana juu ya mienendo ya kiongoz wetu. Kuna watu wangne wamefunga na kuomba ili mkuu wetu awe na hekima. Lakin juhud hazijazaa matunda. Mim sina mzuka kabxa wa kuwaombea wauaji wakat viongoz wetu bdo maombi hayajawafikia.
 
Kuna haja Amirijeshi mkuu atembelee Kibiti kuongoza mapambano na kuwatia moyo askari
 
Back
Top Bottom