Rais Magufuli: Wauaji Kibiti, Rufiji waombewe waokoke

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
32,821
2,000
Rais John Magufuli amewataka Watanzania wawaombee wanaofanya mauaji mkoani Pwani, waokoke ili wajue kuwa damu ya mtu ina thamani kubwa.

Ameyasema hayo (Jumanne) wakati akihutubia katika mkutano wake wa kwanza katika ziara yake ya siku tatu, mkoani Pwani.

“Niwaombe wananchi wa Pwani, msishirikiane na watu waovu, wanachelewesha maendeleo. Ndiyo maana huko Kibiti hata viwanda hakuna, hakuna imani ya dini inayosema watu kuuana,” amesema.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano si ya kuchezea kwa sababu mpaka sasa wauaji hao wameshaanza kuuona moto.

“Watanyooka, actualy wameshaanza kunyooka, kama wapo hapa wanaotusikiliza, wakapeleke salamu,” amesema na kuongeza;

“Niwaombe sana, tuwaombee hawa watu waokoke, ili wajue damu ya mtu ina thamani kubwa.”
 

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,935
2,000
Hahaha Hahaha
Yani ubabe, ujeuri na mikwara yote inaishia kwa wanafunzi wanaotiana mimba, ila wanaume halisi unapambana nao kwa maombezi
hahaha hahaha
haki yake bibi mzaa baba hii kweli ni nchi ya vi-maajabu
hebu wadau angalieni udhaifu uliopo kwa viongozi wetu, yaani kauli kama hii inaonesha woga mkuu.
ACHENI KUTAKA HURUMA PAMBANENI NINYI RAIA WANAKUFA
 

Odili

JF-Expert Member
Feb 8, 2015
1,755
2,000
Mara tuwaombee mara wamenyooka yani huyu rais haeleweki wala hatoi msaada kama amiri jeshi mkuu. Ubabe, kutotaka mashauriano na kukosa diplomasia ni tatizo kubwa sana ktk utatuzi wa migogoro hatari kama hiyo.
 

Kps chad

JF-Expert Member
Jan 10, 2017
539
1,000
Hata mm sipendi mauaji kbs. Ni ujinga tuu maana hata wanachokitaka hawasemi.
 

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,935
2,000
Wanafunzi wakitiana mimba wa kike anaharibiwa maisha wa kiume jela miaka 30
wawindaji wadogo ambao wanaitwa majangili wakimshambulia hata nguchiro jela miaka 20
wazururaji jela miezi 3 hadi 6
mafisadi ambao wengi wao ni wanasiasa (kama wakikutwa na hatia) kifungo cha nje miaka 3 na kufagia
MAJAMBAZI WAOMBEWE
[HASHTAG]#MadeInTanzania[/HASHTAG]
[HASHTAG]#ProudlyTanzanian[/HASHTAG]
 

runyaga

JF-Expert Member
Dec 23, 2013
506
250
Hahaha Hahaha
Yani ubabe, ujeuri na mikwara yote inaishia kwa wanafunzi wanaotiana mimba, ila wanaume halisi unapambana nao kwa maombezi
hahaha hahaha
haki yake bibi mzaa baba hii kweli ni nchi ya vi-maajabu
hebu wadau angalieni udhaifu uliopo kwa viongozi wetu, yaani kauli kama hii inaonesha woga mkuu.
ACHENI KUTAKA HURUMA PAMBANENI NINYI RAIA WANAKUFA
Mkuu vimaneno vidogo tu vinakutoa povu kiasi icho, ungejua kwanza hiyo kauli imetanguliwa na maneno gani sidhani kama povu lingekutoka kiasi icho
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,745
2,000
Tuache kuwaombea mabinti zetu wasiingie kwenye majaribu ya kupata mimba eti tuyaombee magaidi wauaji wakubwa huyu mzee vipi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom