Bb YangeYange
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 337
- 184
Leo nimdona kwenye TV mazishi ya Mzee Elinawinga aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Mwalimu Nyerere. Maelezo yaliyotolewa ni kwamba kiongozi huyo hadi mauti inamkuta alikuwa akipata pensheni ya shilingi 25 elfu kwa mwezi! Wapo watumishi wa serikali waandamizi na wale wa nafasi za chini waliofanya kazi kwa uadilifu mkubwa katika awamu ya kwanza na ya pili ambao wanaishi maisha ya dhiki sana ukilinganisha na wale waliostaafu baada ya Rais Mkapa kurekebisha na kuboresha mafao ya watumishi waliostaafu katika kipindi cha uongozi wake. Tokea kipindi hicho wastaafu serikalini wameendelea kupata pensheni nzuri zinazowahakikishia maisha mazuri wakisubiri Mungu awapumzishe na wale waliostaafu wakati wa Nyerere na Mwinyi wameendelea kuishi kwa dhiki. Nadiriki kusema kwamba kutokana na uadilifu wao mkubwa wamekaa kimya wakifa kiofisa na tai shingoni!
OMBI kwa Rais wetu Magufuli anayejali sana maisha ya wanyonge aangalie kwa moyo wa huruma wastaafu wote wa kipindi kile ambao pensheni walizopata na wanazopata kila mwezi ama kila baada ya miezi 3 ni ndogo mno ukilinganisha na walizopata na wanazopata watumishi baada ya marekebisho ya Rais Mkapa ambayo hayakuwagusa wastaafu wa Nyerere na Mwinyi.
Nawasilisha hili ukumbini hapa nikijua kwamba wapo mtakaounga mkono na hatimaye likamfikia Rais wetu msikivu wa sauti za wanyonge maana wastaafu hao ni babu, bibi, baba na mama zetu waliofanya kazi kwa uadilifu mkubwa bila kuota MAJIPU yoyote!