Rais Magufuli: Watendaji wangu wengine wana vichwa vigumu kama Kamongo!

Mh Raisi mbona tumezungumza Sana, na wabunge Bungeni wamezungumza Sana suala la wawekezaji kuikimbia nchi yetu ,Nadhan Muda umefika Sasa Mambo ya badilikeni hata kwa wafanyabiashara
 
hivi mtu atawezaje kuja, wakati wewe unashindwa kuwalinda, mara unawaita mabeberu? na tabia unazozieonyesha hadharani, nani atakuja....?
 
Mh Raisi mbona tumezungumza Sana, na wabunge Bungeni wamezungumza Sana suala la wawekezaji kuikimbia nchi yetu ,Nadhan Muda umefika Sasa Mambo ya badilikeni hata kwa wafanyabiashara
yaani anajifanya hajui au makusudi tu....?
 
Well watafute watu waliosomea fani mbali za management na kufaulu vizuri ideal wanaweza shauri namna sahihi za kuweza kuibadili idea into practice au vinginevyo wanunue huduma za management consulting firms.

Kwa wenzetu chief strategists wa kila wizara ni katibu mkuu, na hadi ufike hiyo nafasi si suala la mzaha kabisa ni lazima uwe na level 7 and above za strategic management competence, why so technically ndio watu wanaoendesha nchi pamoja na senior civil servants wote wanaosimamia idara zilizo chini yao.

Ndio maana uwezi kusikia viongozi wao wakilaumu hao watu kwenye siasa zao (pamoja na kwamba wanachagamoto za kutekeleza ilani za serikari tofauti) maana wote ni technocrats wanaojua kazi yao na ukipewa CV ni watu waliofaulu vizuri kuanzia shule za awali, halafu wameanza chini huko wilayani pengine kama ma DED and workded their way up with good performance.

Sisi wataalamu ni bomu watu wanateuana tu matokeo yake hawafikirii angle zote kabla ya kuamua namna gani sahihi ya kutekeleza jambo, let alone kuweza kulisimamia kujua wapi kinaendelea nini at any given date.
Huyu wetu ameteua makada na watu wanaoweza kutukana wapinzani wake kisiasa then anategemea technical issues ziwe handled na kada mwenye uzoefu tu wa kutukana wapinzani na utangazaji wa redio au mipasho?Mwalimu mwalimu tu saizi yake chaki huku kungine tuwahurumie tu
 
View attachment 1066960
Rais Magufuli amezungumza hayo akiwa Mkoani Njombe akiwahutubia wananchi wa maeneo kutokana na kero alizoambiwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke juu ya wawekezaji kupata usumbufu kutika TIC ambapo wanapelekea wawekezaji hao kuondoka na kwenda nyingine.

Mh Rais amemtaka Bi. Sarah Cooke kama kuna mwekezaji atakuja nchini Tanzania akazungushwa TIC au Waziri au Katibu Mkuu wa Wizara basi amemuomba Bi. Sarah Cooke kuchukua jina la huyo mtu na amfikishie yeye mwenyewe hilo jina ili naye amzungushe huyo anaewazungusha wawekezaji.

Mh Rais ameitaka TIC kubadilika kama ataona hawabadiliki chini ya Waziri Mkuu basi ataipeleka katika ofisi yake (Ofisi ya Rais) ili adili nao vizuri.

=======

Rais John Magufuli amesema baadhi ya watendaji serikalini wamekuwa vichwa ngumu, akiwafananisha na samaki aina ya kamongo.

Amesema kuna baadhi ya watendaji hawataki kuelewa na wamekuwa wakimuona mwekezaji kama adui badala ya kumwona rafiki na kuwataka kubadilika haraka.

Amesema hayo leo wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha majani ya chai katika kijiji cha Kabambe mkoani Njombe, ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mikoa mbalimbali.

“Kuna matatizo ya uwekezaji katika nchi yetu, saa nyingine inakuwa inakatisha tamaa kuja kuwekeza, mtu anapotaka kuja kuwekeza saa nyingine anapata shida, masharti ni ya ajabu ajabu, baadhi ya watendaji wetu wamekuwa ni matatizo katika uwekezaji.”

“Ninawaomba watendaji ndani ya serikali wabadilike, mtu anataka kuja kujenga kiwanda unamzungusha mpaka mwaka mzima. Yeye ana pesa zake anataka kujenga kiwanda hata mabati na ajira zitapatikana hapa, lakini watu wamekuwa na vichwa vigumu sana, nafuu vichwa vya kamongo. Hawataki kuelewa, wapo wawekezaji wamekuja hapa wamewekewa mikwara mpaka wakaamua kwenda nchi za jirani,” amesema.
Ninachoweza kucomment hapa ni "Like father, like son"! Halafu kuna kamsemo kengine pia kanasema "Waarabu wa Pemba wanajuana kwa vilemba.
 
A true and candid description of some of our people in government, as a result of which we're not viewed favourably by investors! Technocrats in government and some politicians need a lessons to prime their mindsets towards building our nation!
 
Magufuli yeye anajionaga bonge la kipanga,wakati korosho tu zimemshinda.
Hata suala la sukari aliingia kichwa kichwa akakwama. anawakoromea TRA wakati yeye ndiye alikuwa anashinikiza kupandishwa kodi, tena kodi lukuki. Wapinzani miaka yote mitatu ya Magufuli wamekuwa wakilalamikia biashara nyingi kufungwa lakini kauli yake daima ni WANAOFUNGA BIASHARA NI WAPIGA DILI. Na makada na mawaziri wake wamekuwa wakiimba wimbo huu. sasa Magufuli amebadilisha wimbo, wenye makosa ni TRA. kwa suala la korosho, wenye makosa ni wakulima ambao wanalalamika kwamba hawajalipwa, WANATAKIWA KUKAA KIMYA!!
Hukon ndiko kukwama kwa Jiwe.
 
Magufuli yeye anajionaga bonge la kipanga,wakati korosho tu zimemshinda.
Acha UONGO wa mchana! Zimemshindaje, kwani korosho hazIkununuliwa? Kwani hazibanguliwi? Hata juzi kafungua kiwanda cha kubangua hizo korosho wewe unasema zimemshinda! Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni HATA KAMA UNAMCHUKI BINAFSI.
 
Unaishi dunia gani wewe hadi hujui kama kamongo wa magogoni kashindwa kununua korosho?

Victoire

Back
Top Bottom