Rais Magufuli : Watanzania tujifunze kuheshimu sheria

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watanzania kuheshimu sheria mbalimbali za nchi ili kuepuka madhara yatakayotokana kwa kutoheshimu sheria hizo.

Akizungumza leo Kimara Stopover jijini Dar es salaam, wakati akiweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa njia nane wa barabara ya Morogoro kutoka eneo la Kimara hadi Kibaha mkoani Pwani, yenye urefu wa kilometa 19.2 na kugharimu shilingi bilioni 141.5.

“Watanzania tujifunze kuheshimu sheria, ukisogelea barabara hasa hifadhi ya barabara madhara yake ni umaskini, nataka kuwaambia wananchi waliobomolewa nyumba zao na wakiwemo ndugu zangu ni kwa sababu ya kutoheshimu sheria” alisema Rais Magufuli

Rais Magufuli, alifafanuwa kuwa Serikali ilitumia fedha nyingi kuweka alama za kuonesha hifadhi za barabara nchi nzima lakini kwa bahati mbaya baadhi ya wananchi hawakutii sheria na kuendeleza maeneo hayo ya hifadhi kwa kujenga nyumba za makazi ama za biashara.
 
Back
Top Bottom