johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,798
- 141,696
Hii kauli ya mh Rais Magufuli aliyoitoa leo pale Ikulu imenitia moyo sana na ni imani yangu viongozi wote iwe wa umma au wale wa kisiasa watakuwa wamemuelewa.
Ni pale tu viongozi wetu watakapotambua ukweli huu na kuukubali kwamba Watanzania siyo wajinga ndio kwa pamoja tutaweza kuliletea taifa letu maendeleo.
Mwisho nimkumbushe Tundu Antipas Lisu watanzania tunajua ruzuku ya Chadema ambayo ni kodi zetu ndio inayokuzungusha huko Ulaya ukilidhihaki taifa lako mwenyewe lakini ukumbuke kuwa Watanzania siyo Wajinga.
Maendeleo hayana vyama!
=====
Mambo ambayo Magufuli aliyaibua kuhusu uchunguzi wa jeshi la polisi
Kuacha maswali mengi yakiwa hayajajibiwa.
Rais Magufuli amesema, kitendo cha Jeshi la Polisi kutotoa taarifa kuhusu hatua inazochukua kuhusu matukio yanayotokea huacha maswali mengi ambayo hukosa majibu
"Mnatakiwa muelewe kwamba Watanzania sio wajinga wanafahamu, natolea mfano tulipata stori nyingi za maelezo, wameteka wazungu lilipokuja kumalizika lile swala limekuja swali zaidi, yule aliyetekwa alikutwa Gymkhana, watu wanajiuliza alifikaje pale? Baadaye tunaona aliyetekwa anakunywa chai na Mambosasa (Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam), maelezo hayapo," Alisema Magufuli
Rais Magufuli amesema Watanzania walitaka kujua hatua ambazo Jeshi la Polisi ilizichukua kwa watu waliokamatwa wakihusishwa kuhusika na tukio hilo, ikiwemo mtu aliyekamatwa akidaiwa kuwabeba watuhumiwa waliomteka Mo Dewji.