Rais Magufuli: Watanzania siyo wajinga

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
40,292
2,000
Hii kauli ya mh Rais Magufuli aliyoitoa leo pale Ikulu imenitia moyo sana na ni imani yangu viongozi wote iwe wa umma au wale wa kisiasa watakuwa wamemuelewa.

Ni pale tu viongozi wetu watakapotambua ukweli huu na kuukubali kwamba Watanzania siyo wajinga ndio kwa pamoja tutaweza kuliletea taifa letu maendeleo.

Mwisho nimkumbushe Tundu Antipas Lisu watanzania tunajua ruzuku ya Chadema ambayo ni kodi zetu ndio inayokuzungusha huko Ulaya ukilidhihaki taifa lako mwenyewe lakini ukumbuke kuwa Watanzania siyo Wajinga.

Maendeleo hayana vyama!

=====

Mambo ambayo Magufuli aliyaibua kuhusu uchunguzi wa jeshi la polisi

Kuacha maswali mengi yakiwa hayajajibiwa.

Rais Magufuli amesema, kitendo cha Jeshi la Polisi kutotoa taarifa kuhusu hatua inazochukua kuhusu matukio yanayotokea huacha maswali mengi ambayo hukosa majibu

"Mnatakiwa muelewe kwamba Watanzania sio wajinga wanafahamu, natolea mfano tulipata stori nyingi za maelezo, wameteka wazungu lilipokuja kumalizika lile swala limekuja swali zaidi, yule aliyetekwa alikutwa Gymkhana, watu wanajiuliza alifikaje pale? Baadaye tunaona aliyetekwa anakunywa chai na Mambosasa (Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam), maelezo hayapo," Alisema Magufuli

Rais Magufuli amesema Watanzania walitaka kujua hatua ambazo Jeshi la Polisi ilizichukua kwa watu waliokamatwa wakihusishwa kuhusika na tukio hilo, ikiwemo mtu aliyekamatwa akidaiwa kuwabeba watuhumiwa waliomteka Mo Dewji.
 
Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
12,322
2,000
Hii kauli ya mh Rais Magufuli aliyoitoa leo pale Ikulu imenitia moyo sana na ni imani yangu viongozi wote iwe wa umma au wale wa kisiasa watakuwa wamemuelewa.

Ni pale tu viongozi wetu watakapotambua ukweli huu na kuukubali kwamba Watanzania siyo wajinga ndio kwa pamoja tutaweza kuliletea taifa letu maendeleo.

Mwisho nimkumbushe Tundu Antipas Lisu watanzania tunajua ruzuku ya Chadema ambayo ni kodi zetu ndio inayokuzungusha huko Ulaya ukilidhihaki taifa lako mwenyewe lakini ukumbuke kuwa Watanzania siyo Wajinga.

Maendeleo hayana vyama!
Hahaha mzee wa kutwist na kugeuza mambo. Unatumia kauli ya rais kugeuza ili ionekane imeenda kwa wapinzani. Wkt kauli hiyo waliambiwa polisi tena mfano akatolewa Mo dewji.

Kaka nimekushtukia. Uache kuchukulia kauli za rais kuzitumia kunufaika kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
107,263
2,000

Kweli muongo haachi ASILI!

Mwenye Phd ya uongo.

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
38,374
2,000
Kauli yake ile imechangiwa na mijadala humu mitandaoni, kwamba anajua serikali yake haitoi majibu stahiki ya maswali mazito bali umma una hofu ya kuhoji hadharani. Humu mitandaoni ndio anaweza kupima uwezo halisi wa watu kuelewa mambo kwani ndiko hasa maswali chokonozo yalipo ambapo ukihoji huko mtaani lazima upigwe risasi au utekwe na kupotezwa mazima.

Kauli ile ni kama kampa kinga ya kujitetea Kabudi huko kwa wazungu pindi watakapohoji hayo malalamiko ya Lissu kwamba hata rais ameigiza hatua zikichukuliwe dhidi ya hayo matukio. Hiyo kauli tunaita janja ya nyani kula mahindi mabichi. Ni hivi haya matukio ya kutekwa, kupotezwa na risasi ni maagizo toka juu fullstop.
 
Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
7,395
2,000
Ni kweli sio wajinga, wooote mpaka wale wa korosho, mpaka wale wa "kodi ya kichwa", mpaka wale waunga "juhudi", mpaka wale wa bureu de change, mpaka wale wafungwa wa kisiasi, hakika mpaka Nape, Mwigulu na Bashe, na kama sikosei mpaka Edward!!!
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
107,263
2,000
Naam yumo humu Mkuu tena mfuatiliaji mzuri sana. Na hili linathibitishwa na kauli zake nyingi ambazo chanzo chake ni hapa jamvini.

Kauli yake ile imechangiwa na mijadala humu mitandaoni, kwamba anajua serikali yake haitoi majibu stahiki ya maswali mazito bali umma una hofu ya kuhoji hadharani. Humu mitandaoni ndio anaweza kupima uwezo halisi wa watu kuelewa mambo kwani ndiko hasa maswali chokonozo yalipo ambapo ukihoji huko mtaani lazima upigwe risasi au utekwe na kupotezwa mazima.

Kauli ile ni kama kampa kinga ya kujitetea Kabudi huko kwa wazungu pindi watakapohoji hayo malalamiko ya Lissu kwamba hata rais ameigiza hatua zikichukuliwe dhidi ya hayo matukio. Hiyo kauli tunaita janja ya nyani kula mahindi mabichi. Ni hivi haya matukio ya kutekwa, kupotezwa na risasi ni maagizo toka juu fullstop.
 
Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
10,243
2,000
Hahaha mzee wa kutwist na kugeuza mambo. Unatumia kauli ya rais kugeuza ili ionekane imeenda kwa wapinzani. Wkt kauli hiyo waliambiwa polisi tena mfano akatolewa Mo dewji.

Kaka nimekushtukia. Uache kuchukulia kauli za rais kuzitumia kunufaika kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu mpumbavu bado anafikiri Watanzania WOTE ni wajinga kama vibaraka wa ccm wanaowahonga chumvi na vibiriti!!haelewi kuwa kuna watanzania zaidi yahao! Ukiwapinga kwa hoja wanafikiri umetoka sayari ingine,hawaamini kama kuna watanzania wanaojitambua!
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,851
2,000
Hii kauli ya mh Rais Magufuli aliyoitoa leo pale Ikulu imenitia moyo sana na ni imani yangu viongozi wote iwe wa umma au wale wa kisiasa watakuwa wamemuelewa.

Ni pale tu viongozi wetu watakapotambua ukweli huu na kuukubali kwamba Watanzania siyo wajinga ndio kwa pamoja tutaweza kuliletea taifa letu maendeleo.

Mwisho nimkumbushe Tundu Antipas Lisu watanzania tunajua ruzuku ya Chadema ambayo ni kodi zetu ndio inayokuzungusha huko Ulaya ukilidhihaki taifa lako mwenyewe lakini ukumbuke kuwa Watanzania siyo Wajinga.

Maendeleo hayana vyama!
Kama watanzania wenyewe ndo hawa wasio na uwezo wa kutofautisha serikali na nchi-Basi cheo cha ujinga bado tunacho sana
 
Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,157
2,000
Hii kauli ya mh Rais Magufuli aliyoitoa leo pale Ikulu imenitia moyo sana na ni imani yangu viongozi wote iwe wa umma au wale wa kisiasa watakuwa wamemuelewa.

Ni pale tu viongozi wetu watakapotambua ukweli huu na kuukubali kwamba Watanzania siyo wajinga ndio kwa pamoja tutaweza kuliletea taifa letu maendeleo.

Mwisho nimkumbushe Tundu Antipas Lisu watanzania tunajua ruzuku ya Chadema ambayo ni kodi zetu ndio inayokuzungusha huko Ulaya ukilidhihaki taifa lako mwenyewe lakini ukumbuke kuwa Watanzania siyo Wajinga.

Maendeleo hayana vyama!

Hivi wewe una akili timamu kweli kwa hili andiko lako la kibashite? Listen n' listen good.
We ni sehemu ya utawala huu mnaowafanya Watz kuwa WAJINGA..!Hivi nani hajui kuwa Magufuli ndo anawafanya Watz kuwa wajinga? Unapofanya njama za kutaka kumwua Mhe. Tundu Lissu(MB)na baada ya jaribio hilo ku-fail Serikali ya Magufuli ikaanza kuwalaghai Watz kuwa wahusika ni WATU WASIOJULIKANA ambao hadi leo hawajakamatwa.
Hivi nani hajui kuwa SIKU 1 kabla ya jaribio la kumwua Lissu Rais Magufuli alitamka kuwa" UKIWA MSALITI KWENYE VITA HUTAKIWI KU-SURVIVE....". Baada ya Lissu kupigwa risasi,Rais Magufuli, Bunge na Serikali wamekataa kulipia gharama za Matibabu kwasababu za kipuuzi kabisa! Hapa haihitaji sayansi ya kurusha rocket angani kujua nani alihusika na huu uhuni....!!!
MO DEWJI ametekwa na kufichwa kwa siku kadhaa tunaambiwa watekaji ni Raia wa KIGENI baadaye tunaambiwa ameonekana katelekezwa kwenye maeneo nyeti ambapo ilipashwa watekaji wawe wamekamatwa.....lakini kwa Magufuli na Serikali yake wanatufanya mabwege wakasema walivosema.......Lakini Watz siyo wajinga hivo wanajua kabisa nani walimteka MO na for what reasons.....!

Leo hii kuna zaidi ya Wabunge 10 wa UPINZANI wako MAHABUSU KWA KESI ZA KUTENGENEZWA KWA MAELEKEZO TOKA JUU!!Lakini pia bado kuna Wabunge wa upinzani zaidi ya nusu wana kesi FAKE Mahakamani....Halafu Magufuli asivo na haya anasimama na kuwaambia Watz KUWA MAENDELEO HAYANA CHAMA......!!!Huu kama sio unafiki ni kitu gani??Huku sasa ndiko kuwafanya WATANZANIA KUWA WAJINGA....!
Watz na Watu wengine wenye Akili wanajua tukio la Lissu kuuliwa kilipangwa na ndo maana kule nje anasikilizwa anachokisema maana ni UKWELI MCHUNGU NA SI AJABU BUNGE LA CONGRESS LIMEMWALIKA LISSU KUHUTUBIA MWEZI WA 4 KIWA MTZ WA KWANZA KUPATA NAFASI KAMA HIYO....!!!!
Hata hii kufanya mabadiliko madogo ya BLM Mahiga kurudishwa NDANI na Kabudi kwenda NJE ni katika juhudi za kutaka KUKABILIANA NA TUNDU LISSU jambo ambalo halitasaidia lolote maana tayari Magufuli amefanya DAMAGE KUBWA SANA KWA TANZANIA hasa KIDIPLOMASIA na KIUCHUMI!

Twendeni tu lakini mwisho wa siku tutajua nani anayewafanya Watz kuwa Wajinga.....Time gonna tell..!!!
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,851
2,000
Ni kweli sio wajinga, wooote mpaka wale wa korosho, mpaka wale wa "kodi ya kichwa", mpaka wale waunga "juhudi", mpaka wale wa bureu de change, mpaka wale wafungwa wa kisiasi, hakika mpaka Nape, Mwigulu na Bashe, na kama sikosei mpaka Edward!!!
Bidhaa iliyouzwa hairudishwi unless iwe imenunuliwa na serikali ya ccm.Hata bombadia zikituleteea ungese tunarudisha tu
 
Mnyanyembe wa Mboka

JF-Expert Member
Feb 10, 2017
1,778
2,000
Hii kauli ya mh Rais Magufuli aliyoitoa leo pale Ikulu imenitia moyo sana na ni imani yangu viongozi wote iwe wa umma au wale wa kisiasa watakuwa wamemuelewa.

Ni pale tu viongozi wetu watakapotambua ukweli huu na kuukubali kwamba Watanzania siyo wajinga ndio kwa pamoja tutaweza kuliletea taifa letu maendeleo.

Mwisho nimkumbushe Tundu Antipas Lisu watanzania tunajua ruzuku ya Chadema ambayo ni kodi zetu ndio inayokuzungusha huko Ulaya ukilidhihaki taifa lako mwenyewe lakini ukumbuke kuwa Watanzania siyo Wajinga.

Maendeleo hayana vyama!
Lakini pia mkumbuke watanzania sio wajinga tunajua zilikuwepo camera mahala pale ...

Tunajua mahala pale pana ulinzi wa kutosha tunalijua hilo tangu 2010 ...

Pia kumbuka watanzania sio wajinga na huwa hatusahau yaliyo semwa ... Kwa sababu tulimsikia mchumia tumbo yule akithibitisha kuwa kulikua hakuna kamera mahala pale ...

Aibu yenu na hili mnalo halito waacha salama kwa sababu limeshikiliwa na mkono wa Mungu!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom