Rais Magufuli: Watanzania endeleeni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Korona. Sijazuia matumizi ya Barakoa!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,491
2,000
Ameyasema hayo akiwa St. Peters katika Ibada alipopewa nafasi ya kutoa neno.

3354F5E1-E6F3-4E7E-BB2D-1CDB1D4CBE1C.jpeg

DD2ED37A-A9AB-4AE7-B6FD-6705C3E880CF.jpeg


fe6d9709-7854-43d5-be3a-73069c99e147.jpg


VIDEO:

 

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,257
2,000
Tiyari ameanza kukubali taratibu, nilivyokuwa nasikia namna anavyozungumza Majaliwa kwenye Msiba wa Balozi kijazi nikajua kabisa anasafisha njia kwa Jiwe kukubali Corona ipo nchini na watu wanapaswa kuchukua taadhari

Mimi nashauri angehutubia Taifa moja kwa moja kuhusu hili suala linalogharimu maisha ya watu na siyo kujificha makanisani kutoa matamko ya chini kwa chini kwa Jambo serious kama hili
 

The Underboss

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,580
2,000
He is now coming to his sense.

Alikuwa anawasifia watu wasipovaa barakoa sasa akili inaanza kumrudia.

Alisema corona haipo sasa akili inamrudia kuwa huu msala upo na hauna utani.

Nimesikia sasa anakimbilia kwenye vita ya uchumi, eti hii ni vita ya uchumi, corona ni vita ya uchumi, uchumi gani? Kwamba wazungu wameanzisha corona kupambana na Tanzania, kwa uchumi gani iliyonao hadi western countries zote zinanzishe vita na ya kiuchumi na Tanzania? South Afrika, Nigeria na Misri wao watasemaje kama hii ni vita ya uchumi?
 

Abigail Nabal

JF-Expert Member
Sep 2, 2020
645
1,000
Wahanga wa cororna walitakiwa wawe traced na watibiwe eneo maalum sio kujichanganya hospital na wagonjwa wengine. Na pia ukishajua huyu ni mgonjwa wa corona unatakiwa atibiwe kwa tahadhari lakini imekuwa kinyume. Wagonjwa wa covid wametapakaa kwenye zahanati

Wafadhili ndio nao mmewajibu kwa nyodo, msaada wa corona ndo basi tena. Kkila mwananchi apambane kivyake.

Wale wazee wasio na hata hela ya kula wakiumwa wakimbilie wapi?

Serikali ya ovyo
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
4,435
2,000
Hapa ndipo nimejifunza kama watu ndani ya taifa hili tukiamua kusimama na kupigania haki zetu kwa pamoja hakika tungeshinda kila vita inayokuja mbele yetu.

Uoga ni dhambi, na dhambi huzaa mauti; tatizo letu tu waoga, wengine ni wavivu wa kusubiri mpaka wengine waanze, na wale wachache wasiojielewa wanaojipendekeza kwa watawala hata kama baadhi ya maamuzi ya hao watawala yanawaumiza mpaka wao.

Kwa hili niwapongeze viongozi wa dini kwa kuonesha njia na uthubutu, naamini sasa wameuona umuhimu wao katika kuongoza kondoo wao kwenye njia sahihi, na wajue pia, popote wanapochelewa kuchukua maamuzi sahihi, wanasababisha kuchelewesha ukombozi wa watanzania.
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,064
2,000
He is now coming to his sense.

Alikua anawasifia watu wasipovaa barakoa sasa akili inaanza kumrudia.

Alisema corona haipo sasa akili inamrudia kua huu msala upo na hauna utani.
Msiba ukiwa kwa jirani wala husikii maumivu, msiba ukiwa kwako sasa ukagusa ndugu, jamaa, rafiki yako ndiyo utajua jirani yako alipofiwa ilikuwaje?

Sasa wameguswa haswaa ndiyo wanazungumzia!

Tumtegemee Mungu bila kuchukua tahadhari, ni kumjaribu Mungu.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
30,692
2,000
Wahanga wa cororna walitakiwa wawe traced na watibiwe eneo maalum sio kujichanganya hospital na wagonjwa wengine. Na pia ukishajua huyu ni mgonjwa wa corona unatakiwa atibiwe kwa tahadhari lakini imekuwa kinyume. Wagonjwa wa covid wametapakaa kwenye zahanati...
Pia watu waliokufa kwa Corona wanazikana hovyo na kuongeza maambukizi mara dufu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom