Rais Magufuli, wapinzani na watanzania kwa ujumla tuchukue Panama canal kama "Case Study"

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,478
2,301
Panama canal (mfereji wa panama kwa kiswahili) ni mradi ulianza kujengwa mwaka 1881 na wafaransa lakini badae mradi ulisimama kuendelea kutokana na ugumu wa kazi husika Watalamu wanasema huu ndio ujenzi mgumu kuwahi kutokea tokea dunia iumbwe. Ugumu wa kazi kuna wakati ulipelekea vifo na hadi vifo. Badae wamarekani walikuja kuumalizia mradi huu mwaka 1904-1914 na kujilipa hadi mwaka 1999 walipourudisha kwenye serikali ya panama. Kwa sasa mradi huu umekuwa wa manufaa sana kwa panama katika kuchangia pato la Taifa na ajira kwa ujumla.

Hapa tunajifunza nini?
Kama walioanzisha mradi huu wangeogopa gharama leo hii kusingekuwa na panama canal wala kitu kinachoitwa mchango wa panama canal katika uchumi wa Panama.

Leo watanzania tuna umia kwaajili ya miradi mikubwa inayojengwa na Rais Magufuli lakini matunda yake tutayaona kesho au vizazi vijavyo.

Ukweli ni kuwa tumechelewa sana kwa sababu ya kuogopa gharama, angalia strigglers gorge imeplaniwa toka enzi za mwalimu eti leo ndio tunaanza. Waliokuwepo enzi za Nyerere waliogopa gharama, kaja Mwinyi, Mkapa na Kikwete hivyo hivyo.

Kama watanzania wa kipindi kile wangekubali kuumia sisi leo tungekuwa tunakula bata.

NAWEZA KUWA SIMKUBALI RAIS MAGUFULI KATIKA MAMBO MENGI LAKINI KATIKA HILI YA UJENZI WA MIRADI MIKUBWA NAMUUNGA MKONO. SHIME WATANZANIA WOTE TUMUUNGE MKONO
 
Sahivi mmeanza kuja na Maneno... eti "pamoja na kumpinga jiwe Kwa mambo mengi...."
 
Mimi mradi wa stiglazi goji nauogopa sana....Kuna dalili kuwa maji ya yanayotirirka Katika mto Kirombero,Ruaha na Rufiji yanapungua kila Mwaka! Tuombe Mungu maumivu haya yasitokee kwa kuwa itakuja kuwa kilio cha kusaga meno! Nishati ya kutegemea mvua ni risk sana!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom