Haikuishia Hapo
Member
- Jan 13, 2017
- 67
- 49
Ni mara baada ya kuhitimu elimu yangu ya chuo kikuu naingia mtaani kujishughulisha wakati huo nikisubir rehema za ajira kutoka serikalini naanza kwa kurudi kijijini kwa wazazi na kuomba shamba walau nijishikishe kwa kulima walau nafaka naandaa shamba mwezi wa saba na kung'ojea mvua za mwezi wa tisa Mvua zinagoma kushuka walau kidogo.
Naamua kuachana na shamba mwezi wa kumi na moja na kuanza kujishughulisha na kuosha magari lakini cha ajabu kila kunapokucha afadhari ya jana gari zinapungua kila siku hadi ikafika kipindi napata gari moja au hakuna kabisa sijui wanaosha wenyewe siku hizi.
Haikuishia Hapo nikaamua kuwa fundi viatu huku nikijifariji kuwa ajira zinaweza kuwa karibu kutoka, nimeshona viatu ,Malapa kwa muda lakini napo hali ikawa ngumu kila mtu pesa hakuna hata mia mbili ya malapa mtu inamuuma hadi anafunga waya.
Haikutosha nikaamua kuwa Dereva bodaboda ya jirani yetu aliyenionea huruma lakini cha ajabu hapa mtaani kwetu tupo wengi yaan hadi wateja ni wakugombania ila najifariji na kauri kuwa huwenda kuna ajira zinakuja....
Kinachovunja moyo ni kauli za viongozi wetu eti tujiajir wakati huo hizo kauli hazikuja mapema tusingesumbuka kwenda vyuoni kupoteza mamilioni ya mtaji ukizingatia ni pesa za wazazi na mkopo tutazilipaje ghafla hivyo?
Leo hii wanasema sisi walimu wa masomo ya sanaa hatuna chetu kwanini hakukuwa na taarifa mapema tutafute namna nyingine...
Rais naye bila huruma anasema wanaolaumu kuwa pesa hakuna ni wala rushwa na wapiga dili, hivi kweli mla Rushwa aje mtaani kulilia nini wakati kala vya kumtosha na ana akiba kwake ni lini atakuja mtaani kupiga kelele na sisi day worker
Kumbuka Si wewe mkeo wala Waziri mkuu ualimu uliwatoa kwenye dhiki iweje mtubanie sisi hiyo national cake. ...please. .! tukumbukane mhe Raisi. ..please. !
Kumbuka hakuna fisadi wala mpigadeal anayekosa sh 20000 ya kununua debe la mahindi ila ni sisi watoto wa masikini ....Hakuna fisadi anayeng'ang'ana na Jembe la mkono ila ni sisi ....hakuna fisadi anayeng'ang'ana na kupanda kwa gharama za maisha ila ni sisi masikini
Ombi langu:
Naomba utukomboe na hili janga la ufukara walau kwa kutupatia hizo ajira za serikalin ili tulipe mikopo ya Ada na kuwaokoa wazazi wetu na mizigo ya madeni.
Tuonekane na sisi tunadhamani katika jamii na elimu zetu
Mwisho natoa shukrani kwa viongozi wote wanaohusika na suala la elimu na ajira za walimu kwa kubadilisha matamko kila kukicha Asante....