mitindo huru
JF-Expert Member
- Apr 26, 2016
- 1,610
- 1,601
Halotel - Viettel ni moja kati ya kampuni ya mawasiliano iliyowekeza hapa nchini. kama nchi tunajivunia muwekezaji huyu lakini nyuma ya pazia kuna mengi mabaya yanayofanywa na uongozi wa kampuni hii kwa wadogo zetu na ndugu zetu wanaofanya na waliowai fanya kazi katika kampuni ya Halotel.
Kampuni ya Halotel inayomilikiwa na wavietnum imekuwa inanyanyasa sana watanzania kwa namna nyingi.
Leo nitaongelea swala la mifuko ya hifadhi ya jamii. wengi wa waajiriwa katika kampuni hii makato yao ya mishahara hayapelekwi kwenya mifuko husika ya jamii hasa GEPF. Ifahamike kuwa kampuni hii imekuwa na mtindo wa kufukuza wafanyakazi bila utaratibu maalum unaweza ukawa umetoka nyumbani asubuh halafu bila taarifa yeyote ya awali unaambiwa na mkurugenzi hauna kazi, na kipindi unafanya kazi mshahara wako ulikuwa unakatwa ela ya mifuko ya hifadhi ya jamii.
Mh Raisi JPM tunaomba msaada wako katika hili ili tuweze kupata stahiki zetu kwani baada ya kufukuzwa kazi tumekuwa tukiishi maisha magumu sana tukifatilia mafao yetu mfuko wa hifadhi ya jamii GEPF bila mafanikio.
GEPF sio wa kweli kwa kuwa wanajua kwamba kampuni ya Halotel haipeleki michango katika huo mfuko, lakini hao GEPF wamekuwa wanatoa taarifa za uongo kwetu tukifatilia stahiki zetu.
Utaratibu na sheria ni kwamba endapo mwanachama ameachishwa kazi ana haki ya kupata mafao yake endapo akiitaji na ni siku saba za kazi baada ya kujaza form zao. Lakini kwetu ni tofauti kwani tunadhurumiwa na kunyanyaswa na Halotel wakishirikiana na mfuko wa hifadhi ya jamii GEPF.
tunamashaka kwamba GEPF wanashirikiana na Halotel katika hili kwani wafanyakazi wake hawana ushirikiano nasi pindi tunapodai stahiki zetu za mafao, kwani wengi ambao tulijiunga na mfuko huu akaunti zetu za mafao zinaonesha hakuna mchango uliowai pelekwa na mwajiri ambaye ni halotel - viettel kwenda mfuko wa GEPF katika akaunti zetu za mafao.
Mh Rais tunaomba utusaidie ili tuweze kupata stahiki zetu za mafao ukizingatia kwa sasa hatuna kazi, kwani tumejaribu fatilia SSRA bila mafanikio. Mh Rais tunakuomba kupitia wizara ya kazi na ajira kuweza fatilia hili tatizo letu na kutatua kama ulivyotuahidi pindi ulipokuwa dodoma sikukuu ya wafanyakazi mei mosi kuhusu waajiri wasiopeleka mafao ya wafanyakazi katika mifuko ya hifadhi ya jamii hasa GEPF.
Kwani tatizo kama hili liko kwa wafanyakazi wa mitandao mingine pia kama vodacom kupitia kampuni wanayoitumia katika uajiri ya Elorink na wizara ya ajira na kazi inajua hilo.
Note
Hii ndio hali halisi Mh Rais na watanzania wote inayoendelea kati ya Halotel - Viettel na mfuko wa GEPF pia wenye nyongeza kuhusu hii hali katika mitandao mengine kama vodacom, Tigo, Airtel n.k waongezee kwani hii mada haina nia ya kuichafua halotel au GEPF bali ni kwa manufaa ya watoto na ndugu zetu waweze kunufaika na elimu zao ambapo wazazi walipata tabu sana kuwasomesha.