Rais Magufuli: Wafanyabiashara msiponunua Korosho kwa bei reasonable, Serikali tutanunua kwa siku mbili tu. Uwezo tunao!

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Rais John Magufuli akizungumza leo na wanunuzi wa zao la Korosho katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kutoa msimamo wa Serikali kuhusu bei ya Korosho kuwa isipungue Sh3000 kwa kilo moja.

Serikali tunaunga mkono wakulima kukataa bei ya korosho

Aliyekuwa anawatisha wakulima waliokuwa wanagomea bei, tumemuondoa

Korosho lazima itanunuliwa, eidha inunuliwe na wafanyabiashara au itanunuliwa na Serikali. Lazima inunuliwe kwa bei inayoeleweka

Wafanyabiashara wa korosho tutaufungua mnada. Nasikia hamtaki serikali iwaingilie na Serikali haitaki Wakulima wapunje. Msiponunua tutanunua na fedha tunazo. Kama tunajenga reli tutashindwa kununua korosho?

Ukishalipa ushuru wowote katika Halmashauri moja, ukienda Wilaya nyingine hakuna kulipa ushuru. Mkulima asitozwe kodi mara mbili. Waziri mkuu na Waziri wa Wizara kasimamie hili.

"Serikali ina hela, inaweza kununua korosho za wakulima wa Lindi na Mtwara kwa siku mbili. Tumenunua ndege, tumejenga reli, hatuwezi kushindwa kununua korosho."

"Najua wafanyabiashara hamtaki serikali iingilie minada, basi mkanunue kwa bei ya zaidi ya shilingi 5,000."- Rais Dkt Magufuli

Rais Dkt Magufuli amefuta kodi ya asilimia 11 iliyokuwa ikitozwa na Bodi ya Korosho, na kuagiza bodi hiyo kurejea kwenye tozo ya mwaka jana ya shilingi 10. Amesema haiwezekani serikali inafuta kodi halafu bodi inaanzisha nyingine."

"Wafanyabiashara ni lazima waweke bondi wanapotaka kununua korosho, kwani wananchi wasipolipwa serikali ndiyo inalaumiwa na siyo wafanyabiashara"

"Kama tutaona Bodi ya Korosho ndio tatizo katika maisha ya wakulima wa korosho, itaondoka yote, hatutajali. Hivyo wafanyekazi kuhakikisha kuwa bei inakuwa juu."- Rais Dkt Magufuli

Rais Dkt Magufuli amesema atawaruhusu wafanyabiashara wa korosho kusafirisha bidhaa zao kwa kutumia Bandari ya Dar es Salaam, endapo tu watamhakikishia hawatazidisha uzito na kuharibu barabara wakati wakisafirisha korosho.

"Waziri Mkuu hakikisha Bodi ya Korosho iliyopo chini yako unaisimamia, kama mtu hafanyikazi fukuza hata kama ni kila siku, ili unusuru maisha yako. Mimi sioni shida ya kumfukuza hata Waziri Mkuu kama mambo hayaendi."

"Nawataka wafanyabiashara muelewe kuwa, hakuna korosho itakayouzwa chini ya shilingi 3,000. Kama hamtanunua, mniambie."- Rais Dkt Magufuli


======

Taarifa kwa vyombo vya habari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Oktoba, 2018 amekutana na wanunuzi wa zao la korosho na kutoa msimamo wa Serikali kuhusu bei ya zao la korosho kufuatia kuwepo kwa mvutano wa bei ya zao hilo kati ya wanunuzi na wakulima.

Mhe. Rais Magufuli amekutana na wanunuzi hao katika mkutano wa majadiliano uliokuwa ukiendelea kati ya wanunuzi wa korosho na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Katika msimamo huo Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inaungana na msimamo wa wakulima kukataa bei zilizotolewa na wanunuzi katika mnada uliofanyika hivi karibuni ambapo kampuni za ununuzi wa korosho zilitangaza kununua korosho kwa bei ya kati ya shilingi 2,717/= na shilingi 1,900/= kwa kilo ikiwa imeshuka kutoka zaidi ya shilingi 3,600 ya msimu uliopita.

Mhe. Rais Magufuli amesema endapo wanunuzi hao hawatakuwa tayari kununua korosho kwa bei isiyopungua shilingi 3,000/= kwa kilo, Serikali ipo tayari kununua korosho kwa bei yenye maslahi kwa wakulima na kutafuta masoko yenye bei nzuri.

“Kama hamtanunua korosho kwa bei yenye maslahi kwa wakulima, Serikali itanunua korosho kwa bei nzuri kwa wakulima na tutaihifadhi, nipo tayari hata kutumia majeshi yetu kununua korosho na tutatafuta masoko ya uhakika ili tuuze kwa bei nzuri” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Wakizungumza katika mkutano huo, wanunuzi wa korosho wamekubali kununua korosho kwa bei isiyopungua shilingi 3,000 kama ilivyoelekezwa na Serikali na wameomba baadhi ya tozo zinazosababisha kupungua kwa bei ya zoa hilo kwa mkulima ziondolewe pamoja na kuruhusiwa kusafirisha korosho kupitia bandari ya Dar es Salaam ambako wanaweza kupata meli zinazotoza gharama nafuu za usafirishaji wa korosho kwenda kwenye masoko ya nje ya nchi.

Mhe. Rais Magufuli amekubali kuondolewa kwa utozaji ushuru wa mara ya pili wa ushuru wa halmashauri uliokuwa ukifanywa baada ya korosho kufikishwa Mtwara, kupunguza ushuru wa Bodi ya Korosho kutoka shilingi 17/- hadi shilingi 10/- kwa kilo na ameruhusu wafanyabiashara kununua magunia yao wenyewe kwa ajili ya korosho badala ya kuuziwa na vyama vya ushirika kwa bei kubwa.

Kuhusu bandari ya kusafirishia korosho Mhe. Rais Magufuli amekubaliana na maombi ya wanunuzi kutaka kusafirisha korosho kwa kutumia bandari ya Dar es Salaam ambapo kilo moja inasafirishwa kwa shilingi 47/- kwa kutumia meli ambazo zimeleta mizigo mingine ikilinganishwa na bandari ya Mtwara ambako kilo moja inasafirishwa kwa shilingi 203/- kwa kutumia meli zinazokodiwa kwa ajili ya kubeba korosho tu.

“Bandari ya Mtwara na bandari ya Dar es Salaam zote ni bandari za Serikali, mimi sina tatizo na kusafirisha korosho kupitia bandari ya Dar es Salaam lakini na nyinyi muwe tayari kutozidisha uzito kwenye magari mnaposafirisha kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, kutotorosha korosho na pia kutimiza masharti ya usafirishaji” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Ameagiza Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuweka utaratibu mzuri utakaowezesha usafirishaji wa korosho hizo kupitia bandari ya Dar es Salaam kama ambavyo wanunuzi hao wameomba.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka wanunuzi hao kuwekeza viwanda vya kubangua korosho ama kuwahamisisha washirika wao kuja kuwekeza katika viwanda hivyo na kwamba Serikali itaunga mkono juhudi hizo ikiwa ni pamoja na kuweka vivutio vya kikodi.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

28 Oktoba, 2018
 
Nadhani tunarudi kwenye ujamaa!?, VP kuhusu bei elekezi 1500.... Atawajibisha wataalamu!? Iweje wakishindwa kufika bei hiyo!? Serikali yake ipo tayari kulipa wakulima tofauti!? Minada mingi ya mazao inaongozwa na mahitaji soko la dunia( Demand and supply)
 
Zitto ashamwambia izo korosho azinunue jiwe maana ndo amesabanisha! Kama mfuko wa export levy ungekuwepo ungeweza fidia tofauti (subsidise) sasa haupo na alouvunja kwa mbwembwe ni jiwe so yeye ndo anunue kwa wakulima kwa elfu 3 Alafu akauze kwa 2000. Unamwambia/unampangia bei mfanyabiashara halafu akapate hasara? Jamaa hajielewi
 
Back
Top Bottom