Rais Magufuli, waagize TAKUKURU waimulike Maxmalipo na waliopo nyuma ya kampuni hii

james msuva

New Member
Apr 12, 2016
4
40
MUENDELEZO MPYA

Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia kampuni yenye maksi nyingi katika malipo (Maxmalipo) kwa jinsi ambavyo imepeta sana chini ya uongozi wa awamu ya nne,Je ni nani na nini kipo nyuma ya pazia?

Nikiwa mtu ambaye nalenga kumsaidia raisi katika utumbuaji majipu ambayo bado yamejificha ningependa kuandika habari fupi kuhusu kilichofanyika Katika Tenda ya Tra ya Road licence.

Nikiwa Kama mfanyakazi makao makuu Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa takriban miaka nane kufikia October 2013 Kampuni yenye maksi nyingi katika malipo ilishinda dhabuni ya ukusanyaji wa kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania yenye namba AE/023/2013-14/HQ/G/001 Ambayo nimeambatanisha Nakala ya Mkataba huo hapa uliokuwa wa miaka miwili ambapo kufikia June 2015 ndio muda uliokuwa wa mwisho wa mkataba huu.

Kama ambavyo wengi mmekuwa mkisikia kampuni hii kuwa na mikono ya Baadhi ya watu wachache wazito nchini katika awamu ya nne baadhi wakiwa wameshatumbuliwa, ilipofika muda wa kutangaza Tender upya kutokana na sheria za PPRA nikiwa katika mchakato wa uandaaji wa mazingira ya Tender hii kwa mara ya pili ndipo ambapo nilishtuka nilipoona mabosi wangu wakiwa wana mpango wa kuongeza muda wa mkataba juu kwa juu bila kufuata sheria.

Niliandika barua moja kwa moja kwenda PPRA kuwatonya kuhusu kinachoendelea idarani kwangu (ambayo nimeambatanisha hapa kwenye thread hii) lakini kilichotokea ni kutumwa Barua Kutokea ngazi za juu magogoni iliandikwa na OS kuelekea TRA ikiamuru mkataba uongezwe pasipo kutangaza tender upya wala kusitisha makubaliano ya awali.

Nilipoonesha kufuatilia hili swala, nilipokea barua ya uhamisho moja kwa moja kutoka kituo changu cha kazi kwenda office za mpakani.

Naomba JPM, Uchunguze hili swala sina nia ya kurudishwa tena kazini ila na nia ya kuokoa upigaji wa pesa unaopitishwa kwa Matajiri hawa wanaonunua haki ya mtu na kutumia Pesa kwa ajili ya kunyanyasa wanaopigania haki na sheria Takatifu za Nchi yetu ya Asali.

Endlezo

Kabla ya kupokea uhamisho nilielezwa kwa kina na Mkuu wa kitengo changu ofisin kwamba nilipogusa(Kufuata sheria na taratibu) ni pabaya hivyo hakuna njia zaidi ya kuhamishwa eneo la kazi kuokoa kibarua changu, Nilipewa Maelezo mbalimbali jinsi ambavyo swala la kufuata sheria za ppra lilikuwa haliwezekani ikiwemo nakala za barua na memo mbalimbali zilizotoka juu kwajili yaku backup ukiukaji wa Taratibu huu ambapo baadhi ya barua na memo nilizo oneshwa (Nimeambatanisha Nakala ya Barua ya kwanza) iliokuwa ikitumika na Mkurugenzi wa kampuni kama reference toka juu kuzuia ufuatiliaji kwa wafanyakazi mbalimbali wa mamlaka waliotambua swala hili.

Pesa inayo kusanywa imekuwa ikutumika kuzungushwa na kampuni hii (karibia billion 9 mpaka billion kumi na moja ) imekuwa ikizungushwa kwenye biashara kwenye kampuni hii kinyume na makubaliano ya Tender ambayo ni kupelekwa kwenye account ya Tra kila bada ya siku moja ila mchezo uliotendeka ni Tra hupokea pesa kila baada ya siku 30 suala hili likiungwa mkono na vigogo mbalimbali ambao wamekuwa wakizungusha pesa kwa manufaa binafsi,

Hakuna Reconciliation ambayo imewai fanyika kama makubaliano wa kimkataba kati ya Tra na kampuni hii (Inayopelekea Tra kupokea tu pesa na kutoweza hakiki mapato halisi yanayopatikana kwenye ukusunyaji road licence).

Vigogo wengi wamekuwa wakizima wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato ambao wamekuwa wakitambua mchezo huu unaotia hasara Nchi yetu (kwa kuwafukuzisha au kuwahamisha eneo la kazi)

Muendelezo

kuna Maovu mengi yaliofanyika wakati wa michakato hii ikiwemo wafanyakazi wa mamlaka tumewatesa sana watanzania wengi kwa kuwambia mtandao haupo hivyo wakalipie maxmalipo kila siku ambayo hili swala liliendelea bahasha ilipitishwa moja kwa moja toka kwa mkubwa wetu kwa walioshiriki hili swala(Wafanyakazi Wa Mamlaka wanaelewa ni kwa jinsi gani nilikuwa nikipinga kazi hizi za kukusanya kodi zifanywe na private company wakati kuna team Za IT zilizoenda mafunzo nje ya nchi kutengeneza mifumo hii toka mamlaka nchi nzima,

Nime attach tender evaluation report ambayo ilitumika kupitisha kampuni hii, Ili vyombo vyote vijue kwamba michezo hii huwa inasukwa na Vigogo ambao siku zote huka nyuma ya pazia kasoro zilizopo ni zifuatavyo

1.Kampuni hii ilieleza mamlaka ina experience ya kufanya kazi hii kupitia kampuni waliopartner nayo inayoitwa LUCENTTECHNOLOGY LTD na mkataba wake ulikuwa na gharama za dollar million thelasini zaidi ya billion sitini za kitanzania kwa kuprovide national electronic identification system Ecuador lakini baada ya tender board kufanya utafiti ilionekana kampuni ya lucent haijawai kufanya kazi kama hio na nikampuni iliosajiliwa india kuuza magenerator na sio payment system na haina uhusiano wowote na maxmalipo

2. kampuni hii ilisema imefanya project ya smart licence project kenya lakini kulikuwa hakuna uthibitisho hata mmoja na majibu kuja kwamba swala lilikuwa la uongo. Baada ya Tender Board Kutia shaka swala hili kila mmoja alipokea simu kutishwa kuhusiana na wao kusign haraka kwa kutoa maksi nyingi kwenye tender iliokuwa na makampuni mengi ambayo sioni kama yote yalishinda Team ya Ndani ya Tra kufanya zoezi la ukusanyaji kodi yenyewe kwa kupewa resource zilizoitajika japo ukisoma tender report utajua nature ya kazi iliotolewa na kufanywa ni vitu viwili tofauti na siku zote mamlaka inatambua sekta binafsi ina umuhimu kwenye kuisaidia kukusanya kodi.

3.Sababu pekee mpaka leo reconciliation inapigwa chenga ni sababu aletea mada kama hizi utulizwa kwa vitita ndani ya mamlaka pesa inayoibiwa serikali

Rais wetu umeweka elimu bure pesa zinazoibwa kupitia mchezo huu ni nyingi na nyingi sana karibia billion mbili mpaka Tatu kwa miezi miwili utafiti ufanyike kwa kina kuhusu swala la hizi kampuni binafsi kufanya kazi ambazo zinawezwa fanya na mamlaka moja kwa moja (Vigogo wakiwa nyuma ya kampuni hizi)

Naomba ikumbukwe sijafichua haya kwajili ya kupata sympathy toka kwa mtu yeyote ila nia na dhumuni langu pekee nikumsaidia Mheshimiwa Raisi wa awamu ya Tano katika kutambua yanayotendeka nyuma ya pazia katika Taasisi zetu Serikalini kwa manufaa ya kila mtanzania.

Ni mimi Msema kweli.
 
Attachments

  • 9th July 2015_SEEKING_FOR_PPRA_ADVICE_FOR_CONTRACT_EXECUTION.PDF
    116.1 KB · Views: 216
  • 16th_July_2015_PPRA_LETTER_TO_TRA.PDF
    120.5 KB · Views: 215
  • 20150703 - TRA Contract for Electronic Tax Collection - Maxcom (1).pdf
    1.9 MB · Views: 421
  • Ikulu.pdf
    238.5 KB · Views: 214
  • CMVRS Tender Evaluation.pdf
    1.3 MB · Views: 228
Mambo mengine yanashangaza sana, hapa umetumika ujanjaujanja mpaka vikampuni vya wakubwa vimechomekwa katika mfumo wa ukusanyaji kodi. Ni kweli ukusanyaji wa kodi kwa kutumia njia ya kielektroniki hupunguza gharama za uendeshaji, lakini kwa mtindo huu tunatengeneza gharama nyingine bila sababu za msingi.
Kama unavyoona kwenye hili bandiko, watu wakubwa wameanzisha vitu vingine ambavyo havifai. Hivi vikampuni vimekuwa kama kupe, je TRA imeshindwa kununua technolojia yake kwa kutumia vyuo au wataalamu wetu?
 
Hmmmmm! huu ni uhuni na ufisadi wa hali ya juu. Kwani TRA wameshindwa kukusanya kodi wenyewe mpaka vikampuni mshenzi vya mafisadi vipewe mikataba ya kifisadi kukusanya kodi kwa niaba ya TRA? Ni nani wamiliki wa hii kampuni? Usikute kuna mtu ndani ya Ikulu ndiye mmiliki wa kampuni hii au alikuwa karibu mno na kingunge ndani ya Ikulu.
 
Kama kweli tunataka kuchunguza makapuni yote ya ukusanyaji kodi na vitu vinavyofanana tuanzie kote kote maana najua wote wameshika makampuni yote makubwa na ushindani mkubwa sana upo kati selcom,Maxcom na Techno Brain wamekatama TRA, TANESCO, Manispaa zote Dar, DAWASCO, NHIF etc! Kote huko wana mikono yao na inasemekana wakati wa tender rafu nyingi sana zilitokea kubakia walishindwa kulalamika kwa PPRA: Magu ana kazi sana! Inahitaji muda na weledi kupambana na ujanja wao!! Takukuru wana kazi miaka hii 5 maana uozo mwingi ma file yatajaa meza zao za uchunguzi hadi watapoteza mwelekeo! Mambo ni mengi sana! Tuwasaidie kuwapa info ili kazi iwe rahisi
 
Safi sana mzalendo ni wakati wa mabadiliko sasa tuliishi kimazoea na ubabe kuna baadhi ya vikampuni Vingi pembeni pembeni vilifunguliwa kwa minajiri ya kupiga hela na kunzengea zengea kodi zetu
 
...Nadhani katika utumbuaji wa mh.magufuli, na kwa hali hii amefanikiwa kwa only 30%,nikimaanisha madudu ambayo bado hayaoneka wala kuguswa mpaka sasa ni 70%.
*possibly upuuzi upo katika ngazi ya Juu,kati na chini.
KAZI IPO ///
 
ushauri wangu kwa raisi, atambue kuwa yapo mambo mengi yamefanyika nchi hii ambayo watumishi wengi wana ushahidi wa kila kitu lakini watu hawa hawajui ni wapi wanaweza kutolea ushirikiano.

wengi mtasema polisi wapo lakini na mimi nasema walikuwepo siku nyingi.

cha msingi ni kuona jinsi gani kinaweza kuundwa chombo ambacho kinaweza kukusanya taarifa hizi na kuzifanyia kazi.

na chombo hiki kiwe endelevu kwa maana ya wananchi kwa ujumla wakiona jambo ambalo hawariziki nalo kwa watendaji wa sasa ambalo hawasikilizwi basi hoja zinatumwa huko. cha msingi chombo hicho kitoe elimu ni mambo gani wananchi wanaweza kupeleka huko.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia kampuni yenye maksi nyingi katika malipo (Maxmalipo) kwa jinsi ambavyo imepeta sana chini ya uongozi wa awamu ya nne,Je ni nani na nini kipo nyuma ya pazia?

Nikiwa mtu ambaye nalenga kumsaidia raisi katika utumbuaji majipu ambayo bado yamejificha ningependa kuandika habari fupi kuhusu kilichofanyika Katika Tenda ya Tra ya Road licence.

Nikiwa Kama mfanyakazi makao makuu Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa takriban miaka nane kufikia October 2013 Kampuni yenye maksi nyingi katika malipo ilishinda dhabuni ya ukusanyaji wa kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania yenye namba AE/023/2013-14/HQ/G/001 Ambayo nimeambatanisha Nakala ya Mkataba huo hapa uliokuwa wa miaka miwili ambapo kufikia June 2015 ndio muda uliokuwa wa mwisho wa mkataba huu.

Kama ambavyo wengi mmekuwa mkisikia kampuni hii kuwa na mikono ya Baadhi ya watu wachache wazito nchini katika awamu ya nne baadhi wakiwa wameshatumbuliwa, ilipofika muda wa kutangaza Tender upya kutokana na sheria za PPRA nikiwa katika mchakato wa uandaaji wa mazingira ya Tender hii kwa mara ya pili ndipo ambapo nilishtuka nilipoona mabosi wangu wakiwa wana mpango wa kuongeza muda wa mkataba juu kwa juu bila kufuata sheria.

Niliandika barua moja kwa moja kwenda PPRA kuwatonya kuhusu kinachoendelea idarani kwangu (ambayo nimeambatanisha hapa kwenye thread hii) lakini kilichotokea ni kutumwa Barua Kutokea ngazi za juu magogoni iliandikwa na OS kuelekea TRA ikiamuru mkataba uongezwe pasipo kutangaza tender upya wala kusitisha makubaliano ya awali.

Nilipoonesha kufuatilia hili swala, nilipokea barua ya uhamisho moja kwa moja kutoka kituo changu cha kazi kwenda office za mpakani.

Naomba JPM, Uchunguze hili swala sina nia ya kurudishwa tena kazini ila na nia ya kuokoa upigaji wa pesa unaopitishwa kwa Matajiri hawa wanaonunua haki ya mtu na kutumia Pesa kwa ajili ya kunyanyasa wanaopigania haki na sheria Takatifu za Nchi yetu ya Asali.

Ni mimi Msema kweli
 
Back
Top Bottom