Rais Magufuli wa kazi, historia na fundisho

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Na Emmanuel J. Shilatu

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu Tanzania upande wa ngazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aambapo idadi ya waliopiga kura ilikuwa kura 15,091,950 ambapo kura halali ni 14,830,195 ambapo Mhe. John Pombe Magufuli wa CCM amepata kura 12,516,252 sawa na 84.4% huku anayemfuatia kwa mbaali akiambulia kura 1,933,271 sawa na 13.04%.

Nampenda kuungana na mamilioni ya Watanzania kumpongeza Mhe. Dk. John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi kuchaguliwa tena kwa awamu ya pili kuwa Rais wa Tanzania.

Ni ushindi wa kihistoria tangu kuanza mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1995. Historia inaonyesha aliyewahi kupata kura nyingi tangu mfumo wa vyama vingi uanze nchini alikuwa Hayati Benjamin Mkapa kwenye uchaguzi Mkuu mwaka 2000 ambapo alipata kura milioni 5.9 sawa na asilimia 71.7 ambapo mwaka 2020 Dk. Magufuli amevunja rekodi hiyo na zote kwa kupata kura zaidi ya milioni 12.5 sawa na asilimia 84.4 .

Ni ushindi mnono ulioutoa shimoni CCM ambayo kura zake zilikuwa zikipungua kila mwaka wa uchaguzi. Ambapo mwaka 2005 Mzee Jakaya Kikwete alipata ushindi 80.3%, mwaka 2010 kura zikapunguka akapata 63.8%. Uchaguzi wa mwaka 2015 uliomuingiza Dk. Magufuli madarakani CCM ilizidi kuporomoka kwa kupata ushindi wa 58.6%. Mwaka huu 2020 Mgombea wa CCM na Mwenyekiti CCM Taifa Dk. Magufuli amepata ushindi wa kishindo na wa kihistoria wa asilimia 84.4 , sitakosea nikisema Mwamba Dk. Magufuli ameitoa CCM shimoni na kuirudisha kwenye ramani.

Ni Watanzania ndio walioamua kuchagua kazi, historia, amani, haki, usawa na maendeleo ambayo wameona mwangaza wa upatikanaji wake kupitia Rais Magufuli, kupitia CCM kutoana na kuridhishwa na sera, ilani ya CCM.

Imani ya CCM imerudi kwa jamii kutokana na uadilifu, uzalendo, uchapa kazi, ufuatiliaji na ucha Mungu alionao Rais Magufuli ambaye amejitolea kwa dhati kabisa kuwa sadaka ya Watanzania ya kuwaletea maendeleo ambapo leo hii sisi Watanzania tunasomeka Duniani kote tumeingia kwenye nchi zenye uchumi wa kati. Hakika, Rais Magufuli ni jembe.

Ni ushindi uliojaa fundisho kwa wale wote wasiotutakia mema, wasiopenda amani tuliyonayo, wasiopenda maendeleo tunayoanza kuyaona kupitia kiongozi jasiri na shupavu, Dk. Magufuli.

Ni ushindi wa kishindo, fundisho na salaam Duniani kote kuwa tunaridhishwa na kuunga mkono mambo yote yanayofanywa na Rais Magufuli ya ukombozi wa kiuchumi kwani Tanzania ni tajiri na tunaweza kujikomboa sisi wenyewe.

Ni ushindi uliojaa fundisho kwa wale wanaotaka kutugawa ili watuvuruge kuwa Watanzania wa leo wameelimika sana wamejaa umoja, mshikamano na uzalendo kwa Taifa lao tukufu la Tanzania na wapo tayari kuilinda Tanzania na Rais Magufuli kwa gharama yeyote ile.

Kwenye uchaguzi wowote ule kuna kushinda na kushindwa, ni muhimu Wanasiasa na wagombea kuheshimu maamuzi ya Watanzania kama ambavyo zaidi ya Wagombea 9 wa nafasi ya Urais walivyokubali wameshindwa kihalali kabisa kwani muda wa uchaguzi na siasa umekwisha.

Ni muhimu kutambua pia kuna maisha baada ya uchaguzi. Amani tuliyonayo, maendeleo tuliyonayo, Tanzania tuliyonayo ni muhimu zaidi kuliko kitu chochote kile. Tuitunze Tanzania yetu kwani hatuna Tanzania nyingine.

Narudia tena kumpongeza Rais Magufuli kwa ushindi mnono, wa kihistoria na wa fundisho alioupata.

Mungu Ibariki Tanzania.

Shilatu, E.J
 
Ni uchaguzi wa ovyo sana.Tangu kuanza kuwaengua wapinzani.Harakati za Mahera kuwafungia waliobaki na sakata la mawakala na matumizi ya vyombo vya habari
 
Poleni mlioshindwa kwenye uchaguzi huu.

Sasa rejeeni kwenye hali zenu za kawaida baada ya mihemuko ya kushindwa. Mjiulize kwa makini mmekwama wapi na kisha kwa hekima na busara tafakari kwa namna gani mtajitoa hapo mlipo kwama na muanze sasa kuonyesha kwa vitendo kuwa hamtakwama tena kwa sababu sasa mtakuwa na ajenda yenye nia njema ya kuhakikisha Tanzania inazidi kuwepo vizazi na vizazi ikiwa imara na yenye nguvu katika kila nyanja ya maendeleo.

Niwatakie kila la heri na kwa mara nyingine na wapa pole ya dhati kabisa kwa kushindwa kwenu.
 
Ni uchaguzi wa ovyo sana.Tangu kuanza kuwaengua wapinzani.Harakati za Mahera kuwafungia waliobaki na sakata la mawakala na matumizi ya vyombo vya habari
Na wakurugenzi kupigwa mkwara wasitangaze mpinzani kashinda.
 
Poleni mlioshindwa kwenye uchaguzi huu.

Sasa rejeeni kwenye hali zenu za kawaida baada ya mihemuko ya kushindwa. Mjiulize kwa makini mmekwama wapi na kisha kwa hekima na busara tafakari kwa namna gani mtajitoa hapo mlipo kwama na muanze sasa kuonyesha kwa vitendo kuwa hamtakwama tena kwa sababu sasa mtakuwa na ajenda yenye nia njema ya kuhakikisha Tanzania inazidi kuwepo vizazi na vizazi ikiwa imara na yenye nguvu katika kila nyanja ya maendeleo.

Niwatakie kila la heri na kwa mara nyingine na wapa pole ya dhati kabisa kwa kushindwa kwenu.
Tulikwama kwenye tume huru,na katiba Mpya.
Ndo tumetafakari upya kilichotuangusha,asnte kwa ushauri wako kuwa tuchukue hatua.
Hatua tuliyoamua kuchukua ni kuamdamana kwa amani ili tupate haki yetu tuliyoporwa.kuanzia kesho jumatatu,chondechonde ndugu msitupige risasi maana hatutakuwa na silaha yoyote.ni maandamano ya amani kabisa .
 
Msisahau tuna sheria zinazotuongoza sisi watanzania. Tunahimizwa tuzifuate bila shuruti.
 
Huu ushindi niushindi wa watanzania wote.
ajashinda Magufuli wala CCM ni taifa kwaujumla limeshinda.
walioshindananae na wakashindwa ni sehemu ya ushindi wa taifa.
na wasiopiga kura na waliopiga kura wote ni sehemu ya ushindi.
#Rais wetu ni JPM na sisiwote na wananchi wake.
tuchape kazi kwa bidii,mafanikio yako yapo mikononi mwako,hayapo kwa CCM wala Chadema.
 
Back
Top Bottom