Rais Magufuli Vita yako dhidi ya wanyonge inaweza kuigharimu nafasi yako ya urais mwaka 2020

Nathason2

JF-Expert Member
May 20, 2015
598
680
Habari kwenu wana JF

Kwa muda mrefu Raisi wetu mpendwa amekuwa akijimbanua kama mtetezi wa wanyonge na Yale ayafanyayo anayafanya kwa faida ya wanyonge watanzania.ki ukweli kundi hili ndilo kundi kubwa kuliko makundi mengine hapa kwetu Tanzania.

Kwa muda mrefu nimechunguza haya mapambano ya Mh Rais na nimejiridhisha kuwa kwa sehemu kubwa ni mapambano dhidi ya wanyonge na hayalengi kuwasaidia au mambano yenyewe yanaishia kuwa athiri wanyonge.mathalani.

1.Mapambano dhidi ya waingizaji wa sukari yaliishia na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo hali ambayo ilituathiri wanyonge.

2.Hivi majuzi TCU wametoa majina ya wanafunzi 8,000 na zaidi wasio na sifa ya udahili ikumbukwe tu kwamba TCU ndilo waliwadahili na kuwapangia vyuo vya kusoma huku wakijua wanafunzi husika hawana sifa za kujiunga na vyuo vikuu raisi amebaliki maamuzi haya kwa kuwa yupo kimya mpaka sasa.

Sisemi atetee wanafunzi wasio na sifa la hasha ninachosema ni kwamba waliowatia hasara wazazi wa wanafunzi hawa wakalipa ada miaka mitatu badala ya kununua mbolea bado wapo pale TCU na raisi hana mpango wa kuwagusa kwa kuwa ni wateule wake. Hao watu elfu name ni kura untakazo zikosa 2020 kwa kuwa wanafunzi hao hawakujipeleka vyuoni Bali walidahiliwa na wateule wako.

3. Kupanda kwa makato ya HESLB pamoja na manyanyaso amvayo wateule wako wanawafania watumishi wa umma. kwenye ongezeko hapo napo umekaa kimya kama huoni labda nikukumvushe Mh raisi sehemu kubw ya hao watumishi wanalipa PAYE 30% HESLB 15% Hifadhi ya jamii 5%-10% bima ya afya 5% vyama vya wafanyakazi 5%-10% ukijumlisha more than 65% ya mshahara wa mtumishi mnabaki nayo

Anachokipata ni kidogo sana ukilinganisha na hali ya maisha ya mtanzania bado kuna wateule wako wamethubutu mpaka kuwapigisha deki walimu wakuu kuweka rumande watumishi n.k yote hayo yanakupunguzia idadi ya kura 2020.

4. Tatizo la ajira ni wewe ujuaye kitu ulicho kifanya lakini nakukumbusha tu hili nalo ni kundi lingine la wanyonfe amvalo kwa dhati kabisa umekusudia likunyime kura kwenye ychaguzi ujao. Serikali na vyombo vyake vyote ni kweli hamjakamilisha uhakiki wa watumishi hewa? Au umejiamulia kuwatenda hivo hao wanyonge unaowatetea.

5. Upungufu wa chakula kwa baadhi ya maeneo naona hauko serious kabisa umediliki kuwaambia ukweli wanyonge kwamva serikali haina shamba huwezi kuwapikia n.k nikukumvushe tu ni hero kukaa kimya kuliko kuwakasilisha wapiga kura wako ni kweli serikali haina shamba lakini njaa ni mbaya Huyo usema kwel utakugharimy huko mbele ya safari

6. Wahanga wa tetemeko.hapa wachangiaji wantakuwa na mengi ya kukulaumu muhimu kumbuka ni kura ngapi zinapotea

7. Bomoa bomoa sehemu kuna watu wanakulilia hapa Luna sehemu mahakama ilitoa amri ya kuvunja nyumbani 5 wavunjaji wakavunja 500 na zaidi na wewe mtetezi wetu upon kimya

Inafaa kukumbuka Rais aliyekutangulia aliingia madarakani mwaja 2005 akiwa na kura asilimia 81% ya kura zote baada ya utendaji wake wa miaka mitano kutowaridhisha wengi mwaka 2010 aluporomoka mpaka kupata kura sawa na aslimi 61% were umeingia na asilimi 57% na we wakwaza wanyonge anguko la asilimia kum tu litatosha kukuita rais mstaafu ni vyema ubadili mbinu ya mapambano bado una nafasi ya kufanya hivo.
 
Wapiga dili lazima muone Tanzania Chungu hebu nendeni Commoro mkajaribu maisha.


ba9e4dca11d61e1224fe583714827fdd.gif
 
Unahuburi wokovu kwa walio okoka! Huko aliko atakuwa kakuonyesha dole la Kati Na kwa taarifa yako unaitwa post uliyeanzisha thread.
I wish I could be ..........
 
Mi nilikuwa nampenda sana lkni yupo biased. Ukaguzi wa vyeti hujawai kuisha na watumishi hewa. Mishahara watumishi wa umma haikuongezeka.
 
  • Thanks
Reactions: ffq
Back
Top Bottom