Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,599
- 6,669
Rais John Magufuli amesema hatua anazochukua kwa ajili ya kuwasimamisha watumishi wa umma kazi zisitafsiriwe kama ni ukatili kwakuwa watumishi hao wamekuwa wakifanya mambo kinyume na maadili ya utumishi wa umma na kusababisha kuwadhulumu watanzania walio wanyonge kwa muda mrefu.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jijini ARUSHA wakati alipohudhuria ibada katika kanisa katoliki Prokia ya TOKEO LA BWANA, BURKA leo ikiwa ni ibada ya Kupaa Mbinguni kwa Bwana Yesu Kristo.
Akihuburi katika ibada hiyo, Padri Germin Longio, amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii kwani hata Yesu alifanya kazi yake na ndiyo maana Jumapili kama ya leo alipaa kwenda mbinguni baada ya kumaliza majukumu yake hapa Duniani.
Mwenyekiti wa parokia, Jonathan Mushi amesema watanzania wamuunge mkono Rais kwa hatua anazozichukua za kuhakikisha wanyonge wanapata haki zao ili kutoa matabaka ya walionacho na wasionacho.
Waumini wa kanisa katoliki parokia ya TOKEO LA BWANA BURKA wamemtangaza Rais MAGUFULI kuwa mwanaparokia wa parokia hiyo.