Rais Magufuli utaendelea kuiona kazi ya Urais kuwa ngumu, kwa kuwa huruhusu nchi iwe na taasisi imara

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,357
2,000
Nimekuwa nikimsikiliza Mara kwa Mara Rais wangu Magufuli, katika hotuba zake mbalimbali, anazotoa kwenye majukwaa ya kisiasa na Mara kwa Mara amekuwa akirudia kauli yake ya kulalamika na kusema kuwa kazi ya Urais ni ngumu sana na kama yeye angelijua hilo kabla, basi hata fomu ya Urais mwaka ule wa 2015 asingeenda kuchukua!

Nimekuwa nikatafakari sana kauli hii na kujiuliza hivi ni nini tafsiri ya kauli hii ya Rais?

Amekuwa pia akisema kuwa Mara kwa Mara amekuwa akienda na mafaili ya kazi hiyo ya urais, kwenye chumba chake cha kulala na amekuwa akikesha akifanya kazi hiyo ya urais

Nilichogundua ni kuwa kazi ya Urais siyo ngumu kivile kama ambavyo anavyodai Mheshimiwa Rais, lakini ni yeye mwenyewe anayeifanya kazi hiyo ya Urais iwe ngumu sana, kutokana na "hulka" wake wa kutaka kuifanya kazi hiyo ionekane kuwa ya "one man show" ndiyo tatizo kubwa

Hivi utawezaje kuona kazi ya Urais ngumu, wakati una taasisi nyingi zinazokusaidia kazi na hivyo kukurahisishia kazi yako?

Hivi katika nchi ambayo inaongoizwa na utawala bora, ambapo mihimili mitatu, ambayo ni Serikali, Mahakama na Bunge, ikiwa kila mhimili unafanya kazi yake kwa Uhuru bila kuingiliwa kati na mhimili wa serikali, utawezaje kuiona kazi ya Urais ngumu??

Nimsihi Rais wangu Magufuli ili ajiepushe na kuzeeka haraka, aruhusu kila aliyempa jukumu la kiutendaji, basi afanye kazi yake akiwa huru na yeye aingilie kati pale tu atakapothibitisha kuwa mteule wake "ameboronga" katika utumishi wake, lakini itakaootokea kuwa wewe mwenyewe Rais, una-wish You could be IGP, una-wish pia you could be CJ na pia una-wish You could be Speaker!

Huo si utawala bora na ni lazima "at the end of the day" utakwama na hutapata mtu wa kuja kukukwamua!
 

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
13,720
2,000
Kikwete aliwahi kusema, ukiwa Rais unaweza amuru mtu yeyote kukamatwa na atakamatwa tena kwa haraka na wakishamkamata watakufuta tena kukuuliza "tumfanyeje" hilo ndio tatizo kwa maana nyingine watumishi wengi wa umma hawana confidence, utendaji kazi wao unategemea utashi wa watu wengine. Unakuta wabunge hata kama jambo la hovyo ilimradi limeletwa na wa chama chao wataunga mkono tu na akibadili mawazo na wao wanabadilikia.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,357
2,000
eddy,
Ni kweli kabisa ulichoongea Mkuu Eddy, kuwa madaraka ya kiutendaji unayopewa wewe Rais ndani ya Katiba ya nchi, ni makubwa mno, kwa hiyo uki-abuse power yako, basi utawaamiza watu wengi sana ndani ya jamii
 

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,125
2,000
Mystery,

Hata baba wa Taifa Mwl. Nyerere aliwahi kusema kazi ya Rais sio kazi ndogo. Tunaona kwenye ma ofisi changamoto kubwa ya uongozi. Hata kwenye ndoa ni hayohayo na wengine ndoa zimevunjika na familia zimesambaratika.

Ndio maana Biblia inasema tuwaombee wenye MAMLAKA ili tuishi kwa AMANI. Hivyo kumuombea Rais Magufuli ni wajibu sio hiari.

Mwisho hebu tumuangalie Mungu na vita yake na Lusifa. Lucifa alitaka kumpindua Mungu ndipo akatupwa duniani. Huwa najiuliza kwanini Mungu hakuacha demokrasia ichukue mkondo wake?

Kuongoza watu ambao kila mtu ana akili zake sio mchezo. Kwenye HR wanakwambia the most difficult resource to hande ni human resource.

Queen Esther
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,180
2,000
Miezi kama minne iliyopita nilikua nahitaji kibali cha kukusanya maoni kuhusu issue Fulani, nikapeleka barua TAMISEMI baada ya week mbili nikaitwa kuhojiwa, nikamaliza ikaja kimbembe cha kupata kibali sasa, dah! Kila MTU anaikimbia barua...anaogopa kusaini, funny enough hadi Katibu Mkuu! Huu ninaousema ni ukweli sio majungu!

Nikajiuliza, huu uoga unatokana na Nini? Sikupata jibu kabisa!

Kulikua na Mzee wa Ghana yule nadhani alikua anataka kuanzisha Program ya mambo ya Rushwa, duh as we speak nadhani hajapata kibali bado!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,357
2,000
Miezi kama minne iliyopita nilikua nahitaji kibali cha kukusanya maoni kuhusu issue Fulani, nikapeleka barua TAMISEMI baada ya week mbili nikaitwa kuhojiwa, nikamaliza ikaja kimbembe cha kupata kibali sasa, dah! Kila MTU anaikimbia barua...anaogopa kusaini, funny enough hadi Katibu Mkuu! Huu ninaousema ni ukweli sio majungu!

Nikajiuliza, huu uoga unatokana na Nini? Sikupata jibu kabisa!

Kulikua na Mzee wa Ghana yule nadhani alikua anataka kuanzisha Program ya mambo ya Rushwa, duh as we speak nadhani hajapata kibali bado!

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani huu utawala wa awamu ya tano unaendesha Serikali yake kwa "mikwala"

Na ndicho kinachosababisha watumishi wafanye kazi kwa hofu kubwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom