tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,307
- 4,585
Hivi majuzi Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya mchapakazi, akiwa Morogoro alitoa taarifa kwamba hospitali za rufaa za mikoa zinakusudiwa kuhamishiwa Wizara ya Afya, toka mamlaka ya TAMISEMI.
Ingawa serikali ni moja, lakini kitendo cha hospitali za rufaa za mikoa kuwa chini ya TAMISEMI kinarahisisha mambo mengi sana ya kiutawala hasahasa katika kutatua kero za watumishi wa afya kama kutoa ajira, kuwaingiza watumishi haraka kwenye payroll, kulipa madai ya mishahara kwa wakati, kupandishwa vyeo kwa wakati n.k. Na pia wananchi kufikisha malalamiko yao kirahisi. Hii ni kwa sababu mamlaka zinazosimamia hospitali hizi zipo jirani na hospitali, tofauti na wizara ya afya ambayo iko centralized sana. Watumishi wa afya wa hospitali husika sasa watapaswa kusafiri kwenda Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam ili kufuatilia madai yao mbalimbali, ambayo yalikuwa yakihudumiwa vizuri na ofisi ya Katibu Tawala wa mkoa (RAS). Bahati mbaya sana hili litarejesha nyuma ufanisi wa hospitali hizi.
Ni bahati mbaya sana kwamba Wizara ya Afya imeshindwa kuzihudumia vizuri hospitali zake chache katika rasilimali watu, mfano Mirembe, Kibong'oto na hospitali ya rufaa Mbeya, sababu kubwa ikiwa ofisi yake pekee iko jijini Dar es Salaam, huku TAMISEMI ikiwa imesambaa. Chukua hospitali yoyote ya mkoa, halafu nenda kalinganishe na hospitali zilizo chini ya Wizara ya Afya uone ipi ina malalamiko mengi ya watumishi!!! Za TAMISEMI zina manung'uniko machache sana.
Lakini pia baadhi ya watumishi wasio waaminifu wa Wizara ya Afya, huzitumia hospitali zilizo chini yake kufanya ubadhirifu mbalimbali. Mfano kuzihamishia pesa zisizo maelezo kwenda hospitali husika, na kisha kurejeshwa kwenye akaunti za Watumishi wasio waaminifu.
HAKUNA UMUHIMU wa kuzihamisha hospitali za mikoa kutoka TAMISEMI naamini hili hata watumishi wa hospitali hizi hawalipendi, cha muhimu wizara ya Afya na TAMISEMI wapeane ushirikiano katika kutatua changamoto zilizopo. Mkuu wa mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa wanatosha sana kumwakilisha Rais katika kusimamia hospitali hizi ambazo ndizo uti wa afya mikoani, Wizara ya Afya ibaki kuwa na majukumu iliyonayo sasa ikiwa ni pamoja na regulation, kama kuna mapungufu basi yanapaswa kutatuliwa.
Hospitali za rufaa za mikoa zahamishiwa Wizara ya Afya
Monday, November 27, 2017
Kwa ufupi
Tamisemi itaendelea kusimamia hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati.
By Habel Chidawali, Mwananchi hchidawali@mwananchi.co.tz
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo amekabidhi hospitali za rufaa za mikoa kwa Wizara ya Afya.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa pendekezo la Rais John Magufuli aliyetaka waziri wa Tamisemi na wa Waziri ya Afya wakae kujadili namna ya kuzifanya hospitali za mikoa kuwa chini ya Wizara ya Afya badala ya kusimamiwa na Tamisemi kama ilivyo sasa.
Jumamosi Novemba 25,2017 alipozindua Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), kampasi ya Mloganzila, Rais Magufuli alisema kufanya hivyo kutaondoa mkanganyiko na kupanga watumishi holela kwenye hospitali, jukumu ambalo wamepewa watu wasio na utaalamu wa masuala ya afya.
Rais Magufuli alisema Tamisemi watabaki wanasimamia hospitali za wilaya na nyingine ndogo.
Waziri Jafo amesema leo Jumatatu Novemba 27,2017 kuwa tayari wameshafanya mazungumzo.
"Kuanzia leo hospitali zote za rufaa zitakuwa chini ya Wizara ya Afya na kwetu sisi (Tamisemi) tutabaki na hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati pekee," amesema.
Kuhusu madaraka ya waganga wakuu wa mikoa amesema wataendelea kuwa chini ya Tamisemi lakini waganga wafawidhi wa hospitali watapelekwa Wizara ya Afya.
Amewataka waganga hao kufanya kazi waliyokubaliana na Tamisemi ya kusimamia ujenzi wa vituo vya afya 172 nchi nzima.
Akizungumza mgongano wa madaraka kwa waganga wa mikoa, Naibu Katibu Mkuu Tamisemi (Afya), Dk Zainabu Chaula amesema hakutakuwa na shida kwa kuwa kila kitu kimewekwa sawa.
Dk Chaula amesema hata kabla ya kupelekwa huko, hospitali za mikoa zilikuwa zikipeleka taarifa moja kwa moja wizarani.
My Take
Kuna mtu hajamshauri vizuri Mheshimiwa.