Rais Magufuli upo wapi? Waajiri wako tunataka kujua upo wapi? Viongozi wenzako wa EAC/SADC na marafiki wanakutafuta mbona hujitokezi?

Naandika hili andiko nikitumia haki yangu ya kikatiba kutaka kujua rais Magufuli yupo wapi...Tuna haki ya kujua maana hatujui aliko na kwenye Ikulu zote mbili hajaonekana kwa zaidi ya mwezi na huu ni mwezi wa pili sasa. Tumesikia amekataa kuhudhuria mkutano wa SADC kwa Webinar na mkutano wa EAC kujadili CORONA imeonekana hataki kujihusisha....Rais nia yako ni nini?
Leo rafiki yake mkuu Raila Odinga ameonekana kwenye Television akisema amemtafuta kwa simu na kumwachia message hajibu.....Inatisha sana kuona hataki kuongea na Taifa hasa kwenye mapambano haya ya CORONA (Viongozi wote wanakuwa kwenye podiun wakijadili au wakiongea na Press kuhusu mikakati ya kuzuia na kuutokomeza ugonjwa wa CORONA, Yeye haeleweki yupo wapi na strategies zipi anatumia ili tuwe salama)
Tumeona kwenye magazeti mipaka inafungwa na baadhi ya nchi majirani zetu, tunaona magari na madereva wetu wanakatazwa kuingia karibu nchi zote jirani, tumesikia pia madereva wetu wengi wanaopimwa hizi nchi wamepatikana na ugonjwa wa CORONA!!!
Rais Magufuli una nia gani na Taifa hili? Weka wazi nia yako ili watanzania tujue kuwa DIRECTION GANI.
Mheshimiwa rais, katika kipindi hiki tungependa kusikia strategies zipi zinatumika ili wananchi wetu wasipotee.

Kama mwananchi wa kawaida ni haki yangu kujua alipo rais na ana nia gani na nchi yetu....
Mwongozo uliopo toka kwa kiongozi wetu ni: "chapeni kazi". Sasa wewe badala ya kuchapa kazi unaleta umbeya hapa ili kufurahisha mabeberu!!
Niwaombe watanzania wenzangu tuwajibu watu kama hawa kwa kuchapa kazi!! Peleka jibu kwa mabeberu kuwa "Watanzania wanachapa kazi"
Niwaombe watanzania wenzangu kws kipindi hiki tuwe macho sana na hujuma !!. Kwa mfano watanzania watakaolazimika kusafiri nje ya nchi ni vizuri wakapima kabla ya kuondoka. Maana wakipimwa huko nje wanaweza wakabambikizwa corona ili nchi yetu ionekane watu wake wote wana corona!!
 
Naandika hili andiko nikitumia haki yangu ya kikatiba kutaka kujua rais Magufuli yupo wapi...Tuna haki ya kujua maana hatujui aliko na kwenye Ikulu zote mbili hajaonekana kwa zaidi ya mwezi na huu ni mwezi wa pili sasa. Tumesikia amekataa kuhudhuria mkutano wa SADC kwa Webinar na mkutano wa EAC kujadili CORONA imeonekana hataki kujihusisha....Rais nia yako ni nini?

Leo rafiki yake mkuu Raila Odinga ameonekana kwenye Television akisema amemtafuta kwa simu na kumwachia message hajibu.....Inatisha sana kuona hataki kuongea na Taifa hasa kwenye mapambano haya ya CORONA (Viongozi wote wanakuwa kwenye podiun wakijadili au wakiongea na Press kuhusu mikakati ya kuzuia na kuutokomeza ugonjwa wa CORONA, Yeye haeleweki yupo wapi na strategies zipi anatumia ili tuwe salama)

Tumeona kwenye magazeti mipaka inafungwa na baadhi ya nchi majirani zetu, tunaona magari na madereva wetu wanakatazwa kuingia karibu nchi zote jirani, tumesikia pia madereva wetu wengi wanaopimwa hizi nchi wamepatikana na ugonjwa wa CORONA!!!

Rais Magufuli una nia gani na Taifa hili? Weka wazi nia yako ili watanzania tujue kuwa DIRECTION GANI.

Mheshimiwa rais, katika kipindi hiki tungependa kusikia strategies zipi zinatumika ili wananchi wetu wasipotee.

Kama mwananchi wa kawaida ni haki yangu kujua alipo rais na ana nia gani na nchi yetu....
Marais hutafutana kwa simu maalumu kupitia wasaidizi wao acha uzandiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watu wanaotafuta kila siku na kuhoji kila siku eti kwa nini Rais hayuko Dodoma au Dar? Shida wanamtafutia huku mitandàoni, waende ikulu wakaulize huko.Ni nani aliyeenda ikulu akamkosa?
 
Back
Top Bottom