Rais Magufuli upo wapi? Waajiri wako tunataka kujua upo wapi? Viongozi wenzako wa EAC/SADC na marafiki wanakutafuta mbona hujitokezi?

Sio kwamba nakubaliana na Magufuli lakini tuone hizi nchi zinazotuzunguka na hatua walizozifanya kama zimewasaidia
  • Uganda wamejifungia ndani - lakini mwisho wametoka
  • Kenya wanaendelea na shughuli zao lakini usiku ndani- inawezekana wanaendelea vizuri kwakuwa maambukizi yameshuka
  • Rwanda wamejifungia ndani- ila hali za wananchi ni mbaya wanalalamika
  • Burundi wako kimya- wanafanya wanachoweza
  • Tanzania wanaendelea na maisha kama kawaida - nanga inapaa kwa hiyo mapendekezo yetu mnafikiri tufanye nini?
  • kitu kimoja nakiona changamoto ni jinsi gani tunaweza kuwa na data sahihi kwa wagonjwa wanaokufa na jinsi tunavyokwenda itafika wakati wagonjwa wa korona hawatakuwepo kwa kuwa ikijulikana utazikwa na serikali.
  • lililomuhimu chukua hatua binafsi katika kujilinda na corona kwa kuwa hauna dawa na pia tuwalinde binti zetu na ikitokea wakapata MIMBA tusiwatoe kwakuwa wenyewe walishatoa nyingi inawezekana ikawa wewe ndio unamalizia mjukuu wako wa mwisho.
kinachotusumbua ni kuendelea kuona kuwa jambo zuri lazima lifanywe na waliotutawala na kingine watanzania tumekuwa watu wa kutazama ubaya kwetu kama hatuna vizuri.
 
Dah!...Yupo Chato anaongoza mapambano ya Corona kutokea huko. (Kumbuka Chato pia ni Tanzania).
 
Mwongozo uliopo toka kwa kiongozi wetu ni: "chapeni kazi". Sasa wewe badala ya kuchapa kazi unaleta umbeya hapa ili kufurahisha mabeberu!!
Niwaombe watanzania wenzangu tuwajibu watu kama hawa kwa kuchapa kazi!! Peleka jibu kwa mabeberu kuwa "Watanzania wanachapa kazi"
Niwaombe watanzania wenzangu kws kipindi hiki tuwe macho sana na hujuma !!. Kwa mfano watanzania watakaolazimika kusafiri nje ya nchi ni vizuri wakapima kabla ya kuondoka. Maana wakipimwa huko nje wanaweza wakabambikizwa corona ili nchi yetu ionekane watu wake wote wana corona!!
 
Back
Top Bottom