Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 137
- 179
Salaam Wana JF.
Nianze andiko hili kwa kurejea usemi huu usemao "Africa consumes what it does not produce and produces what it does not consume" Kuna mantiki pana juu ya usemi huu na kinachoendelea kwa sasa dhidi ya chanjo ya Covid 19, Rais wa Tanzania ameibua mjadala mpana ndani na nje ya Tanzania baada ya kuhoji ubora wa chanjo inayoendelea kutolewa kwa sasa kama sehemu ya mapambano dhidi ya Corona, Wapo wanaobeza na kukejeli juu ya kauli ya mkuu wa nchi, lakini ukweli ni kwamba Rais Magufuli yupo sahihi kabisa kuhoji na kutaka kujiridhisha dhidi ya ubora wa chanjo hiyo, kabla haijafanya kazi kwetu na huu ndio uongozi wa kujali na kulinda watu dhidi ya afya zao, Ni Rais Magufuli tu aliyethubutu kuhoji mpaka sasa kwa viongozi wa bara la Afrika, sijasikia mwingine mpaka muda huu.
Ukweli ni kwamba Tanzania sio kuwa tunaishi katika sayari tofauti na hii ya dunia la asha! wala Tanzania sio kisiwa tunahitaji kushirikiana na Wanadunia wenzetu pale inapohitajika kuungana na kupambana kwa pamoja, lakini sio kila kitu kinacholetwa kwetu tukubaliane nacho bila kuhoji na kudadisi faida, athari, ubora na umuhimu wake kwa afya ya binadamu, hata kama wenzetu wameamua kukubaliana na Jambo/kitu hicho. Bahati mbaya tumekuwa na watu wenye kariba tofauti katika jamii zetu wengi wao wakiwa ni wale "wa bora liende na kuthamini cha wazungu vs cha mwafrika" Huu ni utumwa kama ulivyo utumwa mwingine.
Mantiki ipo wazi ukiwauliza wale wote wanaombeza na kumshambulia Rais hasa Watanzania kuwa "Wanauelewa gani juu ya ubora wa hii chanjo wanayoishadadia?" hamna jibu la msingi zaidi ya Wazungu hawakosei na wanajua zaidi ya Mwafrika, Je Waafrika tutajipenda na kujithamini lini? Kwanini tunajibagua na kuona hatufai kwa lolote, nani aliye "tuchawia", Nilitegemea kauli ya Rais Magufuli itaonyesha njia na kumuunga mkono kwa kile alichokihoji badala yake imeonekana kama nongwa na dhambi fulani hivi, huu ni upuuzi kabisa kubeza maono ya viongozi wetu wanaothamini utu wa mwafrika na afya yake kwanza, ni Mara ngapi tunasikia athari ya chanjo tofauti tofauti zinazoletwa Afrika? au nalo hilo hatuna habari nalo, Je ni bora kwenda kuchanjwa tu bila kujua madhara ya hapo badae ya chanjo hiyo? ni bora kuhoji kuliko kutohoji kabisa.
Nilifikri hoja za Watanzania zitakuwa katika upande wa kuhamasisha wanasayansi wetu kutafiti na kutengeneza chanjo dhidi yetu lakini imekuwa tofauti kabisa badala yake tumekuwa vinara wa kushadadia chanjo tusiyoijua A to Z yake ni ipi katika afya zetu, Je liko wapi kosa la Rais Magufuli katika hoja yake dhidi chanjo ya Corona? Kwasababu tunapenda vya uzunguni miaka ya 1996 tuliwai kuingiziwa maziwa ya mbwa" fresh" sokoni na watu wakayatumia bila kuhoji japo badae ilikuja kubainika na kupigwa marufuku, tutangulize maslahi ya Uafrika wetu na tusikubali kupokea kila aina ya huduma bila kuhoji faida na hasara zake.