Rais Magufuli unawaonesha cha kuwatendea Watumishi wa Umma lakini Ndumbaro na Mkuchika wao hawajui kuitenda hiyo haki hata sasa

Tila-lila2

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
653
1,058
Rais wangu hujali gharama, anatoka mtu unaweka mtu. Hata kama katoka ncha nyingine ya nchi hujali gharama za kumhamisha. Unawapa ulaji. Hasa wale watumishi wenye elements za kiutumishi. Safi sana!

Aliyechukua nafasi ya Katambi wa Dodoma anatoka Geita, anakuja kulipwa mahela na masalahi mengine ya Ukuu wa Wilaya - kwa muda mfuoi tu. Hukutaka nafasi ya Katambi mtu wa Ofisini kwake au hata wa Mkoa wa Dodoma akaimu. Umemtoa - na yeye pia atalipwa mahela na yatamsaidia kwenye Kampeni zake za kuwania Shinyanga Mjini. Safi sana Rais wangu, hujali gharama - mtu anatoka na mahela yake unamweka mwingine na kumpa mahela yake. Wote hao kina Ole Sendeka, Mkenda na wote hao, wanaondoka na neema unawaleta wengine kwenye neema!

Sasa huku kwa wanaosimamiwa na kina Mkuchika hali sio hivyo Rais wangu. Hali ni mbaya sana. Watu wanakaimishwa miaka zaidi ya miwili. Utumishi wamekalia tu barua za kuidhinisha watumishi kwenye nafasi zao. Mtu hamna hata shaka kuwa anakaimu nafasi ambayo haina mtu lakini mtu hathibitishwi eti kisa kuepuka gharama kuwa kama hamna barua yakuthibitishwa na Utumishi asilipwe. Halmshauri watu kibao wanakaimu, wameombewa Utumishi na TAMISEMI lakini hawathbitishwi. Mpaka ninaacha utumishi wa Umma mwaka 2017 nilikuwa nimeshakaimu zaidi ya miaka miwili na nusu. Haki iko wapi Ndumbaro na Mkuchika?

Angalieni Rais asivyopenda watu kukaimu. Mtu anatoka yeye anaweka mtu. Nyie Utumishi hivi hizo fedha ni za kwenu au za Serikali? Acheni roho mbaya. Mmheraibu sana utumishi wa umma. Mnasbabisha Rais achukiwe bure kumbe tatizo ni ninyi. Kama tatizo lingekuwa ni kwa Rais mbona yeye sasa hakawizi. Acheni mambo yenu hayo. Na mwaka huu kwa kweli mnachangia sana kupunguza kura za CCM. Hovyo kabisa ninyi!
 
Ndiyo sisi watumishi wa umma ni kama Majendaheka au panzi au tufanye ni nyumbu au hata mindondocha, au tuseme mijitu ya karne ya 3 au mipumbavu tu.

Tunamchagua mtu tunampa nguvu ili awe na nguvu ya kuishinda nguvu ya wote walio mchagua.

------ndiyo sisimabandikabandua-----
 
Ndiyo sisi watumishi wa umma ni kama Majendaheka au panzi au tufanye ni nyumbu au hata mindondocha, au tuseme mijitu ya karne ya 3 au mipumbavu tu.

Tunamchagua mtu tunampa nguvu ili awe na nguvu ya kuishinda nguvu ya wote walio mchagua.

------ndiyo sisimabandikabandua-----
Inaumiza sana!
 
Back
Top Bottom