Rais Magufuli unamuua mama yangu

Baba yenu

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
1,053
1,417
Hii ni kweli jamani ni story imemkuta mama mdogo

Mamdogo ni mwalimu wa msingi na anatarajia kustaafu mwakani hivyo kwenye akili yake alishajiandaa kustaafu

Kitu ambacho hatukujua ni kuwa muda wote aliofanya kazi hakuwa akitumia cheti chake halisi( shangazi alifariki zaman sana hivyo ukoo ukakubaliana kumpa mama mdogo cheti cha shangazi akaingilia chuo cha ualimu miaka hiyo ya sabini na..
Mpk akaajiriwa)

Sasa kwa hesabu ya haraka mwakani anapaswa astaafu!! Ila ukaguzi huu wa Magufuli umemkumba

Mama anateseka presure inapanda asubuhi na jioni, vyeti vimehangaikiwa mpaka viapo vya kubadilisha jina ila wapi? Baraza wamekaba kooo!

Tunajua yawezekana ni kweli amekosea kutumia cheti cha mtu kazini lakini tutumie ubinadamu mama huyu kafanya kazi miaka zaidi ya 25 na alikuwa anategemea mafao yake karibia million 100 mwakani halaf leo hii ziyeyuke kirahisi hivi??

Rais Magufuli watu wa aina hii ya mama waonee huruma jamani mama atakufa hivi hivi tunamuona!
 
Hamna namna yeye angestaafu kwa hiari pale aliposikia Rais anataka kushughulikia tatizo la watumishi hewa. Sasa ni too late lazima atastaafishwa kwa kosa la fojari au kutumia cheti siyo chake. Nampongeza sana RAIS kwa zoezi hili Pendwa na kupunguza hewa kila sehemu. Ushauri wangu kwa Admin JF waangalie namna ya kupambana na WANAJUKWAA au WANAJAMVI HEWA .
 
duh sasa jaman hata kama ni kusukuma mashambiulizi ila hapa jpm mnamuonea...aaaaaaaah nmeboreka maana mtafanya hata wanaokosoa baadhi ya mambo kwa nia njema waonekane hawana maana
 
Hamna namna yeye angestaafu kwa hiari pale aliposikia Rais anataka kushughulikia tatizo la watumishi hewa. Sasa ni too late lazima atastaafishwa kwa kosa la fojari au kutumia cheti siyo chake. Nampongeza sana RAIS kwa zoezi hili Pendwa na kupunguza hewa kila sehemu. Ushauri wangu kwa Admin JF waangalie namna ya kupambana na WANAJUKWAA au WANAJAMVI HEWA .
Huyu mama umeambiwa kuwa ana zaidi ya miaka 25 kazini chini ya utendaji wake ni vijana wengi sana wamepata elimu kupitia kwake,si ajabu ukakuta wengine waliopata elimu chini ya huyu mama ni hawa hawa wanaowaita wenzao watumishi hewa au wanaweza wakawa ni ndugu zao au wanaweza wakawa ni watumishi katika serekali hihi ya kuwaita wenzao watumishi hewa,sasa je kama huyu mwalimu ana itwa mtumishi hewa na wale waliopata mafanikio kwa kupitia elimu yake waitwe akina nani?.
 
Kwa kuwa alipitia chuo na vyeti vya chuo ni vyake huyu mama angesamehewa tu.
 
Huyu mama umeambiwa kuwa ana zaidi ya miaka 25 kazini chini ya utendaji wake ni vijana wengi sana wamepata elimu kupitia kwake,si ajabu ukakuta wengine waliopata elimu chini ya huyu mama ni hawa hawa wanaowaita wenzao watumishi hewa au wanaweza wakawa ni ndugu zao au wanaweza wakawa ni watumishi katika serekali hihi ya kuwaita wenzao watumishi hewa,sasa je kama huyu mwalimu ana itwa mtumishi hewa na wale waliopata mafanikio kwa kupitia elimu yake waitwe akina nani?.
No... zoezi ni kuhakiki watumishi hewa na wala siyo Zoezi la kuangalia utendaji kazi wa Watumishi HEWA. Tofautisha vitu hivyo kwanza Mkuu.
Suala la kusoma kwa kutumia cheti cha mtu mwingine ni kosa kisheria. Kwa hiyo Haki hupatikana japo kuwa huchelewa .
 
Sawa kibinadamu tumfariji mwenzetu na huyo mama mwalimu mhanga wa janga hilo, lakini kwa style tunayokwenda nayo awamu hii ya tano swala la kuonewa huruma huyo mama ni sawa na kupigia mbuzi bongo flava ukitegemea atacheza! Wahanga wa tetemeko Kagera ni mfano hai, tumepatwa na jua!
 
Inaleta majonzi sana, wamsaidie astaafu kwa amani jamani. Kaz ya ualimu siyo mchezo then mwishoni unyimwe mafao yako, so sad
 
Hamna namna yeye angestaafu kwa hiari pale aliposikia Rais anataka kushughulikia tatizo la watumishi hewa. Sasa ni too late lazima atastaafishwa kwa kosa la fojari au kutumia cheti siyo chake. Nampongeza sana RAIS kwa zoezi hili Pendwa na kupunguza hewa kila sehemu. Ushauri wangu kwa Admin JF waangalie namna ya kupambana na WANAJUKWAA au WANAJAMVI HEWA .

No... zoezi ni kuhakiki watumishi hewa na wala siyo Zoezi la kuangalia utendaji kazi wa Watumishi HEWA. Tofautisha vitu hivyo kwanza Mkuu.
Suala la kusoma kwa kutumia cheti cha mtu mwingine ni kosa kisheria. Kwa hiyo Haki hupatikana japo kuwa huchelewa .
Hayajawahi kukuta utanywea na hautathubutu siku nyingine kukejeli wahanga. Ushabiki mpaka kwenye maisha ya watu.

Mtu amefanya kazi karibu miaka 30 unamuitaje mfanyakazi hewa ?! Kweli awamu hii WaTz wamepatikana! !
 
Huyu mama umeambiwa kuwa ana zaidi ya miaka 25 kazini chini ya utendaji wake ni vijana wengi sana wamepata elimu kupitia kwake,si ajabu ukakuta wengine waliopata elimu chini ya huyu mama ni hawa hawa wanaowaita wenzao watumishi hewa au wanaweza wakawa ni ndugu zao au wanaweza wakawa ni watumishi katika serekali hihi ya kuwaita wenzao watumishi hewa,sasa je kama huyu mwalimu ana itwa mtumishi hewa na wale waliopata mafanikio kwa kupitia elimu yake waitwe akina nani?.
Watu wangapi miaka yote hiyo wamepata elimu duni toka kwa mtu ambae hana sifa? Sio ajabu kuna watu wamefeli mtihani na wanateseka kwa ajili ya udanganyifu wa huyu mama na nduguze wana ukoo.
 
Nimebaki mdomo wazi sababu alikuwa anaanza kutumia akijua sio cheti chake, na alidanganya tangu mwanzo akijua analofanya.

Kama ndugu mnampenda kweli, basi mumchangie pesa aishi maisha anayotaka na mtakayopendezwa nayo.
 
Back
Top Bottom