Rais Magufuli, unamkumbuka mwandishi huyu?

MWATANI

Member
Feb 14, 2014
44
125
Wanabodi nawasalimu kwa heshima kubwa.

Jioni ya leo nimetoa maoni yangu kwenye uzi wa Ng'wamapalala, unaosema '' Kwanini wanahabari wazaliiwa wa maeneo ya Kagera huwasumbua watawala nchini'' Kwenye maoni yangu nikasema wapo baadhi ya waandishi wanatoa hoja zao kwa mantiki na mrengo chanya wa kuisaidia serikali na nikatoa mfano wa kumtaja Deogratius Mutungi.

Sasa nimepata na kujua mengi juu ya mwanahabari huyu na hii ni baada ya kulitaja jina lake humu Jukwaani, Licha ya kuandika makala zenye weledi na kujenga utaifa na maendeleo ya nchi kumbe pia ni miongoni mwa vijana wachache waliomshauri JPM kuchukua fomu kugombea urais.

Aidha nimejulishwa kuwa mwaka 2009 alikutana na JPM wakati ameenda kwa ndugu yake Eng. Severine Mugumisa pale Wizara ya miundo mbinu na ndipo alipomuomba JPM kuchukua fomu wakati ukifika na ndivyo ilivyokuwa kwa JPM kuzingatia ushauri wa Deo na wengine wote waliompa ushauri.

Maswali kwako JPM:

1) Je, unamkumbuka mwana habari huyu?

2) Je, unasoma na kupitia makala zake anazoandika kupitia RAI NGUVU YA HOJA?

3) Je, licha ya kukupa ushauri ambao pengine umechangia kuwa kiongozi wa Taifa hili na kuleta mapinduzi chanya kwa Taifa zima, unajua maswahibu gani Deo anapitia hapo TBC?

Nimeambiwa mengi juu ya mwanahabari huyu ambaye licha ya kukushauri lakini bado anaendelea kutangaza mazuri ya Serikali yako na anapokosoa anakosoa kwa hoja kinyume na wana habari wengine.

Ikikupendeza, mkumbuke hata kwa salamu tu maana ni miongoni mwa wanataaluma wanaoinadi Awamu ya Tano kwa nguvu zao zote.
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,356
2,000
Siku hizi mambo ni kujipigia pande! Naona mkuu umesahaulika pamoja na kuandika sasa umeamua kupitia JF ili ujumbe ufike.

JPM huwa hasahau watu waliomfanyia hisani. Wewe/huyo mwandishi huenda hufikii viwango.

Endelea kuomba
 

Uhuru Wetu

New Member
Aug 21, 2019
1
20
Nimekuwa nikiona na kusoma makala zake ndani ya Rai zina hoja zinazoeleweka katika mustakabari wa kusaidia nchi kusonga mbele.
 

Rooney

JF-Expert Member
Jan 16, 2015
3,790
2,000
Huo mwaka 2009 una mengi.

Mie pia nlitabiri atakua next prezdaa mpka ubishani ulikuwa mkali baina yangu na wadau.

Fast forward siku kapitishwa tu kugombea, wadau tulikutana maeneo fulani, wengi wakiwa curious nliona nini?

Sasa fast forward now
 

No retreat no surrender

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
1,869
2,000
Wabongo bwana? Eti alikushauri?

Werevu husema Ishi kwa ushauri unaowapa wengine. Basi aje anishauri na Mimi niwe rais?

Tangu JPM akae Serikalini miaka 20 kabla ya kuwa Rais wa nchi unadhani kakutana na wangapi wakimshauri awe Rais? Sasa unataka fadhila zipi eti nilikushauri?

Anyway maandiko yanasema "ushauri wa masikini hausikilizwi" na "tenda wema uende zako"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom