Rais Magufuli unakumbuka hii ahadi yako hii kwa wafanyakazi?

chevirole

Senior Member
Sep 27, 2017
145
225
Wana jamvi amani iwe nanyi, nakumbuka wakati mh rais anaingia marakani alituahidi watanzania kwamba atapunguza mishahara minono ya mpaka milion45 kwa mwezi na kuwapandishia wanyonge kima cha chini ambacho ni laki 3 kwa mwezi.

Mpaka leo hii vigogo wameendelea kulamba mishahara minono huku mfanyakazi wa chini akiambulia pesa kiduchu ambayo haikizi mahitaji muhimu kwa mwezi. Haiwezekani nchi moja mwengine apate mil 45 na mwengine apate sh laki 3.

Najiuliza kweli tutafika? Maana gepu ni kubwa mno na mpaka sasa takribani miaka 2 tangu uongozi wako ushike hatamu hujaongeza kiima cha chini na juzi umetamka wazi hutaongeza mishahara kabisa.

Baba napenda kukukumbusha hii ahadi yako inawezekana umeisahau au uliongea kisiasa tu? Maana nchi ni moja lakini tumegawanyika kimatabaka kati ya walionacho na malofa, wengine wanaishi kama malaika ukiwamo wewe, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi, na vigogo wengine: wakati huo wafanyakazi wa kawaida wanaishi kama mashetani, hawa ni walimu,manesi,askari,watumishi wa halmashauri,mahakimu na makarani n.k.

Mwisho sipendi kunukuu ule msemo kwamba ccm timeichagua wenyewe acha tuisome namba, ccm ni mbele kwa mbele.

Mungu ibariki tanzania
 

manzuki

JF-Expert Member
Aug 21, 2017
275
250
daaaaa! jamaa kwel umetukumbusha mbali cc huku tunahsngaika na mabonde yetu tumeshaanza kulima nyanya na mbogamboga kama kauli asiyefanya kazi na asile na asipokula afe
 

pangalashaba

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
1,236
2,000
Kuna tetesi kuwa mapato ya serikali yemepungua mpaka kufikia billion 600 na ushee kwa mwezi. Kama ni kweli hiyo ahadi yake ni bora uisahau kabisa.
 
Top Bottom