Rais Magufuli unakiri uwepo wa Corona ila hotuba zako zinafubaza mapambano dhidi ya Corona

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,486
2,332
Binafsi sina tatizo na wewe kwa kutoiweka nchi katika lockdown wala sina tatizo na na kauli zako kuwa corona ni kaugonjwa kadogo ni sawa na magonjwa mengine. Tumekubali kufanya kazi na hali iliyopo ila usitufanye kupuuzia kabisa hata zile njia ndogo ndogo zinazoweza kutusaidia kupunguza maambukizi.

1. Mara ya kwanza ulianza kwa kusema masks za viwandani zitakuwa na corona zichunguzwe, watu wakaacha kuzivaa kabisa wakiamini zina corona na ukahimiza za vitambaa za kushona wenyewe.

2. Mara ya pili ukawananga watu wa maabara tena hadharani kuwa yawezekana wanatumiwa na mabeberu. Hii ni kuwavunja moyo wao kama wafanyakazi pia ukatufanya watanzania tuamini vipimo vyote walivyopima matokeo ni feki, ila cha ajabu bado mnaitumia na mnasema Wakenya walikutwa na corona.

3. Ukiwa Chato kanisani ulisema wewe hujavaa barakoa na hata waumini unaona hawajavaa hivyo hakuna sababu ya kuogopa. Nilidhani umeteleza ila hata jana ukiwa Singida umeirudia hii kauli ya matumizi ya barakoa. Sasa hivi watu wanaanza kuona hakuna haja ya barakoa tena.

4. Najiuliza hotuba ijayo utatupunguzia jambo gani tena, nahisi litakuwa la kunawa mikono maana ndio pekee njia tuliyobakiwa nayo ya kupambana na huu ugonjwa.
 
Back
Top Bottom