Rais Magufuli unaipeleka wapi hii nchi? Chanjo mahospitalini hakuna!

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
5,083
8,222
Kwa siku kadhaa nilikuwa nasikia kwamba chanjo kwa watoto wadogo hazipo katika hospitali karibia zote Tanzania. Mimi nilidhania hizo ni propaganda chafu tu za kuichafua hii serikali 'sikivu' ya Mkuu sana Magufuli.

Leo nimeshuhudia mwenyewe huku Dodoma, kwani leo ilikuwa ni tarehe ya kwenda kumpatia chanjo ya miezi miwili mwanangu. Muda si mrefu tumefika hospitalini na kuambiwa kwa sasa hizo chanjo hazipo. Tulipouliza tunaweza ipata wapi wametujibu kwamba Dodoma nzima kwa sasa hizo chanjo hamna kwani kituo kikuu cha kusambaza hizo chanjo (Hospitali ya Makole) nao hawana. Wao wenyewe huwa wanaenda kuchukulia Makole, and Makole zimeisha.

Tulipouliza ni lini zitapatikana wametujibu hata wao hawajui!!
Hivi jamani tumefikia huku kama taifa? Hawa watoto wana makosa gani hadi serikali ishindwe kuagiza kitu muhimu kama hiki? Wanataka watoto wetu waanze kuugua tena magonjwa ambayo yalishatokomezwa?

Tafadhali sana watu ambao mnasoma humu na mna 'access' ya kuongea na Magufuli mwambieni chanjo mahospitalini hamna. Fanyeni yote lakini msicheze na afya za watoto wetu tafadhali.

Inauma sana.
 
mh....inatia huruma sana pengine anataka tujute kwanini tulimuweka pale akae kwenye kile kitu. au kinamuunguza mbona afanyi kama tunavyotegemea
Mkuu imeniuma sana mwanangu kukosa chanjo Leo, yaani ni kwamba tumeambiwa hamna kabisa. Halafu hospitali tuliyoenda ni kubwa tu tena ya kidini. Sasa hizo nyingine sijui ni vipi?
 
Jamani hali ni mbaya KWELI KWELI hata vile vidonge vya majira clinic hakuna na kwenye famasi vipo vichache tena vimepanda bei balaa sasa hii familia inapangwaje kwa waliozoea vile vidonge jamani?! Hali ni tete baada ya kufungu maduka ya MSD kila kanda dawa ndio zimekuwa adimu kuliko yalipokuwa hayapo, mweee, .
 
Isije kua raisi Magu anajaribu kusafisha uozo uliokuepo na huku wengine wakimfanya makusudi ili mradi aonekane mbaya na hajali watu wake.
Ingekua vizuri hili suala liwafikie huko juu na tupate majibu ilitujue makosa yako wapi.
 
Alikimbia muhimbili sasa huu msala wa nchi nzima,nasikia hata ile mashine ya MRI imeharibika.
..heeheeeeeee safi sana b
 
Watasema chadema ndio chanzo.....madhara ya USAID yanaonekana,bado Dawa za ukimwi.....kwa msaada wa watu wa marekani lazima goti lipigwe,USAID walitukanwaaaa weeeeeee haya sasa,polio itarudi kwa kasi vilema waongezeke
 
Isije kua raisi Magu anajaribu kusafisha uozo uliokuepo na huku wengine wakimfanya makusudi ili mradi aonekane mbaya na hajali watu wake.
Ingekua vizuri hili suala liwafikie huko juu na tupate majibu ilitujue makosa yako wapi.
Hilo linawezekana pia
 
Back
Top Bottom