Habari wanaJamvi,
Kwanza nianze kukupongeza kwa kututembelea katika mkoa wetu mpya wa Songwe kwa Mara ya kwanza tangu umekuwa mkuu wa nchi.Ni jambo jema kwa ustawi wa mkoa wetu
Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu,leo wakati unaweka jiwe la msingi katika barabara ya Mpemba-Isongole kuna mambo kadhaa yaliibuka hasa baada ya Mh.Mbunge wa jimbo la Ileje Janeth Mbene kusema kwamba mkurugenzi anakwamisha mengi Ileje na utusaidie kumuondoa
Mheshimiwa Mbunge alikuwa anatoa sauti ya wanaIleje wasio na sauti ya kukufikia,na sikama ulivyodanganywa kwamba yeye ni mchapakazi hadi anafundisha,watume vijana wako wakafanye utafiti wakwambie kama kweli anafundisha na ni shule gani? maana sikweli.
Huyu mkurugenzi anaundugu na waziri mkuu,mh. Kasimu Majaliwa na ndiyo fimbo yake tangu akiwa afisa elimu pale manispaa ya iringa na ndiyo maana anaogopwa na haguswi na hata mawaziri wako(Jafo),na RC anajua
Kwanza anatuhumiwa kwa ufisadi wa pesa ya ujenzi wa hospital ya wilaya pale Itumba,amekuwa akidai rushwa kwa wakandarasi akihitaji ten percent, haya mkuu wa wilaya anajua hata mkuu wa mkoa anajua na RC alishamuundia hata tume kumchunguza,ila hata RC hajakwambia ukweli.Maana kuna waliohusika pamoja na mkurugenzi waliwekwa mahabusu kwa amri yake.
Hawapi posho madiwani ni zaidi ya miaka kadhaa sasa,Uhusiano wake pia haupo vizuri na watumishi wa halmashauri,na mwenyekiti wa halmashauri ameshaandika barua nyingi tu kuhusu huyu mheshimiwa ila kwasababu anangao ya PM hachukuliwi hatua yoyote.
Sauti ya Mbunge Mbene Si yakinafiki kama ulivyomtafsiri ila uliamua kujitoa muhanga ili upate picha ya hali halisi ya wilaya ya ileje,maana hakuna mshikamano wa viongozi hata DC anamuogopa na maendeleo unayohubiri utakuwa unampigia mbuzi gitaa tu,maana saizi anatamba kuwa wameumbuka na genge lake,eti hawamuwezi kwasababu umemtetea mbele ya umma.
Kama unataka kuupata ukweli tuma vijana wako,utapata ukweli usiyo na shaka,ili utuondolee hili jipu maana anakwamisha maendeleo kwenye wilaya iliyonyuma sana hasa kwenye miundombinu ya barabara.
Ukweli utabainika tu bila shaka
Tatizo la wabongo tunapenda kukariri, kwa hiyo mlitaka atumbuliwe jukwaani..!
Rais amesema anasubiri uchunguzi ulio chini ya Waziri-Tamisemi..
Halafu ataona ukweli wa malalamiko hayo.
Ndipo achukue hatua..