Rais Magufuli, ulipotaja kuwa umezalisha ajira milioni 6 huoni kuwa unanidanganya hata mimi?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Rais wangu, hivi unajua kuwa pamoja na kukupinga sana ila ni miongoni mwa watendaji wako wasaidizi wakuu ndani ya serikali? Kwa taarifa yako ninasimamia moja ya taasisi ambazo kwa siku za hivi karibuni umeelekeza macho yako yote pale. Nipo na vijana wako unaowatuma kila siku na mambo yanaenda vizuri sana kwao chini ya usimamizi wangu usiofuata mkumbo wala ulambaji viatu. Pale ofisi ya msajili mkuu wa Hazina ni nyumbani kwangu na tunafanya vikao kila mara.

Twende kwenye mada.

Unajua kuwa mimi ni mwenyeji mkubwa pale Hazina? Unajua kuwa naelewa madudu yote uliyofanya dhidi ya sekta binafsi kuanzia mwaka 2016 mpaka jana? Unajua kuwa ninazo taarifa za uhakika kuwa kwa utaifishaji holela na uvurugaji wa mipango uliofanya nchi nzima umegharimu ajira za watu siyo chini ya elfu 50?

Naomba nikueleze kuwa siyo kila msaidizi wako anafurahishwa na jinsi unavyoendesha nchi! Naomba kwa leo niishie hapo ila nyongo ikizidi itatoka!

Tukutane Dodoma kesho kwenye ripoti muhimu uliyotutuma kuifanyia kazi Dar!
 
Uthibitishie umma kuwa magu kateta uongo..?
Hata ukiweza kututhibitishia hapohapo jiulize swali hili "kwanini watu wanachepuka"
Ukijijibu hilo then fatilia mfumo tulioiga wa siasa unaendeshwaje hapo hautapata tabu kujisumbua!
 
Wanakuja watakwambia fisadi leo nilikuwa bungeni aliposema ajira direct 1milion+ na inderect 6milion mkapa aliinama na kutizama chini sema kamera sijuwi kama zimeona duh!

Yaani ajira direct 1milion zina impact kubwa sana kwenye uchumi tungekuwa tunaona imagine ukate mishahara yao kodi kwa 11% mapato ya serikali yangekuwaje.

Jamaa anaonekana ni mpishi mzuri wa pilau.
 
Rais wangu, hivi unajua kuwa pamoja na kukupinga sana ila ni miongoni mwa watendaji wako wasaidizi wakuu ndani ya serikali? Kwa taarifa yako ninasimamia moja ya taasisi ambazo kwa siku za hivi karibuni umeelekeza macho yako yote pale. Nipo na vijana wako unaowatuma kila siku na mambo yanaenda vizuri sana kwao chini ya usimamizi wangu usiofuata mkumbo wala ulambaji viatu. Pale ofisi ya msajili mkuu wa Hazina ni nyumbani kwangu na tunafanya vikao kila mara.

Twende kwenye mada.

Unajua kuwa mimi ni mwenyeji mkubwa pale Hazina? Unajua kuwa naelewa madudu yote uliyofanya dhidi ya sekta binafsi kuanzia mwaka 2016 mpaka jana? Unajua kuwa ninazo taarifa za uhakika kuwa kwa utaifishaji holela na uvurugaji wa mipango uliofanya nchi nzima umegharimu ajira za watu siyo chini ya elfu 50?

Naomba nikueleze kuwa siyo kila msaidizi wako anafurahishwa na jinsi unavyoendesha nchi! Naomba kwa leo niishie hapo ila nyongo ikizidi itatoka!

Tukutane Dodoma kesho kwenye ripoti muhimu uliyotutuma kuifanyia kazi Dar!
Ajira 6 million?labda wale fisi kule burigi wamepelekewa walinzi kutoka ccm lumumba kina jingalao,kawe alumni,magonjwa mtambuka,bia yetu,motochini etc..hawa wote wameajiriwa burigi kulinda fisi
 
Pia wanasema kuna viwanda vipya elfu 8 , hivi vinatengeneza bidhaa gani na zinauzwa wapi ?
Tukitumia scale ya cherehani nne ni kiwanda jiwe atakuwa yuko sahihi, ukiona majiko manne ya kuchoma chips mtaani kwako hicho ni kiwanda cha kutengeneza kihepe, kaya nne zenye friji hicho nacho ni kiwanda cha kutengeneza barafu, ukiwa na blenda nne hicho nacho ni kiwanda cha juisi, kwa hiyo Mzee yuko sahihi kabisa nami nakubali
 
Wanakuja watakwambia fisadi leo nilikuwa bungeni aliposema ajira direct 1milion+ na inderect 6milion mkapa aliinama na kutizama chini sema kamera sijuwi kama zimeona duh!

Yaani ajira direct 1milion zina impact kubwa sana kwenye uchumi tungekuwa tunaona imagine ukate mishahara yao kodi kwa 11% mapato ya serikali yangekuwaje.

Jamaa anaonekana ni mpishi mzuri wa pilau.
Kwani "Pascal Mayalla Njaa" anasemaje

Prophet of doom

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukitumia scale ya cherehani nne ni kiwanda jiwe atakuwa yuko sahihi, ukiona majiko manne ya kuchoma chips mtaani kwako hicho ni kiwanda cha kutengeneza kihepe, kaya nne zenye friji hicho nacho ni kiwanda cha kutengeneza barafu, ukiwa na blenda nne hicho nacho ni kiwanda cha juisi, kwa hiyo Mzee yuko sahihi kabisa nami nakubali
Hahahaha, tena viwanda vya nguo / vyereheni ndio vimeingiza pesa nyingi kwa kutengeneza na kuuza bidhaa kama
1.Barakoa
2.Vijora
3.Dila
4.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom