Rais Magufuli, ulipomuamrisha IGP kuwalazimisha wahalifu kuacha ujambazi, ulipaswa umkumbushe yasijirudie ya kama ya akina Zombe

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,284
2,000
Mh rais wewe ni mkuu wa taifa letu, na taifa letu linaendesha kwa misingi ya kuilinda na kuiheshimu katiba ya JMT.

Ibara ya 13 (6)(b) ya katiba ya JMT imetamka wazi kuwa hakuna mtu atakutwa na hatia ya jinai mpaka mahakama ithibitishe na kumtia hatiani.

Kumpa amri IGP awe anawalazimisha watuhumiwa kuacha ujambazi inaleta wasiwasi kwa sisi ambao tunaona kama hukutumia lugha ya wazi. Je, walazimishwe kuacha ujambazi kwa namna gani?

Ni wazi kuwa hakuna mtanzania anayependa uhalifu, lakini nini maana ya kuwepo kwa haki jinai kama mtuhiwa amekamatwa bila kukaidi?

Je, watanzania waanze kusikia habari kama kipindi kile cha msitu wa Mabwepande? Kwamba watu wanakamatwa tena wanatii bila shuruti alafu tunasikia walimiminiwa risasi?

Ilikuwa ni jambo jema umpatie Igp Sirro hiyo amri lakini umpe tahadhari juu ya kutokuathiri uhai wa watu ambao watajikuta wanaingia kwenye madhara ya askari ambao watafanya kama yale tuliyosikia kipindi cha akina Zombe.

Ni wazi kuwa amri uliyoitoa leo inatakiwa itekelezwe kwa umakini sana, la sivyo utasikia malalamiko mengi juu ya uovu wa askari polisi. Maana hata kabla ya akina Zombe kutiwa hatiani kila mtu aliamini anayeuawawa na polisi alikuwa ni jambazi.
 

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
3,283
2,000
kitu kinacho fanya polisi wa tanzania hakuna kitengo kinacho fatilia polisi,kitengo kinacho dili na upelelezi tu,kitengo kinacho dili ujambazi labda kidogo kipo kipo,kitengo cha cyber,kitengo cha usalama kikopolisi tu,polisi wa porini kwa ajili usalama ,hivi wenzetu wameviweza hata ukitokea kitengo fulani kuharibu basi ni rahisi kuelewa upende fulani,ndio maana unakuta vitengo hivi haviingiliani majukumu kwenye kazi ikitokea itajumuishwa kazi moja watashirikiana
 

cmoney

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
3,313
2,000
Mzee hili swala ni dunia Nina... Hukusikia maduro alikua anawasaka wauza poda nyumba kwa nyumba.... Cha umuhimu huu utawala mwengine we tafuta tu kazi nyengine ya kufanya... Mkitukuta 18 hamnaga huruma nyie
 

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,284
2,000
Mzee hili swala ni dunia Nina... Hukusikia maduro alikua anawasaka wauza poda nyumba kwa nyumba.... Cha umuhimu huu utawala mwengine we tafuta tu kazi nyengine ya kufanya... Mkitukuta 18 hamnaga huruma nyie
Criminal justice? Je ikitokea wakauliwa wasio na hatia kama wale wafanyabiashara wa madini?
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
101,512
2,000
Hata ufanyeje hatuwezi kukupatia uteuzi hata kama unatokea Usagara
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom