Rais Magufuli ulimtumbua upesi aliyechana Quran, mbona unachelewa Kumtumbua Jerry Muro aliyewadharau Waislamu?

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,401
2,631
Rais Dkt. Magufuli ulimtumbua upesi yule Mtumishi wa Halmashauri ya Kilosa Ndugu Daniel Maleki ambaye alikuwa ni Afisa Kitengo cha Biashara kwa Kosa la Kuchana Kitabu Kitakatifu cha Quran kinachotumiwa na Waislamu, ila tunashangaa ni kwanini hadi hivi sasa hujamtumbua Mkuu wa Wilaya Jerry Muro kwa Kosa la Kuwadhihaki Walimu wa Madrassa kupitia Msemaji wa Simba SC Haji Manara.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli Kauli ya DC Jerry Muro ya Kumdhihaki Msemaji wa Simba SC Haji Sunday Manara kupitia Kituo cha Redio cha Wasafi FM na Mtandao wa WhatsApp wa Klabu ya Yanga kuwa Elimu aliyonayo Haji Manara ni ya Kufundisha tu Watoto Madrassa Kimantiki (Logically) haina tofauti na Kuwatukana Waislamu hasa ukizingatia kuwa hata hao Walimu wa hizo Madrassa wanatumia hicho hicho Kitabu Tukufu cha Quran.

Na najua Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli una mambo mengi ya kikazi (Kiutendaji) hivyo unaweza mambo mengine ukawa hujaambiwa na Mimi Mpiga Kura wako Mzukulu nakuambia muda kuwa tayari Msemaji wa Simba SC Haji Manara nae ameamua kwenda mbele ambapo sasa anaenda Kumshtakia DC wako Jerry Muro kwa Waislamu na kama haitoshi tayari kuna Waislamu kadhaa nao wameshaibuka (hasa Walimu wa Madrassa) wanajipanga ili waone Hatua Kali za Kumchukulia DC wako huyu Mpuuzi Jerry Muro kwani wanasema kuwa Dhihaka aliyotoa DC Jerry Muro hakumlenga tu Haji Manara bali amewalenga pia na Waislamu wote nchini.

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli Waislamu hawa (amba huwa hawana Masihara ukiyagusa Maslahi yao ya Kiimani) wameenda mbele zaidi na Kuhoji ya kwamba kama ni mambo ya Kimchezo ya Utani wa Jadi wa Simba na Yanga kulikuwa na haja gani kwa DC Jerry Muro kuingizia Masuala ya Kiimani (Dini) hadi Kuwadhihaki Walimu wa Madrassa kupitia Msemaji wa Simba SC Haji Manara ambaye anajulikana kuwa ni Mwalimu mzuri mno wa Madrassa?

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli Mtumishi wako huyu DC Jerry Muro hakuanza leo Kumdhihaki Msemaji wa Simba SC Haji Manara na kuna Kipindi huko nyuma aliwahi Kumdhihaki hadi kupitia Ulemavu wake wa Ngozi (Ualbino) kwa Kumuita Dili na hakuchukuliwa hatua ila nina Ushahidi wa Watanzania kama Wawili hivi ambao walikamatwa kwa Kosa la Kuwaita Dili hawa Walemavu wa Ngozi (Maalbino)

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli wapiga Kura wako tunajiuliza Maswali hivi ni kwanini kila ambapo DC wako huyu Jerry Muro akiwa anazungumzia masuala ya Mpira hasa ya Utani huu wa Jadi wa Simba na Yanga akianza Kumtaja Msemaji wa Simba SC Haji Manara ni lazima tu atatoka kwenye lengo na ataanza Kuzungumzia Maisha yake binafsi, kumtukana, kumdharau na kumdhalilisha? Hivi na siku Msemaji wa Simba SC Haji Manara nae akisema afyatuke (afunguke) kwa mambo binafsi ya DC wako Jerry Muro (ambayo mengine ni mabaya kabisa na yanatia Aibu) patakalika Mheshimiwa? au DC wako Jerry Muro anadhani Yeye ni Msafi hivyo, Muadilifu, Malaika na hana Mauzauza yake tena ambayo yanazidi hata anayomdhihaki nayo Msemaji wa Simba SC Haji Manara?

Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kama ulimtumbua Mchana Quran Ndugu Daniel Maleki basi nakuomba pia usijiulize katika kumtumbua Mtukana Walimu wa Madrassa Ndugu Jerry Muro kwani wote (Wawili hawa) ni Watumishi wako katika hii Serikali yako ya awamu ya Tano ambayo tunaamini kuwa inatenda Haki (japo najua haki ya kweli huwa ipo Mbinguni tu Kwake Mwenyezi Mungu) Baba Muumba.

Na nasikitika na hata Kushangaa kuona Mamlaka zako husika TCRA imenyamaza juu ya DC wako huyu ( Jerry Muro ) Kumdhihaki Muislamu na Msemaji wa Simba SC Haji Manara kupitia Kituo cha Redio cha Wasafi FM na pia kwa Jeshi lako la Polisi hasa la Mkoa wa Dar es Salaam kukaa kimya badala ya Kumkamata DC Jerry Muro kwani Kauli yake hiyo inaweza Kuhatarisha Amani na kukatokea Mzozo wa Kiimani nchini unaowahusu Wakristo (akina Jerry Muro) na Waislamu (akina Haji Manara)

Nakuamini Mheshimiwa Rais wangu Dkt. Magufuli na najua hili hutoliacha lipite hivi hivi. Uwe na Kwaresma njema Mheshimiwa.
 
Kawadharau vipi hapo waislam? Kumwambia Manara akafundishe madrasa? Kwani kufundisha madrasa nayo imekuwa dhambi au jambo ambalo mtu apaswi kuambiwa?

Ni kweli Manara akistaafu anapaswa akafundishe madrasa au angekuwa mkristo tunge mwambia akafundishe walimu wa Kipaimara au Sunday School!


Nimegundua Muro ni kiboko ya Manara

Mtetea Upuuzi nae pia huwa ni Mpuuzi vile vile.
 
Khee...!!! Kuambiwa akafundishe madrasa ndo kudharau..!!!?? Kuna waliokwisha tumbuliwa huku wakiambiwa ATARUDIA KAZI YAKE YA ZAMANI... au atapangiwa kazi mpya.. INA MAANA HAPO KAZI MPYA AU YA ZAMANI ZIMEDHARAULIWA..!!??
 
Tatizo wewe mleta mada ndio umeiweka kwenye imani ndio maana inakuumiza

Nawaaminia Waislamu na najua kama Mheshimiwa Rais atashindwa Kumwajibisha DC wake Jerry Muro basi Wao watamuwajibisha kwa namna yao ya Kipekee kabisa na nitashangaa kuona Waislamu wote nchini Tanzania wanalinyamazia hili. Nawakubali sana Waislamu hivyo msiniangushe katika hili na lazima DC Jerry Muro ama awaombeni Radhi haraka au asubiri yale Maombi yenu Maalum na ya Kipekee ya Wakaidi Kwake Allah ( Mwenyezi Mungu ) Msikubali kabisa Waislamu tafadhali.
 
Nawaaminia Waislamu na najua kama Mheshimiwa Rais atashindwa Kumwajibisha DC wake Jerry Muro basi Wao watamuwajibisha kwa namna yao ya Kipekee kabisa na nitashangaa kuona Waislamu wote nchini Tanzania wanalinyamazia hili. Nawakubali sana Waislamu hivyo msiniangushe katika hili na lazima DC Jerry Muro ama awaombeni Radhi haraka au asubiri yale Maombi yenu Maalum na ya Kipekee ya Wakaidi Kwake Allah ( Mwenyezi Mungu ) Msikubali kabisa Waislamu tafadhali.
Kumbe wewe siyo mwislamu bali uko kisiasa zaidi.

Pole!
 
Bado nashindwa kuelewa ubaya upo wapi!

Kumtumikia Mwenyezi MUNGU Ni sifa na utukufu Sasa wewe unaona ubaya upo wapi?

Manara juzijuzi amekuwa barozi wa kuhifadhi juzuu Kama sijakosea, Manara amekuwa kalama ya ushawishi kufundisha madrasa atafanya watoto wengi wasome dini, ubaya upo wapi.

Wewe uliyeoba Kuna ubaya ndo ibilisi kabisa imeitoa kulikokusudiwa na kupeleka sehemu nyingine. Muogope MUNGU.
 
Umeandika maelezo mengi yasiyokuwa na maana!

Mi ni mwanasimba! Km kunamtu wa kuchukuliwa hatua hapo ni H.Manara!!! Haji ni mchochezi.

Kuambiwa rudi ukafundishe madrasa nitusi kwa uisram??? Mpaka unaitisha vyombo vya habari??

Aliyekuwa mkuu wa Usarama Wa Taifa Tiss ndg Kipilimba aliwahi kuambiwa na wanasiasa wa upinzani chademaa kuwa! Afanye kazi ya kuhubiri injiri aachane na kazi ya usarama wa taifa imemshinda na wakaenda mbari zaidi wakisema ana kanisa je! Hapo napo chadema walitukana ukristo?

Manara aachane na kazi ya usemaji wa club ya simba! Simba ni team kubwa africa ukiwa mwajiriwa team hii uwe mweredi! Mvumirivu! Na hata ukikosewa ujue namna yakufikisha malalamiko kwa wahusika lakini kwa weredi.
Swala lakuitisha vyombo vya habari nakumalizia hasira zake kwa umma je! Manara ni msemaji wa watanzania waisram!

Simba wamchukulie hatua za haraka manara! Ipo cku ataharibu ndani ya simba pakubwa.

Ngoma ikilia sana huishia kupasuka! Manara very soon atapoteza heshma hata hii ndogo aliyonayo.
 
Hajji Manara ni mwalimu wa madrasa.

Sioni tatizo la Muro hapo hata yule Swebe mtangazaji wa E fm ni mwalimu wa madrasa!

Dhihaka hiyo angefanyiwa Mkristo nchi ingetulia sasa? Acheni Unafiki DC Jerry Muro amewadhihaki na kuwadhalilisha Waislamu hasa kupitia Walimu wao wa Madrassa. Waislamu wote nchini Tanzania mkilinyamazia hili nanyi sitokuja kuwaelewa tena kwani hapa mmedhihakiwa vilivyo na sasa muda wa Kudhihakiwa hivi ufikie Kikomo. Msikubali ng'o na Sisi Wakristo tunaopenda Haki tutakuwa nyuma yenu kuwaungeni mkono kwani hata Sisi ( Wakristo tunaojielewa ) tumesikitishwa na kukasirishwa sana na Kauli hizi za Kifedhuli za aliyewahi kuwa Msemaji wa Yanga SC sasa ni Mkuu wa Wilaya Ndugu Jerry Muro.
 
Back
Top Bottom