VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Tunafanya kazi. Tunalima pia. Tuna malengo yetu. Tunapambana na maisha. Tuemewekeza pia. Tunategemea kupata riziki zetu. Mbona hakuna nafuu zaidi ya kuusikia 'ukweli' wako kila siku unapohutubu?
Tunacharika. Tunasafiri huku na kule katika kutafuta.Hatubweteki. Tunadamka mapema na kulala kwa nadra. Pesa hakuna. Mbona mazingira si rafiki katika kutuonesha ubora wa tunachokifanya kihalali kabisa?
Kodi zimetamalaki. Karo za vyuo zimekuwa mizigo yetu. Tunapambana na hayo pamoja na kutimiza malengo tunayojiwekea. Inakuwaje mambo yasifunguke ikiwa Serikali yako ni ya Wasemaukweli na watendaji kwelikweli?
Hotuba zako nzuri. Zimejaa ukweli. Kauli zako ni thabiti,huna kupepesa macho. Maneno na matendo yako yanaogopesha na kutisha wateule wako na kuwasukuma wajitume zaidi na zaidi na hata kwa kuigiza. Kwanini bei za vyakula zipae kila uchao na kuyafanya mambo kuwa magumu?
Tatizo ni nini hasa?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam