Rais Magufuli, ukiwa unatoka Chato pitia Hospitali ya Mlonganzila iliyobatizwa Vingunguti

Hao wanaokufa hovyo hapo mloganzila watakuwa vyama pinzani. Sie wachama chetu mbona tunapona kabisa na kupata huduma nzuri.

cc USSR,State Agent, Mgonjwa Mtambuka.

Umoja wetu ndiyo nguvu yetu dhidi ya watawala kuwafanya wawajibike kutatua changamoto zetu.

Huo uongozi wa hapo sijui unafanya nini, wizara ya afya kama haipo pia.

Sio kila jambo hadi Rais afike kulitatua. Yeye ameshazungumza kwa ujumla watu wachape.

Tutamsubiri tu hadi afike yeye huku watu wakiendelea kufa,maana hatuna viongozi isipokuwa yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza nikupongeze kwa kuweza kuifanya hospitali hii kuwa na hadhi ya kimataifa in terms of infrastructure and human resources ila nikutaarifu tu kuwa wananchi wamepabatiza jina kuwa VINGUNGUTI yaani ni kama machinjio ya mifugo kule vingunguti inaima!

Ni kweli kuwa hospital ya Mlonganzila inapokea wangonjwa walioshindikana katika hospitali nyingine hapa nchini kwa maana ya rufaa ila hapa ni zaidi ya graveyards, mtu kutoka hai/kupona ni nadra sana.

Nikuombe tu pitia pale labda kuna vitu sisi wageni /wapitaji hatujui ila wewe unaweza kupata ukweli

NILICHOSHUHUDIA

Nilikwenda kumwongezea damu kaka yangu nikiwa katika foleni nikaambiwa niende ofisi za juu nichukue form; nikapanda lift hadi eneo husika huko nikakuta madaktari (wako bize na simu na story za simba na yanga wakiume walikuwa kama 4 hivi upande wa pili wa kike walikuwa kama 5 hivi) wote vi vijana wa mjini mjini hivi na viduku kibao. Nikaambiwa anayetoa form hayupo nisubiri mimi na wenzangu tukaelekezwa bench tukae tukiwa hapo akaja mama mtu mzima akawaita wale madaktari wakawa kama na kikao kidogo wakiwa wamesimama yule mama akaanza kusema tena kwa sauti akiwakaripia wale vijana kwa uzembe na kusema deaths zimezidi yaani usiku mmoja wamekufa watu wote wale watu kumi na mmoja sio normal. Wakati anafoka daktari mmoja akajibu kuwa ni kweli uzembe umezidi wakaanza kurushiana maneno huku sisi tukishangaa. Akawa anawaonya kuhusu kutoroka na kwenda mtaani usiku na kuwaachia wagonjwa manesi. Inauma hii ni live nasikia tena kutoka kwa madk wenyewe.

Baadae akaja nurse akatuita akatupa form, ndugu yangu alikuwa amepata ajali ya mguu hivyo sikuwa na hofu sana na alikuwa amekaa pale siku tano akifanyiwa stretching maana aliumia kifundo cha mguu ila cha kusikitisha alivyoingia chumba cha upasuaji hakutoka mzima. Inauma sana hii, mguu hadi kifo vipi ingekuwa moyo, kichwa au uzazi!

Usiombe kufika pale, usikubali kulazwa pale, Mlonganzila ni zaidi ya Mwananzila! Mh Rais pale kuna majipu sio mchezo kila mtu analia heri ubaki Mwananyamala, Temeke au Muhimbili sio Mlonganzila. Vijana wanajifunzia udaktari kwenye miili ya wapendwa wetu.

USSR

====

Soma pia:
Haya yanayosemwa kuhusu Hospitali ya Mloganzila ni kweli?
na
Mloganzila yakanusha juu ya taarifa za vifo vya wagonjwa

Hizi taarifa siyo za kweli jamani , Uongozi wa Hospitali umekuja na takwimu , vifo vimepungua.
IMG_20200106_142658_234.jpg
IMG_20200106_142658_235.jpg
 
They don't care mkuu wako na utoto mwingi nikikumbuka yule Dada anawaonesha madk wenzake picha kwenye simu eti yule mchepuko alipigwa chini na jamaa huyu hapa ,wote wakarundikana kungalia picha na story zikaanzia hapo sisi tupo kwenye mstari tunasubili wao wanaoneshana picha za michepuko ,wapuuzi sana hata ndugu yangu kafa kwa uzembe tu

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwanza nianze na kuzungumzia maana ya jina MLOGA NZILA! Kwa watu wanaotoka kanda ya ziwa kina Mayala watanielewa. Neno MLOGA lina maana ya MLOZI(MCHAWI) na NZILA lina maana ya NJIA. Hivo unaposema Mloganzila una maana ya kusema mtu anayeroga njia...!!!Sina hakika nani aliamua Hospitali kubwa kama hii ipewe jina la hovyohovyo kama hilo. Kwanini pasingeitwa jina kama:MWALIMU NYERERE MEMORIAL HOSPITAL? Kuna imani huwa wanasema majina ya roho! Isije ikawa jina linakula vichwa vya watu
.
Baada ya kusema hayo nichangie mada. Hapa inaonekana kuna wapuuzi fulani ambao sitaki kuamini kuwa ni Timu Magufuli wanataka kutetea UJINGA na kupoteza hoja muhimu hapa...!! Mtu ana payuka kama kanywa gongo ati kufia Hospitali ni kawaida ndo maana kuna Mochwari kila hospitals...!!Hizi ni akili za matope na lazima zikemewe kwa nguvu zote!
Hivi hawa vichaa wanajua maana ya Referral Hospital? Kama wagonjwa wanakufa wanapopelekwa kwa rifaa basi hiyo siyo Referral Hospital tena baali ni Mortuary Hospital! Kwamba mgonjwa anaondolewa Mwananyamala au Amana anapelekwa Mloganzila kwenda kuhifadhiwa mortuary na siyo kupata matibabu bora zaidi kutoka madaktari Bingwa na Bora zaidi!!

Tatizo la nji hii kwa sasa kumejaa wanafiki na wapuuzi wakubwa hasa wale ambao wananufaika na Utawala huu wa A5. Hawataki kabisa kusikia Serikali hii inakosolewa aidha kwa huduma mbovu zinatolewa kwene Taasisi au Utawala unaokiuka na kuvunja misingi ya binadamu..
 
Haya mauwaji ya wagonjwa hayataisha mpaka CCM ing'oke madarakani

Kuna ukweli kwa asilimia kubwa katika kauli yako!
CCM wameingiza siasa katika kila kitu hata mambo nyeti kama huduma za afya..!!!Kila kitu ni kupiga siasa na kumsifia Bwana mkubwa hata kama kuna madudu yanafanyika...!!!Hapa ndipo ile kauli na tafasiri ya Mhe. Msigwa kuhusu MWENDAWAZIMU inapoleta maana!
Kufanya jambo lilelile kila siku kwa kutegemea matokeo tofauti. CCM ni walewale na wanafanya mambo yaleyale halafu Watz wanategemea wapate matokeo tofauti...Never! Kuendelea na CCM ni sawa na UWENDAWAZIMU kwa 100%.
 
Kuna ukweli kwa asilimia kubwa katika kauli yako!
CCM wameingiza siasa katika kila kitu
CCM haiko serious na maisha ya Mtanzania wamefikia hadi kwenda kuwapiga risasi kama mvua Wabunge wa Upinzani halafu wanawaambia wakatibiwe Mloganzila sasa hebu niambie Mhe Tundu lissu angepekekwa hapo ati kwa Wazalendo
 
Tutawalaumu madaktari bure lakini ukiingia kiundani unadhani kwa nini hawafanyi hivyo hospital za binafsi? Mishahara yao ni sh. Ngapi? Tangu lini hawajaongezwa mishahara, watapata wapi motivation?

Wengine hapo walikuwa ni Clinical officers wakaenda jiendeleza kwa level za degree wamerudi scale za mishahara zipo pale pale na mkuu hana nia ya kuongeza, wakidai watajikuta lupango kwa makosa ya utakatishaji fedha Sasa nani ajitume happy?

Na sisi wananchi tunawapigia makofi daily wanasiasa. Tusifu na kuabudu ila tujue na matokeo yake.
Issue ya uhai wa binadamu ni muhimu sana, huwezi weka mgomo baridi kwa sababu tu hujaongezewa mshahara. Hilo tuwaachie kada zingine kwani kupoteza uhai wa mtu mmoja kwa nchi zetu hizi ni kuwaachia majanga wategemezi.
 
CCM inaweza kuyamaliza haya ,kama ccm itashindwa hakuna chama kinaweza

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app

USSR,
Taifa lililojifia kitambo (we have RUSSIA now and not USSR!)
Naomba uache propaganda za kichizi. CCM tunayo tangia Uhuru kama TANU(1961) na ikabadilisha jina kuwa CCM(1977).
Majitu yaleyele, tabia ni zilezile, sera ni zilezile na uoza ni uleule. Kubadilisha jina hakubadilishi tabia(characters) ya mtu.
Hivo CCM hawana jipya na usitegemee kumaliza matatizo lukuki ya nji hii!
 
CCM haiko serious na maisha ya Mtanzania wamefikia hadi kwenda kuwapiga risasi kama mvua Wabunge wa Upinzani halafu wanawaambia wakatibiwe Mloganzila sasa hebu niambie Mhe Tundu lissu angepekekwa hapo ati kwa Wazalendo

Well said.
Hizi hospitali za Bongo hazina ubingwa wowote zaidi ya kubahatisha. Kama unataka kuthibitisha hilo angalia viongozi wa CCM, Serikali na Wanasiasa wa upinzani wanapoumwa utasikia wako Sauz, India au China. Wanajua wakienda Mlonganzila au Muhimbili ni kuchukua Death Certificate from Mortuary Hospitals....!!!
 
Ila hawana mbadala maana ukiona wapinzani walivyo bure kabisa unaogopa

State agent

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa sehemu sikubaliani na hoja yako kuhusu wapinzani...!!.
Unaposema wapinzani ni bure kabisa unatumia kigezo gani?
Kumbuka tangu nji hii ianze mfumo wa vyama vingi Wapinzani hawajawahi kuchukua Ikulu! Kipimo ni mtu apewe Ikulu, afanye implementation ya sera zake zishindwe ndipo tujue hawezi...!!!CCM wamepewa Ikulu mara lukuki lakini hatuoni mabadiliko yoyote zaidi ya kuji-mwambafy!
 
  • Thanks
Reactions: prs
Suala la mgonjwa wako kufa, pole kwanza kwa kufiwa. Lakini ungeuliza zaidi kuhusu sababu ya kifo. Si kweli kwamba ajali ya mguu haiwezi kumuua mtu. Unajua average blood loss of a femur? Inaeza muua mtu hasa kama alichelewa kupata blood replacement.
Ndio maana hospitali zinatakiwa kuwa na ‘blood bank’ ya kutosha. Sio mtu anamleta mgonjwa wake unamwambia akatoe damu kwanza kama vile muda una msubiri mgonjwa nae.

The bottom line ni uzembe na a lot has to change kwenye utoaji wa huduma.
 
Kuna jamaa anaitwa mashinji kakimbia leba kaenda kuhesabu wanachama wa Bavicha chadema hawana utu na nchi hii


State agent

Sent using Jamii Forums mobile app

State agent bado huna hoja.
Dr. Mashinji kafanya kosa gani kuhesabu wanachama? Mbona humsemi Dr. Hussein Mwinyi anayehesabu Wanajeshi wapiga kwata?Mbona hujamtaja Dr. Kebwe Steven Kebwe aliyekuwa RC Morogoro ambaye kazi ya u-RC ilimshinda mpaka akatumbuliwa? Kwanini hajarudi leba kuzalisha kina mama wajawazito? Kuna mafisi wengi tu wa Lumumba wame acha taaluma zao kwenda kuganga njaa kwenye siasa...na wanashindwa ku-deliver kwa vile hizo siyo taaluma zao!
 
Back
Top Bottom