Rais Magufuli, ukiwa unatoka Chato pitia Hospitali ya Mlonganzila iliyobatizwa Vingunguti

Gallius

JF-Expert Member
Aug 24, 2019
974
1,000
Yaani kifundo kinaua? hii ni hatari Mimi ni daktari ila kuna cases ambazo zinaweza pelekea mgonjwa kufariki ila sio kifundo cha mguu...

Nyepesi nyepesi ni kwamba hospitali hiyo ya Mlongazila imejaa hawa madaktari wa internship ambao mara nyingi wanakua hawako competate katika baadhi ya cases ambapo mara nyingi hupelekea wagonjwa kufariki...

Pia ni vyema serikali ikajitathimini kwa hili haiwezekani iwekeze fedha nyingi katika kuboresha miundombinu ya hapo mlongazila halafu isahau kupeleka wataalamu wenye ujuzi wa kutosha na hivyo kupelekea hospitali hiyo ya mloganzila kupoteza sifa stahiki...

Ni vyema hata kama kuna wanafunzi wa intern wawe under monitoring na madakatri wazoefu sio kuwaachia hao wanafunzi kila kitu ndio maana vifo vinaendelea kuwepo hapo...

Pia hawa vijana ( Madkatri) wa sasa hawana ule wito wa kuhudumia wagonjwa ipasavyo unakuta hawa madaktari barobaro wanatanguliza maslahi yao mbele kuliko wagonjwa hili linaumiza sana, mara nyingi huwa najiuliza kile kiapo wanachokula pindi wanahitimu kina maana gani...

Serikali iwe makini na hawa madakatri vijana maana ndio wanaipaka matope hiyo hospitali...

Sent using Jamii Forums mobile app
 

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,281
2,000
Mshauri ndugu yako UssR atafute pesa aende hospital za private, Achana na hospital ya Chadema mlongazila

Kumbe mnabwatuka hapa JF halafu ni maskini wa kutupwa

Wewe ni Certified Idiot, Hospital ya Chadema na madaktari wa Chadema mnawafuata hapo mlongazila

Nenda kwenye hospital za ccm huko Appolo India na Marekani
Hahahah navyojua Mimi ukiwa jela imekula kwako hakuna cha kutoka kwenda kwenye sherehe au msiba


State agent

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Bikini

JF-Expert Member
Oct 16, 2018
328
500
Watumishi hawana morali hawana nyongeza za mishahara,vyeo,nk ndo umuharibia anaweza akawa na nia njema akajikuta ngoma anacheza mwenyewe wengine kuwa wapenzi Wa tazamaji.Awaboreshee watumishi hali zao nao wataongeza tija,asikamue ng'ombe bila kuwalisha
Kibongo bongo hata upewe mamilioni mkuu ukishashiba uvivu uko pale pale ... Zaidi sana hizo taaluma ndo zimejaa umalaya tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

state agent

JF-Expert Member
Jul 1, 2019
1,770
2,000
Tangu uvunje ungo akili zimekuruka ,uadhadhani waotibiwa private ndio wenye pesa au huko private watu hawafi

Matajili wote wa nchi hii wanafia muhimbili kwani mamako alikwambia pale ni private nyau wewe


State agent
Mshauri ndugu yako UssR atafute pesa aende hospital za private, Achana na hospital ya Chadema mlongazila

Kumbe mnabwatuka hapa JF halafu ni maskini wa kutupwa

Wewe ni Certified Idiot, Hospital ya Chadema na madaktari wa Chadema mnawafuata hapo mlongazila

Nenda kwenye hospital za ccm huko Appolo India na Marekani

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Undu

JF-Expert Member
May 18, 2013
2,496
2,000
Ile hospitali wamejaa wanafunzi na inakosa madaktari bingwa.Chakufanya ni kuipandisha hazi na kuwa hospitali ya taifa ya watoto nchini .ili watato na wajawazito wote waondolewe muhimbili walazwe mloganziliwa.
 

Allency

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
6,473
2,000
Kwanza nikupongeze kwa kuweza kuifanya hospitali hii kuwa na hadhi ya kimataifa in terms of infrastructure and human resources ila nikutaarifu tu kuwa wananchi wamepabatiza jina kuwa VINGUNGUTI yaani ni kama machinjio ya mifugo kule vingunguti inaima!

Ni kweli kuwa hospital ya Mlonganzila inapokea wangonjwa walioshindikana katika hospitali nyingine hapa nchini kwa maana ya rufaa ila hapa ni zaidi ya graveyards, mtu kutoka hai/kupona ni nadra sana.

Nikuombe tu pitia pale labda kuna vitu sisi wageni /wapitaji hatujui ila wewe unaweza kupata ukweli

NILICHOSHUHUDIA

Nilikwenda kumwongezea damu kaka yangu nikiwa katika foleni nikaambiwa niende ofisi za juu nichukue form; nikapanda lift hadi eneo husika huko nikakuta madaktari (wako bize na simu na story za simba na yanga wakiume walikuwa kama 4 hivi upande wa pili wa kike walikuwa kama 5 hivi) wote vi vijana wa mjini mjini hivi na viduku kibao. Nikaambiwa anayetoa form hayupo nisubiri mimi na wenzangu tukaelekezwa bench tukae tukiwa hapo akaja mama mtu mzima akawaita wale madaktari wakawa kama na kikao kidogo wakiwa wamesimama yule mama akaanza kusema tena kwa sauti akiwakaripia wale vijana kwa uzembe na kusema deaths zimezidi yaani usiku mmoja wamekufa watu wote wale watu kumi na mmoja sio normal. Wakati anafoka daktari mmoja akajibu kuwa ni kweli uzembe umezidi wakaanza kurushiana maneno huku sisi tukishangaa. Akawa anawaonya kuhusu kutoroka na kwenda mtaani usiku na kuwaachia wagonjwa manesi. Inauma hii ni live nasikia tena kutoka kwa madk wenyewe.

Baadae akaja nurse akatuita akatupa form, ndugu yangu alikuwa amepata ajali ya mguu hivyo sikuwa na hofu sana na alikuwa amekaa pale siku tano akifanyiwa stretching maana aliumia kifundo cha mguu ila cha kusikitisha alivyoingia chumba cha upasuaji hakutoka mzima. Inauma sana hii, mguu hadi kifo vipi ingekuwa moyo, kichwa au uzazi!

Usiombe kufika pale, usikubali kulazwa pale, Mlonganzila ni zaidi ya Mwananzila! Mh Rais pale kuna majipu sio mchezo kila mtu analia heri ubaki Mwananyamala, Temeke au Muhimbili sio Mlonganzila. Vijana wanajifunzia udaktari kwenye miili ya wapendwa wetu.

USSR

====

Soma pia:
Haya yanayosemwa kuhusu Hospitali ya Mloganzila ni kweli?
na
Mloganzila yakanusha juu ya taarifa za vifo vya wagonjwa
Kuna doctor mmoja ni rafiki yangu yuko pale, aisee yani huwezi amini kama ni doctor, yuko yuko tu mda wote yuko mtaani tu tena kalewa chakari. Ni kijana mdogo sana na swala la kutoroka kazini kwenda kwenye gambe kawaida sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
15,615
2,000
Wewe utakuwa mpiga dili au CDM mawakala wa mabeberu nyie, mnataka kuichonganisha Serikali na Wananchi..Watu kama nyie ndio mnamkatisha tamaa Rais wetu kipenzi..

Awamu ya tano chini ya Jemedari Dr JPM haiwezi kuwa na uzembe wa hivyo, nidhamu kwa sasa imerudi makazini, watu wanawahi makazini na wanapiga kazi kama mchwa, heko awamu ya tano, heko Rais wetu kipenzi Dr JPM..
Mishahara yao mtaongeza lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,115
2,000
Kuna jamaa yetu tulikuwa tunakunywa naye kahawa akapata ajali akavunjika mguu akalazwa hapo Mloganzila alikuwa mzima wa afya watu wamemtolea damu akafanyiwa operation hakurudi tumebaki na sauti yake akiekezea jinsi ajali alivyoipata

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
15,615
2,000
Boss USSR Pole sana Mkuu kwa kadhia uliyopata.

Nakumbuka hata Utawala wa JK kuna Kashfa iliwahigi kutoka kuhusu Hospitali hii.

Mimi binafsi nashangaa, pamoja na Ukali wa Mh. Rais lakini Viongozi na Watumishi ni vichwa ngumu, Ufisadi ndio kwa kwenda mbele, madudu kila kona. Sijui ndio wanamkomoa au ndio wamekata tamaa na maisha.
Huwezi kufanya kazi kwa moyo kama mshahara hauongezwi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,814
2,000
Mishahara yao mtaongeza lini?

Sent using Jamii Forums mobile app

Wachape kazi tunajenga nchi kwa manufaa ya wajukuu zao, wewe huoni fedha zinazokwenda kujenga MASGR, Kufufua mareli ya zamani mpaka Diamond anakwenda Kigoma kwa train, huoni Madege tuliyonunua, huoni Stiggler's ujenzi umeanza kwa kasi mno, mabarabara nchi nzima, vituo vya Afya.. Wavumilie tu neema inakuja na wenyewe watafurahi kweli. Awamu ya tano inatumikia wanyonge..
 

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
1,922
2,000
Hahahah navyojua Mimi ukiwa jela imekula kwako hakuna cha kutoka kwenda kwenye sherehe au msiba


State agent

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa aliyeleta mada hii ni mpiga dili na anashirikiana na mabeberu wala ndugu yake hajafa, anataka tu kuichafua serikali hii ya awamu ya 5 ambayo umejipambanua katika kutokomoza umaskini. Tumethubutu, tumeweza na sasa tunasonga mbele. Hapa kazi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Gallius

JF-Expert Member
Aug 24, 2019
974
1,000
Labda itakuwa dawa ya usingizi mkuu


State agent

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio hapo nakuambia, hao madaktari wa intern unakuta bado vichwa ni vyepesi. Bado hawajaiva kwenye Anaesthesiology ndio maana nikatoa ushauri haipendezi kuwaachia kila kitu wafanye wao yapaswa wawe chini ya uangalizi...

Though bado inatia shaka kweli, how come one qualify to be a medical doctor, halafu protocol za Anaesthesia zisumbue? kuna shida kubwa sana hapo na kama wanaona injectable anaesthetics zinawasumbua basi wajitahidi watumie inhalant anaesthetics...

Pia naona siku hizi kuna utitiri wa vyuo vingi vinavyotoa kozi za udaktari na ukifuatilia kwa undani zaidi unakuta waalimu husika hawana vigezo husika ama walimu wakongwe wapo kule kibiashara zaidi wanaogopa kuwakazia hawa watoto ili waendelee kuvuta mishahara...

Mwisho wake ndio huu kuzalisha madaktari ambao uwezo wao unatia shaka kiasi...

Hili lipo kwa hosppitali nyingi tu za private, maana hawa vijana waliomaliza vyuo ndio wamejazana huko..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom