Rais Magufuli, ukitekeleza mambo haya matano, niko tayari kuunga mkono juhudi zako

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
1,502
Points
2,000

Keynez

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
1,502 2,000
Mhe. Rais Magufuli,

Nianze kwanza kwa kukiri kuwa kuna mambo makubwa mazuri ambayo unayafanya. Lakini pia kuna mambo makubwa tu yanayochafua utawala wako.

Wengi wetu tukiangalia mabaya yanayotokea tunapata kigugumizi na ukakasi wa hata kusifia mazuri yako. Naomba sana uliangalie hili na ukifanya hivyo nakuhakikishia utapata sifa ambazo haukutegemea hata kutoka kwa wapinzani wako. Na tutafanya hivyo bila kurubuniwa wala kushurutishwa.

Uchunguzi wa matukio ya mauaji na utekaji
Nianze kwa kusema hili linaweza kufanyika bila kukuchafua wewe. Marais siku zote mna special privileges linapokuja masuala ya kashfa. Toka enzi za Nyerere, njia mbalimbali zimetumika kumlinda Rais dhidi ya kashfa ila UKWELI fulani lazima utolewe na mamlaka husika. Hili ni muhimu sana hata ikibidi kutoa watu fulani kafara. Ikionekana vyombo vya ulinzi vimehusika, waathirika walipwe fidia na tusonge mbele kama taifa. Haya mambo hayatusaidii wala hayakusaidii wewe.

Futa na acha uundwaji wa sheria mbovu na kandamizi
Imekuwa ni kawaida miaka hii ya karibuni kwa sheria za ajabu sana kutungwa. Ni kweli kuna watu walikuwa wanaziabuse baadhi ya sheria zilizokuwepo ila kwa jinsi zinavyotungwa sasa ni kama kukomoana na zinaturudisha nyuma saaana. Siwezi kukusupport ninapoona vitu kama hivi.

Tundu Lissu
Tafuta njia ya kutafuta amani na mtu huyu. Sijali kama haya mambo yatafanyika nyuma ya pazia ila tafadhali sana. Ikibidi muombe msamaha kwa yaliyomkuta hata kama hautachukua lawama za moja kwa moja kwa yaliyomkuta kwa sababu mwisho wa siku vyombo vyako vya ulinzi na usalama vilishindwa kumlinda hata pale alipotoa taarifa. Hilo tu linatosha kuhitaji maelezo ya kutosha kutoka kwako au wasaidizi wako.

Ikibidi serikali imlipe fidia na ukurasa wa yaliyotokea ufungwe rasmi. Siyo lazima mjenge urafiki wa karibu naye ingawa kuna vitu mnafanana sitashangaa hilo likitokea kwa jinsi muda unavyokwenda na mkipata nafasi ya kufanya kazi kwa karibu. Tundu Lissu ana mengi sana ya kukusaidia. Lainisha shingo yako, utaliona hilo.

Vigogo wa CCM na Watumishi wa Serikali
Endelea kuwabana mbavu vigogo na mafisadi wa CCM. Ikibidi weka ndani yeyote anayekukwamisha. Wananchi tupo na wewe kwenye hilo.

Pia endelea kuimarisha nidhamu ya watumishi wa umma wafanya kazi kwa weledi na kuwaheshimu wananchi wanaowahudumia. Usisahau kuwalipa stahiki zao kwa mujibu wa sheria bila kuwapunja au kuwadhulumu.

Pia iongezee meno TAKUKURU ili iweze kufanya kazi zake bila kuingiliwa na utashi wa watu fulani. Taasisi hiyo inabidi ifike mahali iweze kufanya uchunguzi na kufungua mashitaka bila kuingiliwa na mtu au taasisi yoyote. Tuige utaratibu kama wa FBI (ingawa na wenyewe walipitia changamoto hizi hizi zinazoikabili TAKUKURU leo).

Biashara
Endelea kufanya juhudi za makusudi kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini. Kuanzia taratibu za kufungua biashara, sheria za leseni, za kodi, zote hizo inabidi zifumuliwe ziwe rafiki kwa pande zote. Turudi kwenye dhana kwamba sekta binafsi ni wadau siyo maadui wa serikali.

Katiba Mpya
Hapa tena narudi kwa Tundu Lissu. Baada ya uchaguzi wa 2020, mpe jukumu la kuunda katiba mpya. Zoezi hilo likianza mwanzoni mwa mwaka 2024, linaweza kukamilika ndani ya mwaka mmoja. Nawaza siku ya sherehe za Muungano April 2025, wewe Mhe. Rais ukipokea na kusaini Katiba mpya kutoka kwa Mhe. Lissu. Litakuwa ni tukio kubwa la kihistoria na utajijengea heshima kubwa.

Uchaguzi wa 2025
Achana na mawazo au ushauri wowote wa kuongeza muda wa Urais. Ukifanya hayo niliyopendekeza hapo juu, na ukastaafu kwa amani, wananchi wengi na hata mimi binafsi tutakuja Chato kukupongeza kwa kazi nzuri. Utakumbukwa kwa vizazi vingi vijavyo.

Ni hayo tu.
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Messages
7,162
Points
2,000

Pythagoras

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2015
7,162 2,000

Akiweza hata moja tu katika haya namuunga mkono, mambo yoote anayofanya ni Futility tu na ndio maana bado watanzania hawamkubali analazimisha kuungwa mkono kwa mtutu na sasa kahamia kwa wazee wa matunguli 900.
 
Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
1,502
Points
2,000

Keynez

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
1,502 2,000

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Messages
1,502
Points
2,000

Keynez

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2007
1,502 2,000
Akiweza hata moja tu katika haya namuunga mkono, mambo yoote anayofanya ni Futility tu na ndio maana bado watanzania hawamkubali analazimisha kuungwa mkono kwa mtutu na sasa kahamia kwa wazee wa matunguli 900.
Ni kweli haya ni mambo mazito na magumu lakini tusikate tamaa. Tuendelee kumkumbusha yale tunayotaka yawe. Mengine akionyesha nia ya dhati ya kurekebisha tuwe tayari kusamehe na kusonga mbele kama taifa.
 
ikipendaroho

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2015
Messages
2,878
Points
2,000

ikipendaroho

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2015
2,878 2,000
Ni kweli haya ni mambo mazito na magumu lakini tusikate tamaa. Tuendelee kumkumbusha yale tunayotaka yawe. Mengine akionyesha nia ya dhati ya kurekebisha tuwe tayari kusamehe na kusonga mbele kama taifa.
Chato iwe jiji la kileo kuliko Dar. Tushachoka sote kukusanyika sehemu moja tu. Na sisi wa Dar tunataka watoto wetu wabadilishe mazingira na walioko maeneo mengine wapungue kuja Dar!
 
Forum statistics

Threads 1,392,922
Members 528,739
Posts 34,122,191
Top