Uchaguzi 2020 Rais Magufuli, ukishindwa uchaguzi uko tayari kukabidhi Ikulu?

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Rais Magufuli kama mgombea wa Chama tawala, anatakiwa kutoa tamko la kukubali matokeo kwa namna yoyote yatakavyokuwa. Itakuwa jambo la hekima kujitokeza hadharani na kuonesha msimamo wake.

Mpinzani wake mkuu, Lissu, ameshasema kuwa akishinda au kushindwa kwa haki, yupo tayari kukubali matokeo.

Wote hawa wanaamini watashinda, lakini je Magufuli ukishindwa utakubali?

TUNAOMBA MSIMAMO WAKO KWA HILI
 
Magufuli hata akishindwa uchaguzi na figisu zake zote ni king'ang'anizi hivyo ni ngumu sana kuwa tayari kuachia madaraka.

Kwa kipindi chake tu hiki cha kwanza cha miaka 5 ameonyesha kila dalili za kutaka kuwa Rais asiye na ukomo wa madaraka.

Watanzania tuamke Magufuli anaharibu nchi.
 
Rais Magufuli kama mgombea wa Chama tawala, anatakiwa kutoa tamko la kukubali matokeo kwa namna yoyote yatakavyokuwa. Itakuwa jambo la hekima kujitokeza hadharani na kuonesha msimamo wake.

Mpinzani wake mkuu, Lissu, ameshasema kuwa akishinda au kushindwa kwa haki, yupo tayari kukubali matokeo.

Wote hawa wanaamini watashinda, lakini je Magufuli ukishindwa utakubali?

TUNAOMBA MSIMAMO WAKO KWA HILI
Itategemeana na nani kashinda ,ikiwa Maganja au shibuda mbona anaachia kwa mbwembwe kabisa
Shida itakuja ukiwa lissu atashinda mzee jiwe atafikiri juu ya mayanga construction company ,25000 hekari ,Mauza uza ya Acacia sijui wasiojulikana ataamua bora waniulie kwa kiti
 
JPM kushindwa u Rais , ni sawa na jua lianze kutoka magharibi kwenda mashariki, au mvua ianze kunyesha kutokea ardhini kwenda mawinguni au mwezi uanze kuangaza mchana na jua usiku.

Epukeni kujipa matumaini hewa ambayo hapo baadae yatawaacha na simanzi kubwa huku mioyo imejaa machozi kwa kutokuamini kile kilichotokea
 
Anajipigia kura mwenyewe? Kumbuka kipindi hiki wapiga kura wote wanavaa uhusika wa 'wajumbe'. Wajumbe siyo watu, usijiapize ndugu.
 
Magufuli hata akishindwa uchaguzi na Figisu zake zooote Ni king'ang'anizi hivyo ni ngumu sana kuwa tayari kuachia madaraka.

Kwa kipindi chake tu hiki cha kwanza cha miaka 5 ameonyesha kila Dalili za kutaka kuwa Raisi asiye na ukomo wa madaraka.

Watanzania tuamke magufuli anaharibu nchi.

Comrade acha kabisa kuwa mpiga ramli chonganishi. Kwasababu Mbowe ameonyesha kila dalili ya kuwa mwenyekiti asiyekuwa na ukomo wa madaraka haimaanishi kuwa Magufuli naye anataka kufanya ivyo. Ccm tuna utamaduni wa kupokezana vijiti.
 
Rais Magufuli kama mgombea wa Chama tawala, anatakiwa kutoa tamko la kukubali matokeo kwa namna yoyote yatakavyokuwa. Itakuwa jambo la hekima kujitokeza hadharani na kuonesha msimamo wake.

Mpinzani wake mkuu, Lissu, ameshasema kuwa akishinda au kushindwa kwa haki, yupo tayari kukubali matokeo.

Wote hawa wanaamini watashinda, lakini je Magufuli ukishindwa utakubali?

TUNAOMBA MSIMAMO WAKO KWA HILI
Hakuna Interview anayo ikubali Magufuli hapa ndio utajua kuwa jamaa ni muoga sana, kauli kama hizi maisha magufuli hawezi kutoa yeye anajua tu kuwa lazima aendelee kutawala kitu ambacho sio kabisa
 
Anajipigia kura mwenyewe? Kumbuka kipindi hiki wapiga kura wote wanavaa uhusika wa 'wajumbe'. Wajumbe siyo watu, usijiapize ndugu.
Mara zote huwa napenda kuwakumbusha wakati wa uboreshaji wa taarifa kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.

CCM ilihamasisha sana watu wake tofauti na nyie mlikuwa mnawaambia wagomee, tena wengine walikuwa wanapost picha mitandaoni kwa furaha kabisa kwamba vituoni hakuna watu na hilo ndio litawagharimu, msitegemee kupata ushindi eti kutoka kwa wana CCM wanaomchukia JPM
 
Itategemeana na nani kashinda ,ikiwa Maganja au shibuda mbona anaachia kwa mbwembwe kabisa
Shida itakuja ukiwa lissu atashinda mzee jiwe atafikiri juu ya mayanga construction company ,25000 hekari ,Mauza uza ya Acacia sijui wasiojulikana ataamua bora waniulie kwa kiti
Ha ha ha ha daaah mkuu umetulia kubwa mno kufikiri !Hakina ndivyo ilivyo
 
Mara zote huwa napenda kuwakumbusha wakati wa uboreshaji wa taarifa kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.

CCM ilihamasisha sana watu wake tofauti na nyie mlikuwa mnawaambia wagomee, tena wengine walikuwa wanapost picha mitandaoni kwa furaha kabisa kwamba vituoni hakuna watu na hilo ndio litawagharimu, msitegemee kupata ushindi eti kutoka kwa wana CCM wanaomchukia JPM
Kwani kuna mtu anamchukia Magufuli? Kumchagua mtu siyo mapenzi, ni wananchi wanaona ni mgombea gani anaweza kuwaletea ahueni ya maisha kwa kuweka sera rafiki.....Kama huko mnachaguana kwa kupendana endeleeni.
 
JPM kushindwa u Rais , ni sawa na jua lianze kutoka magharibi kwenda mashariki, au mvua ianze kunyesha kutokea ardhini kwenda mawinguni au mwezi uanze kuangaza mchana na jua usiku.

Epukeni kujipa matumaini hewa ambayo hapo baadae yatawaacha na simanzi kubwa huku mioyo imejaa machozi kwa kutokuamini kile kilichotokea
Huwa mnafikiria nini mnaposema atashinda tuu.
 
Kwani kuna mtu anamchukia Magufuli? Kumchagua mtu siyo mapenzi, ni wananchi wanaona ni mgombea gani anaweza kuwaletea ahueni ya maisha kwa kuweka sera rafiki.....Kama huko mnachaguana kwa kupendana endeleeni.
Mkuu amini nikwambiacho na akili yako uanze kuiandaa kisaikolojia kuwa JPM mitano tena, bila matusi wala nini
 
Hili swali lingekuwa valid kama angekuwepo mtu wa kushindana nae.

Waliopo ni wakamilishaji wa ratiba tu, alimradi ifike siku ya kura kupigwa.
 
Back
Top Bottom