Rais Magufuli: Ukiikataa bajeti, usiniombe" je ukiikataa sheria hupaswi kuifuata?

GreenCity

JF-Expert Member
May 28, 2012
5,616
4,260
MHESHIMIWA RAIS, nadhani ifike kipindi uanze kutumia hotuba za kuandika.
Muda huu ukiwa Tarime nimeskia ukimwambia mbunge wa upinzani Esther Matiko kuwa, kwa kuwa huwa wanakataa kupitisha bajeti bungeni, basi hapaswi kumuomba rais utekelezaji wa maendeleo jimboni kwake. Hii ni aibu!

Pamoja na castle zangu kichwani, nikajiuliza je, mbunge wa upinzani akikataa kupitisha sheria bungeni na ikapitishwa na wabunge wa chama tawala, huyo wa upinzani hapaswi kuitekeleza?

Kwenye hii ziara ya rais kanda ya ziwa, nimeskia kauli za utata kwa Mheshimiwa rais. Mheshimiwa rais naomba uandikiwe hotuba na uizingatie.

Katika majimbo mengi aliyopita ni kwa John Heche amehoji matumizi ya mfuko wa jimbo! Nina imani ataendelea kufanya hivyo kwa majimbo yanayofuata! Ni swali zuri!

Mungu ibariki Tanzania!
 
Kwenye hii ziara ya rais kanda ya ziwa, nimeskia kauli za utata kwa Mheshimiwa rais. Mheshimiwa rais naomba uandikiwe hotuba na uizingatie.


Wakimuandikia, mengine watakwepesha, bora twende hivihivi, yaliyofichika yafichuliwe
 
Huna jipya. Kilichobaki tuwaoe Dada zenu ili mtuheshimu nyie ma CHADEMA
Rais asipoangalia atapanda chuki! Kuoana sio vibaya, lakini aliposema mkurugenzi aoe dada wa mbunge wa upinzani ili kumkomoa, ni kauli mbaya! Tuipinge!
 
Rais asipoangalia atapanda chuki! Kuoana sio vibaya, lakini aliposema mkurugenzi aoe dada wa mbunge wa upinzani ili kumkomoa, ni kauli mbaya! Tuipinge!
Sasa ulitaka asemeje. We huoni Mbunge hakufuata utaratibu kumwita DED wake wakati kuna namna nzuri ya kumshitaki kwa Rais. Je angekuwa Shemeji yake angeropoka mbele ya Rais.
 
Usitegemee kusikia jambo lolote la maana kutoka kwa hili jiwe kwa wakati huu na ujao, amefikia hatua ya mwisho kabisa ya hali inayomsumbua (ukichaa) ambayo aliitamka yeye mwenyewe pasipo kushinikizwa na mtu.

Subiri miujiza tu kuinusuru hii nchi kwa kipindi hiki, maana anaweza akafanya maamuzi yoyote ya hovyo kutokana na hali yake akahisi yupo sahihi, kitakacho tunusuru ni 2020 tu.
 
Sasa kama wanakataa kupitisha bajeti wa nadhani hayo wanayoyaomba yangetoka wapi?
kuna haja gani ya kupoteza muda na pesa za serikali kulipa wabunge kujadili kitu ambacho hawaruhusiwi kutoa ampendekezo yao ambayo nyie mnayaita kupinga? kwanini waziri na wataalamu wake wasiandae bajeti kisha wataisoma kwa wananchi.
 
Ila alikubali ni sehemu ya demokrasia,pia anajua ni lazima atoe fedha..hili swala kaligusa kisiasa Mwenye masikio aambiwi sikia bali umeelewa..Rais anafahamu Tarime watu hawachagui Chama tu bali mtu wanaemtaka, akacheza karata yake ya kisiasa..
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom