Rais Magufuli, ufufuaji wa sekta ya uvuvi uende sambamba na ulinzi na usalama wa uvuvi haramu

kidumpure

Member
Jul 2, 2020
16
23
Kipindi cha korona wengi tulihuzunika sana mioyoni na kukata tamaa. Tulifika hatua ya kuhuzunika mioyoni tukisema kwanini nchi yetu anapotokea kiongozi mwenye maono mazuri hutokea tukio na kuharibu hayo maono, mfano mwalimu alipambana kuleta maendeleo lakini vita ya Uganda ikaharibu uchumi wetu, kaja wewe korona inataka kututoa kwenye maono, lakini Mungu alisikia huzuni zetu akaponya uchumi wetu baada ya kumtanguliza wewe katika maombi.

Tunashukuru kwa hili, Ila kuna hii aja yako ya kufufua sekta ya uvuvi kwa kununua meli mpya, hilo sisi wananchi wa chini tunakushukuru sana lakini kwetu sisi wananchi wa chini tulikua na ombi moja, ufufuaji wa sekta ya uvuvi uende sambamba na ulinzi na usalama wa uvuvi haramu.

Mh. Rais kwa sasa kuna haja ya kuanzisha jeshi la viumbe maji kama ilivyo kwa TANAPA wanavyopambana na wawindaji haramu wa wanyama, ukianzisha jeshi la viumbe maji yani water bodies force kuna faida kubwa sana.1 Samaki watapatikana kwa wingi hivyo maono yako yatakua yamefanikiwa, 2. Utakua umetusaidia sisi wavuvi ulinzi wa Mali zetu tukiwa ziwani na baharini . Viwanda havitakosa Mali ghafi .
 
Utakuta umekopa benki umenunua machine zako za uvuvi, ukipeleka ziwani unawapelekea majambazi siku mbili wanachukua hivyo pakianzishwa jeshi la viumbe maji, wanakua wanafanya ulinzi na usalama katika maziwa yetu na bahari basi litakua jambo jema uvuvi haramu utakoma
 
Back
Top Bottom