Rais Magufuli: Uchumi mzuri ni pamoja na kuwa hela ngumu kuipata; kizuri hakipatikani hovyo hovyo

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
48,776
102,136
“Ninapowaeleza kuwa uchumi wetu ni mzuri, ni mzuri kweli kuwa na uchumi mzuri hauna maana kuwa na mahela umeyajaza chumbani. Uchumi ni pamoja na kuwa na hela ngumu kuipata, kizuri hakipatikani hovyo hovyo, ni lazima utoe jasho. Nilikuwa nazungumza juzi pale Mwanza kuwa bajeti ya Afya imepanda kutoka bilioni 31 hadi bilioni 269 na Tanzania tukapewa nafasi ya kuuza madawa katika nchi zote za SADC.“amesema Rais Magufuli Tarehe 6 Novemba 2017 mkoani Kagera wakati wa ufunguzi wa mradi wa wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba, mkoani Kagera.

Chanzo: Bongo 5
 
Ni sawa kabisa upungufu wa hela husababisha thamani ya hela kupanda...

Sawa ,sasa kama haionekani Mtaani ndio tunakuwa tumefanya nini ?..

Kwani hakuna namna nyingine ya kuipa thamani pesa yetu ?.
 
Alifafanua alichomaanisha.
Uchumi mzuri sio kuwa na access ya pesa bila kazi. Pesa zinakuwa ngumu kwa maana ya upatikanaji wake unahitaji kufanya kazi halali kwa bidii na kwa kufanya hivyo uchumi unakua
Kazi halali huku wengine waki-free ride?
Vipi kuhusu purchasing power kupungua? Vipi kuhusu mfumuko wa bei na vitu kuwa ghali?
 
alifafanua alichomaanisha.
uchumi mzuri sio kuwa na access ya pesa bila kazi.
pesa zinakuwa ngumu kwa maana ya upatikanaji wake unahitaji kufanya kazi halali kwa bidii, na kwa kufanya hivyo uchumi unakua.
Uchumi haushikwi na pesa halali tuu ata haramu pia... Zinafanya mambo...
 
Kazi halali huku wengine waki-free ride?
Vipi kuhusu purchasing power kupungua? Vipi kuhusu mfumuko wa bei na vitu kuwa ghali?
hayo ni matatizo mengine...
ila vile ndivyo nilivyomuelewa...
wapi hao wanao free-ride...
kupungua inaweza kuwa kweli kwa sababu pesa nyingi zinapelekwa kwenye econimic stimulators (miradi mikubwa) na upungufu wa pesa haramu mitaaani. system itakapokaa sawa kunakuwa na purchasing power nzuri tu ambayo ni product ya kazi halali na sio halali mchanganyiko na ujanjaujanja.
 
alifafanua alichomaanisha.
uchumi mzuri sio kuwa na access ya pesa bila kazi.
pesa zinakuwa ngumu kwa maana ya upatikanaji wake unahitaji kufanya kazi halali kwa bidii, na kwa kufanya hivyo uchumi unakua.
NMB nao hawafanyi kazi?

Wanaopunguzwa kazi kila kukicha hawafanyi kazi?

Wanaolima na mazao yao yanakosa soko na kuharibika nao hawafanyi kazi?!

Mmevuruga kanuni za uchumi sasa mnaleta vioja.
 
Enzi naanza kuelewa mambo sh 5 ilikuwa inanunua dola moja na ndio maana ya sh 5 kuitwa dala. Sh 20 ilikuwa inanunua paundi moja ya Uingereza na ndio sababu ya sh 20 kuitwa paundi enzi hizo. Serikali ya CCM kwa uzembe na ufisadi wake imetufikisha mahali sh 2500 inanunua dola moja. Sasa bila aibu wanatuambia uchumi mzuri ni ugumu wa hela kupatikana badala ya kusema bayana madhara waliyotusababishia kwa kutufanya tutafute mishilingi mingi ili kuipata dola moja kwa sera zao mbovu na ufisadi
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom