kikoozi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2015
- 2,030
- 2,923
Habari Mh rais Dr John Pombe Joseph Magufuli, Pole kwa majukumu mazito ya nchi kwa maana ya kitaifa na kimataifa kwa ujumla.
Awali ya yote tunatoa pongezi za dhati kabisa kwa serikali yako ya awamu ya tano, chini ya uongozi wako kwa kazi nzuri ulizozifanya na unazoendelea kuzifanya katika kuliletea maendeleo taifa letu, tunaona miradi mikubwa ya kimaendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo usafirishaji na uchukuzi kama vile ufufuaji wa shirika letu la ndege ATCL ikiambatana na ununuzi wa ndege mpya kabisa.
Ujenzi wa reli mpya kabisa ya umeme (SGR), uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara kuunganisha mkoa na mkoa na kurahisisha mawasiliano,ujenzi wa barabara za juu (flyovers), Upitiaji upya wa mikataba na uboreshwaji wa sheria za madini hii ni kuhakikisha tunalinda rasilimali zetu na kunufaika kama nchi, mradi wa usambazaji wa umeme vijijini REA kupitia wizara ya nishati, haya ni machache tu katika yale mengi unayoyafanya.
Dhamira yako ya dhati na hulka ya kujitoa bila kujali hali hii inadhihirisha kua wewe ni mzalendo wa kweli.
Dhumuni kuu la andishi langu hapa JamiiForums ni kukuomba Mh rais sisi vijana ambao wengi wetu ni wasomi wa vyuo vikuu hapa nchini mabao tupo kwenye mradi huu wa SGR tunaomba usitusahau Mh rais tunakuomba sana sana utusaidie kupata ajira endapo mradi huu utakamilika, mradi huu umebeba vijana wadogo wenye taaluma mbalimbali, kuna ma engineer, wataalam wa technolojia (IT), Telecommunication, Electrical etc.. etc..
Siku yoyote ile utakapotembelea mradi huu au kuja kuuzindua baada ya kukamilika tunaomba utoe neno lolote jema ambalo litaenda kutuponya sisi vijana tuliopo kwenye mradi huu
Tuna kutakia kazi njema na afya njema baba yetu kipenzi na raisi wetu mpendwa Dr John Pombe Joseph Magufuli
Mungu ibariki Tanzania.