Rais Magufuli tupia macho waliolipwa fidia kupisha ujenzi wa bandari Bagamoyo kuna ufisadi mkubwa

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
6,390
2,000
Serekali inabidi utupie macho waliolipwa fidia kupisha ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo maeneo ya mlingotini kwani kumekuwa na ufisadi mkubwa.

Pamoja na kuwa baadhi ya watumishi wahalmashauri ya Bagamoyo mtathimini wa ardhi na mtumishi mmoja wa chuo kikuu cha ardhi walioshirikiana na halmashauri ya Bagomoyo kufanya tathimini ya fidia kuhojiwa na TAKUKURU bado waliolipwa fidia feki ya mamilioni hawajaguswa mpaka sasa na mtaani wanatamba.

Hata hivyo watumishi hao wamekuwa wakitumia hela waliojichotea kuhakikisha wanashinda kesi hiyo.

Kuna zaidi ya majina feki zaidi ya 100 yalioingizwa kwenye kulipwa fidia lakini baada ya kulipwa waligawana fedha hizo na watumishi wa halmashauri ya Bagamoyo ardhi.

Na jambo la kushangaza ni kuwa wale ambao walipaswa kulipwa kihalili walipwa fedha kidogo tofauti na walewaliingizwa kinyemela wengine walipwa zaidi ya bilioni moja.

Watumishi hao walitumia mchezo mchafu kwa kuweka picha ya mtu mbele ya jengo ambalo lipo sehemu tofauti na maeneo yayopaswa kulipwa fidia ili waweze kujipatia hela kwa njia ya udanganyifu.

Pamoja na kwamba rais Magufuli alifanya ziara Bagamoyo lakini hakulizungumzia ingawa baadhi ya wananchi walilipwa fidia kiduchu walishapeleka malalamiko yao kwa waziri mkuu hata hivyo hakuna kilichofanyika mpaka sasa.

Ni vema sasa serekali ikawachukulia hatu wale wote wsliohusika nabufisadi huu.

Ni vema sasa serakali ikahakisha watu hawa wabachukuliwa hatua mara moja.
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,944
2,000
Halafu mwisho wasiku watu wakishawekeza mnaanza kuwasumbua kwa uzembe kama huu wa watu wetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom