Rais Magufuli tunusuru vijana wako tunapitia kipindi kigumu

Tuvilaumu vyuo vyetu kwa kuzalisha matatizo. Vyuo vinajua kabisa kuwa baada ya nchi kuingia kwenye SAP serikali ilijitoa kuwa mwajiri mkuu. Wao badala ya kudahili wanafunzi kwenye program zisizolazimisha ajira serikalini kila siku wanaongeza udahili kwenye kozi hizo hizo. Vyuo vikuu vilazimishwe kubuni program zinazofaa kwa vijana wetu kulingana na mahitaji ya sasa. Program za ualimu zipunguziwe wanafunzi.
Serikali haiwezi kupunguza idadi ya Ufahili katika kada ya ualimu, kwasababu bado walimu hawatoshi nchini, kilichopo ni serikali kutokuwa na msuli wa kutosha wa kuajili, pia na upungufu wa sector binafsi. Kutokana na uchumi kubana.
 
Ninataka kuwaambia vijana wenzangu ambao kwakias flani mumeshupaza shingo zenu mkisubir ajira chini ya jemedar stone. Hakika umasikin wa kutupwa unawasubiri. Mm ni mhanga wa hizo ajira tangu 2015 ila nilipomaliza nilikaa miez 3 maskan nikaaga nilianza kupanga mtaan chumba ya elfu 20, mkoan nikasugua mwaka nikaona huu utani nikakata tiket nikajitosa Dar jiji linampokea yyote yule nikachukua vyet nikaweka chini ya uvungu nimehangaika sana ila mpaka ninaandika hapa mm ninasikia mtaan wakisema mshua kapita nipo kwangu nyumba yangu kiwanja kubwa square mita 1100 maenea ka bunju sasa ninajua shida ipo ila sahau kuhusu ajira utanishukuru baadae. Wasalamu.
Asante , member muongo!

Na iwe ivo.
 
Mie pia tatizo hili limenikumba ni mwalimu niliyehitimu SAUT ya Mwanza mwaka 2016,hili tatizo lilipoanza kutokea mwaka 2015 nilikuwa nasoma huku nawaza nikimaliza naenda kukabiliana nalo vipi kitaani ila sikuweza kupata majibu ya moja kwa moja cz unakuwa frustrated sana,baada ya kuhitimu nilikaa nyumbani kama miezi 3 hivi hali ikiwa ni mbaya sana mpaka ikafikia hatua hadi hela ya vocha au kuangalizia mpira naomba kwa mama au wadogo zangu kiukwl nilikuwa naumia sana
Kuna siku nimekaa gheto usingizi haukuja kabisa nikiwaza hii hali mpka lini?,ndipo hapo nilipoamua kujipa ujasiri wa kuingia kitaa kupambana na kuweke vyeti vyangu kabatini,kuacha kuona aibu kwa jamii kwamba itanionaje msomi mzima nafanya kazi za namna hii.
Ndugu zangu niliamua kutafuta fani ambayo ni fundi umeme wa majumbani,jamaa niliyempata wa kunifundisha alikuwa mwanafunzi mwenzangu aliferi form 4 akawa ndo boss wangu kuanzia hapo,nikawa saidia fundi kwa namna moja au nyingine wakati huo naendelea kujifunza
Baada ya miaka 2 hivi nikiwa na idea tayari ya ufundi umeme nikaamua kujifunza ufundi bomba(plumbing) ,mpaka sasa nimeiva napata site zangu maisha yanasonga siwazi tena ajira za magufuli cz nw naingiza fedha zinazokidhi mahitaji yangu na familia yangu sina stress tena
Ndugu zangu wasomi tuache kudharau kazi cz unaweza ukaona kazi flani ni za kijinga kumbe watu wanapiga hela nyingi sana kwenye hizo kama hasa kazi za ufundi like kujenga,ufundi umeme,welding etc,
Mwisho kama unaona hauna mtaji,wala hauna connection yoyote ya kukupatia ajira nakushauri tafuta fani(ujuzi)wowote utakusaidia sana nyakati hizi tulizonazo hauta kufa njaa popote uendapo
 
Akaishi wapi mkuu, atafikia wapi, Kodi ataliapaje, kula je? Madawa nk...mkuu yataka moyo Sana

Basi mpe mbinu aanzaje

Yeye atoke tu nyumbani hapo ndio pakuanzia.

Kula
Kulala
Huduma

Hivi vitu vitatu atavitafuta akishatoka nyumbani. Tofauti na hapo hakuna namna atulie
 
Tuvilaumu vyuo vyetu kwa kuzalisha matatizo. Vyuo vinajua kabisa kuwa baada ya nchi kuingia kwenye SAP serikali ilijitoa kuwa mwajiri mkuu. Wao badala ya kudahili wanafunzi kwenye program zisizolazimisha ajira serikalini kila siku wanaongeza udahili kwenye kozi hizo hizo. Vyuo vikuu vilazimishwe kubuni program zinazofaa kwa vijana wetu kulingana na mahitaji ya sasa. Program za ualimu zipunguziwe wanafunzi.
Una point ya muhimu sana bro.
 
Nipe Siri mkuu, maana nimefanya michongo mingi imefeli, napata hela ya kusurvive tu! Dah! Nikiri tu nlisoma ili niajiriwe niweze kujiajiri, Mana mtaji pia ni vigumu Sana kupata

rahisi sana, engange na watu waliofanikiwa one to one! but make sure your willing to sacrifice yourself
 
Mm nahis kutwambia kuna awamu imebak ya ajira 5k n gia ya kututuliza baada ya watu kugundua maovyo ovyo kwenye zile wanazosema ni awamu ya kwanza. Mkuu trust me hizo 5000 tutaambiwa tuombe tena mwakani miez ya 5/6/7. Na watafanya hivo ili waseme tulikuwa tunalekebisha mfumo wetu wa ajira ambazo et ni za kuchaguliwa automatic not manual 🤭🤭🤭, hi cell call ni hatari mkuu.
Kwa madudu yaliyo ibuliwa sina hamu tena na database bora kuomba upya mkuu
 
Kuna watu wanaongea kirahisi humu nadhani hawajui wanachokipitia vijana wenzao.
Hao ni wachache kati ya wengi wanaofurahia hizi shida tunazopitia! Kuna mwingine hadi alidiriki kunitamkia kwamba Magufuri asiendelee kuwaajiri hivo hivo ili tulingane maana mlijifanya kuipenda sana shule sasa mtaa umewapenda zaidi!

ila yote kwa yote naamini ni mapitio tu tunapita ipo siku yatakwisha!
 
Back
Top Bottom