Binti Msichana
Senior Member
- Oct 9, 2016
- 109
- 247
Hakuna ubishi Rais John Pombe Magufuli ni rais Watanzania tulikuwa tunamsubiri kwa muda mrefu.Rais huyu anakosa usingizi kwa kufikiria jinsi gani alivushe Taifa la Tanzania kuelekea kwenye maisha bora na maendeleo ya hali ya juu.
Amekuwa akifanya kila liwezekanalo kutuletea maendeleo Watanzania.Jitihada zake za kupambana na uovu wa kila aina na kunyosha Tanzania ni za kuungwa mkono na kila Mtanzania.
Wapiga dili serikalini na wanaojipatia kipato kwa njia haramu katika serikali ya John Pombe Magufuli hawana nafasi.
Kwa muda mfupi JPM amedhibiti rushwa , ufisadi, ukwepaji kodi, madawa ya kulevya, matumizi holela ya serikali pamoja na uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
Kubwa zaidi JPM amefanikiwa kusimamia urejeshaji wa mikopo ya wanufaika wa elimu ya juu iliyotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kwa mwezi wa February, hakika pesa iliyorudishwa kwa mwezi wa February haijawahi tokea.Ila namlaumu kitu kimoja , amesaini sheria inayodhoofisha urejeshaji wa mikopo kwa makato ya 15% , ingebidi makato yawe hata 30% ya mshahara...
Bunge lirekebishe sheria hii makato yawe walau 30% ili nchi iweze kusomesha vijana wengi zaidi ukizingatia kwa sasa serikali haina pesa , pesa za misaada za wahisani pamoja na mikopo zimepungua kwa kiasi kikubwa.
Hata wewe mtumishi unayekatwa na bodi ya mikopo 15 % usikae na kuilaumu serikali fikiria wadogo zako wanaosomeshwa na pesa hizi kwa mustakabali wa Taifa.