Rais Magufuli tunaomba Wizara ya Utumishi uitolee mamlaka ya kutoa ajira tangu sasa

mzee wa giningi

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
519
336
Mhe .rais magufuli nichukue fursa hii kukupongeza kwa juhudi zako za kupambana na ufisadi na rushwa nchi nzima nakupa hongera .

Nichukue fursa hii ya pekee kukuomba kwamba wiazara ya utumishi wa umma na utawala bora kuitolea jukumu la kutangaza ajira na kutoa ajira maana kwa sasa hawafanyi kazi hiyo mbali unaifanya wewe mwenye mfano ,Jana kuna vijana wanne walienda utumishi wa umma ofisini kwenda kuulizia hatima ya ajira zao walioajiriwa mwezi June 2016 na walipewa mikataba na walipewa pesa za kujikimu wakiwemo vijana walioajiriwa na mahakama ya Tanzania kama mahakimu nk ni miongoni mwa vijana 3000 walioajiriwa mwaka Jana na kusitishiwa ajira zao walipofika ofisini walikutana na mkurugenzi wa utumishi wa umma aliwajibu kuwa swala la hao vijana limeshugulikiwa limekamilika kwa ngazi ya utumishi wanasubiri tamko au ruhusa kutoka kwa rais magufuli atoe kibali kuwa warudi au laa kwa kutumia mfano huu wa jana ni wazi kuwa sasa hivi ajira hazitolewi na wizara ya utumishi wa umma mbali mpaka rais magufuli atoe kibali.

Kufatana na hilo namuomba rais wetu akihamishe hicho kitengo cha ajira kukirudisha kiwe kitengo cha ikulu ili ajira ziwe zinatangazwa ikulu .
 
Kufuatia yaliyomkuta Mramba wa TANESCO kwa kupandisha bei za umeme. Hakuna atakayekubali kupoteza nafasi yake kisa kukutangazia wewe ajira. Kuweni wapole hadi hapo Sizonje atakapomaliza mambo yake na itokee akumbuke mwenyewe kuwa kuna watu hawajaajiriwa.
 
Back
Top Bottom