Rais Magufuli tunaomba utengue uteuzi wa mawaziri hawa

joshydama

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,623
5,037
Habari wana Jf. Ni matumaini yangu kuwa hamjambo na mnaendelea vyema kabisa katika ujenzi wa taifa letu.

Ndugu zangu wanabodi, leongo kubwa la hili bandiko ni kwamba tupige kelele sana ili hawa mawaziri watumbuliwe kwani hawana tija katika jamii/ utendaji kazi wao ni wa hovyo sana.

Ndugu wanabodi napenda kuwataja hao Mawziri kama ifuatavyo.

1. Waziri wa Mambo ya Ndani(Lugola)
Huyu hapa katika utendaji wake amethibitisha kushindwa kuilinda jamii na mali zao. Hivyo imekuwa ni tatizo kwa Wananchi kwa sababu wananchi wanatekwa, wanapigwa risasi hovyo na wengine wanauliwa kabisa mfano mzuri ni MO, MDUDu, n.k. Pamoja na hayo yote hakuna hata jitihada zozote alizofanya kuhakikisha haya matukio ya ajabu yanaisha nchini.

2. Profesa Kabudi Palamagamba
Huyu ni Waziri ambaye mwenye maneno mengi sana ila vitendo sifuri. Hivyo, sisi kama wananchi tunahitaji vitendo na siyo maneno ambayo hayana tija katika jamii. Mfano sakata la kuaibisha wasomi hasa wa kada ya sheria ni Jambo la ajabu sana ambalo lingesababisha uteuzi wake kutenguliwa kwa sababu hakuwa na nia nzuri kwa jamii nzima bali kukatisha tamaa na kuleta fedheha kwa wanachi wa Tanzania hasa vijana wetu waliopo vyuoni, shuleni n.k.

Nawaombeni sana wanabodi mtoe ushirikiano ili hao mawaziri watenguliwe haraka kwa maslahi mapana ya nchi yetu.Pia mwanabodi mwenzangu kama una orodha yako ya Mawaziri wa hovyo ambao ungependa uteuzi wao utenguliwe naomba uwataje hapo chini ili Mh. Rais awashughulikie ipasavyo.

NB: Sina chuki hata kidogo na hawa Mawaziri bali uwezo wao mdogo unaonekana wazi katika utendaji na jamii inawatambua kwa namna walivyoshindwa kutenda wajibu wao.

Ahsante sana Wanabodi na karibuni kwa Michango . yenu. kumbuka ni haki yetu ya kikatiba katika kutoa maoni na n.k
 
kuna mambo hata mimi rais huwa ananipa mashaka utendaji wake,kuacha mtu kama kangi kazini aisee ni zaidi ya kivuruga watu.
Inasikitisha sana Mkuu. Huenda Mh. Rais anatafuta mtu ambaye atakuwa mbadala wake.
 
Huyu waziri mwakyembe ila ana uwalakini jamani, kuacha waraka unamkejeli raisi utolewe kwenye magazeti kabisa, halafu anajidai kuiingilia sana TFF huku akiacha kabisa michezo mingine ikifa. Huyu kwa kweli hapana asee
 
Dah jf watu wana midomo michafu,.. wakianza kuombea utumbuliwaji lazma liwapate waliotajwa. Mifano ni mingi waliotajwa humu na wakapigwa chini kweli. Sijui wengi humu ni kina Mshana?
 
Waraka UPI umemkejeli Rais wetu? Au wewe ndo una mkejeli?
 
Dah jf watu wana midomo michafu,.. wakianza kuombea utumbuliwaji lazma liwapate waliotajwa. Mifano ni mingi waliotajwa humu na wakapigwa chini kweli. Sijui wengi humu ni kina Mshana?
Makonda , Gambo, Hapi wameanza kusemwa lini? ndio ujue Rais haangalii maneno ya wenye chuki bali utendaji kazi wa mtu
 
Habari wana Jf. Ni matumaini yangu kuwa hamjambo na mnaendelea vyema kabisa katika ujenzi wa taifa letu.

Ndugu zangu wanabodi, leongo kubwa la hili bandiko ni kwamba tupige kelele sana ili hawa mawaziri watumbuliwe kwani hawana tija katika jamii/ utendaji kazi wao ni wa hovyo sana.

Ndugu wanabodi napenda kuwataja hao Mawziri kama ifuatavyo.

1. Waziri wa Mambo ya Ndani(Lugola)
Huyu hapa katika utendaji wake amethibitisha kushindwa kuilinda jamii na mali zao. Hivyo imekuwa ni tatizo kwa Wananchi kwa sababu wananchi wanatekwa, wanapigwa risasi hovyo na wengine wanauliwa kabisa mfano mzuri ni MO, MDUDu, n.k. Pamoja na hayo yote hakuna hata jitihada zozote alizofanya kuhakikisha haya matukio ya ajabu yanaisha nchini.

2. Profesa Kabudi Palamagamba
Huyu ni Waziri ambaye mwenye maneno mengi sana ila vitendo sifuri. Hivyo, sisi kama wananchi tunahitaji vitendo na siyo maneno ambayo hayana tija katika jamii. Mfano sakata la kuaibisha wasomi hasa wa kada ya sheria ni Jambo la ajabu sana ambalo lingesababisha uteuzi wake kutenguliwa kwa sababu hakuwa na nia nzuri kwa jamii nzima bali kukatisha tamaa na kuleta fedheha kwa wanachi wa Tanzania hasa vijana wetu waliopo vyuoni, shuleni n.k.

Nawaombeni sana wanabodi mtoe ushirikiano ili hao mawaziri watenguliwe haraka kwa maslahi mapana ya nchi yetu.Pia mwanabodi mwenzangu kama una orodha yako ya Mawaziri wa hovyo ambao ungependa uteuzi wao utenguliwe naomba uwataje hapo chini ili Mh. Rais awashughulikie ipasavyo.

NB: Sina chuki hata kidogo na hawa Mawaziri bali uwezo wao mdogo unaonekana wazi katika utendaji na jamii inawatambua kwa namna walivyoshindwa kutenda wajibu wao.

Ahsante sana Wanabodi na karibuni kwa Michango . yenu. kumbuka ni haki yetu ya kikatiba katika kutoa maoni na n.k

Sikubaliani kabisa na hoja yako...mawaziri hao wote wawili wanafanya kazi nzuri kabisa...Ila Lugola ameniudhi mambo mawili moja ni ...kuruhusu magari kwa maana ya mabasi kutembea usiku..La pili ni 'kuruhusu' polisi trafiki kuchukua rushwa .kwa mfano barabara ya Morogoro na hasa karibu na Kibamba kwenye kituo cha kwa Mangi trafiki asubuhi wanakula rushwa hadharani kwa kusimamisha daladala na magari mengine kwenye kajilima na kupokea rushwa za elfu tanompaka elfu kumi...hovyo kabisa trafiki wale
 
Katika hili baraza la mawaziri na manaibu wao ni Jafo peke yake. Wengine wote akiwemo Mwenyekiti, makamu na wajumbe wake hakuna aliyeonyesha ana tija kwa wananchi
 
Back
Top Bottom