Rais Magufuli,tunakuwa sugu. Urais wako 'hautanoga' tena!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Utamu wa Urais ni kuheshimiwa,kusikilizwa na kuungwa mkono. Urais haupaswi kuogopwa kama ukoma. Urais unapaswa kupendwa,kulindwa na kujivunia. Na Rais anapaswa kuendana na hayo.

Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM,umejipambanua na hulka yako ya kusema ukweli. Unatuambia ukweli toka moyoni mwako na vile unavyoamini. Lakini,ukweli wako unavuka mipaka ya kusikilizika. Ukweli wako hujaa vitisho,'utani',ubabe na ahadi za kikampeni wakati wanasiasa wengine umewaweka pembeni hadi 2020.

Ukweli wako unatufanya tuwe sugu. Tunakuwa sugu na mikwara yako ya kufuta au kuondoa;mikwara yako ya kuzuia au kubomoa. Tunakuwa sugu na kauli zako za kuchoma bila huruma na kushona. Tunakuwa sugu na kusikia kilekile kutoka kwa yuleyule. Urais wako utapoteza ladha.

Tutakuzoea kwa matendo na maneno yako. Tutakuona wa kawaida. Rais hapaswi kuwa kama wengine. Wewe ni mtu wa kipekee,ndiye mboni na alama yetu. Usitufanye tuwe sugu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Siyo hayo tu atadharaulika pia na ninahisi amekwisha dharaulika na watanzania wengi tayari.Kwa sababu ya makelele,kujiona,na upendeleo wa dhahiri
 
Adharaulike mara ngapi Mkuu!? Issues za Lugumi, rushwa kwa Wabunge wa CCM, kudharau katiba na Bunge, kukurupuka, uongo wake mbali mbali na hili la Bashite vimemuharibia sana credibility na reputation kama Kiongozi wa nchi.

Umemaliza Mkuu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Pamoja na kujinasibu mkweli na na mpenzi wa Mungu,kuna mambo anayafumbia macho hata kipofu anaona na hili linakera na kutia doa yale anayosemea ukweli!
 
Back
Top Bottom